Andy Chande hakustahili kuitwa "Sir", wakati George Kahama alistahili kuitwa "Sir"

Paschal Matubi

JF-Expert Member
Sep 15, 2008
235
303
SOURCE: ARTICLE
AUTHOR: JOSEPH
GAZETI: RAIA MWEMA, April 07, 2017, uk. 16
WEBSITE: (www.raiamwema.co.tz/kwa-nini-george-kahama-aliitwa-sir)

- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
RAIS Julius Nyerere aliheshimiwa kwa kuitwa “Mwalimu” wakati wenzake serikalini na bungeni kila mmoja aliitwa “ndugu”. Ilikuwaje hayati George Kahama aliyefariki mwezi uliopita, akaitwa “Sir”.

Si rahisi kuijua heshima ya “Sir” bila kujua historia ya Ulaya, hivyo nitaisimulia historia hii. Haijawahi kutokea utawala wowote kuogopwa na kutawala kama Roma ilivyoitawala duniani kwa miaka 507.

Lakini ilipofika mwaka 330, Constantine aliihamisha serikali ya Roma kwenda Constantinople. Moja ya sababu za kuhama ni serikali kushindwa katika kampeni ya kuwaua wakristo ili waache utii kwa dini yao kuzidi serikali.

Kuhama kwa Constantine, kukatoa fundisho kwa watawala wote duniani, askofu wa Roma akaheshimika, akaanza kuitwa “Papa” na hakuguswa tena na binadamu yeyote duniani hadi leo.

Binadamu wa aina hii, ambaye hakuna serikali duniani inayothubutu kumgusa, wala bunge lolote duniani kumtungia sheria wala mahakama yoyote duniani kumhukumu,tunasema huyo ni “sovereign” au ana “sovereignty”.

Tangu Constantine aukimbie mji wa Roma, Papa akatokea kuwa binadamu pekee ambaye ni kiongozi wa dini tu, lakini uongozi huo ndicho kitu pekee kilichomfanya awe na “sovereignty” hadi leo.

Kazi ya kumlinda “sovereign” ni yake binafsi ndiyo maana anaitwa “Comamnder in Chief” inayotafsiriwa kama “Amiri Jeshi Mkuu”. Ili kuimarisha ulinzi wake, “sovereign” huongeza watu kumsaidia kujilinda. Barani Ulaya walinzi wa “sovereign” hawakuwa wanajeshi, bali walikuwa ni wapiganaji walioitwa “knights”.

Moja ya tofauti kati ya “knight” na wanajeshi ni kwamba“knights” walimlinda“sovereign” kwa zamu yaani siku chache tu, hata siku arobaini tu kisha wanarudi kwenye jamii.

Heshima ya wakristo kwa Papa, ilifanya washindane kumpa ulinzi. Hivyo, wafalme wa Ulaya, walilazimika kuruhusu watu wao wakamlinde Papa.Walipofika huko kwa Papa, wakawa ni “knights” wa Papa.

Kanisa Katoliki lina mfumo wa kusajili vikundi vinavyoundwa na waumini wake, vikiwemo hivi vya “knights” wa Papa.

Kila kundi lililosajiliwa lina “amri” ambazo huwa "utaratibu” wa maisha yao. Utaratibu huo kwa kilatini huitwa “ordo”, kwa kiingereza unaitwa “order”. Hivyo, makundi ndani ya Kanisa Katoliki huitwa “order” na mengi kwa kirefu yanaanza na jina “Order of ….”.

Walioanza kuunda hizi “orders” ni“watawa” na vikundi vyao vinaitwa “Religious Orders”. Binafsi natatizwa na tafsiri inayotaja“order” hizi. Wengi huziita “mashirika" na baadhi huziita “jumuiya”, wengine “congregrasio”!

Hivyo, maneno mengi likiwemo hili “order” au “knight” ninayaandika humu jinsi yalivyo ili nisijitie ujuaji wa kutafsiri nikaishia kupotosha.

Ifuatayo ni mifano ya watu kwenye “orders” unazoweza kuzifahamu. Unapomtaja mtu unalazimika utaje mwishoni herufi za “order” yake. Mfumo huu wa kutaja hivi unaitwa “post nominal”.

Bernadetta Mbawala wa Songea alifariki akiwa kwenye “order” iitwayo “Order of Saint Benedict”, kwa kifupi inaitwa “OSB”.

Katika uhai wake jina lake liliandikwa “Sista Bernadetta Mbawala, OSB” na ndiye Mtanzania pekee aliyefaulu kuvuka ngazi ya jimbo na kufikia ngazi ya kujadiliwa pale Roma kuona uwezekano wa kumtangaza kuwa mtakatifu.

Jorge Mario Bergoglio alijiunga na “order” iitwayo “Society of Jesus”, au “Jesuits” na huandikwa “S. J.”, hivyo aliitwa “Jorge Mario Bergoglio, S.J.”, sasa anaitwa “Papa Francis”.

Jude Thadaeus, alijiunga na “order” iitwayo “Order of Friars Minor Capuchin” yaani “OFM. Cap” au “wakapuchini”, hivyo anaitwa “Jude Thadaeus, OFM. Cap”, ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Mwanza.

Eusebius Nzigilwa wa Dar es Salaam, alichagua iitwayo “Holy Orders” yaani upadri, ameshavuka madaraja yote ya “Holy Orders” na tangu Machi 19, 2010 ni “askofu wa Mozotcori”. Yeye na mapadri, wote wa majimbo huandikwa majina tu na si zile herufi za mwishoni.

Hivyo, tumeona kundi la masista na watawa likiitwa “religious orders”, wakati “Holy Orders” linajumuisha mashemasi hadi maaskofu. Je, George Kahama alijiunga na kundi gani?

Kabla ya kuona aina ya makundi ya akina George Kahama nalazimika kueleza kundi la walinzi wa Papa maalumu kutoka Switzerland. Kundi hili lilimlinda Papa tangu Januari 22, 1502 na hadi leo likiitwa“Pontifical Swiss Guard”.

Aina ya makundi kama alilojiunga George Kahama yanajulikana kama “Equestrian Orders”. Neno “Equestrian” linatokana na neno la kilatini “equus” likimaanisha “farasi” yaani wale “knights” walitumia farasi katika vita.

Makundi haya Pope Urban II aliyaunda kuanzia mwaka 1095 alipotangaza vita iliyoitwa “Crusades” ya wakristo barani Ulaya kuwafukuza waarabu nchini Israel waliopateka Jerusalem tangu mwaka 638.

Hadi leo, Papa hakuyafuta makundi yale, akaanzisha mengine ya kijamii na si ulinzi kama zamani.

Hivyo, hiki tunachokiita kupewa “order”, si kitendo cha kupewa lolote, tena wengine wanaita ni “kupewa “nishani””!

Kile ni kitendo cha kuingizwa na mkuu wa hiyo “order” kwenye “order” yake, kama ni ile ya “Jesuits” anaitwa “Superior General”, ile ya “wakapuchini” anaitwa “Minister General”.

Kiongozi wa “Equestrian Orders” anaitwa “Grand Master”.Jina la “order”aliyojiunga George Kahama ni “Pontifical Equestrian Order of St. Gregory the Great” iliyoanzishwa na Papa Gregory XVI mwaka 1831.

Madaraja ya wanawake ndani ya “order” hiyo ni“DSG”, “DCSG”, “DC*SG” na “GCSG”, wakati ya wanaume ni “KSG”, “KCSG”, “KC*SG” na “GCSG”.

Ingawa ofisi ya Papa haijaweka utaratibu maalumu wa kujiunga, mara nyingi kitendo cha kujiunga kinafanyika kwa askofu wa jimbo kupeleka Roma jina la mtu anayetaka kujiunga. Mwaka 1959, George Kahama alianza uwaziri serikalini, akahamia Dar es Salaam kutokea Bukoba.

Sheria za Kanisa Katoliki, ibara ya 102(2), yaani “Can. 102(1)”, zinamuelekeza muumini anayehama atimize miaka mitano ndipo ahesabike muumini wa jimbo jipya.

Mawasiliano mengi kwenda Roma hupitia kwa mwakilishi wa Papa. Mwakilishi wa Papa akilipata jina ndipo analipeleka kule Roma kwa “Cardinal Secretary”.

Roma wakikubali, wanatengeneza hati iitwayo “diploma” ambamo majina ya mwanzo ya mhusika yanatafsiriwa kwa kilatini. Hivyo, Clement George inaandikwa kilatini yaani “Clemente Georgius”.

Kinachofuata ni sherehe ya kumpatia mhusika “diploma” yake, yaani kumfanya sasa “George” awe ni “knight”.

Kitabu cha Joseph Kahama, kinaeleza sherehe hii kwa George Kahama ilifanyika jijini Dar es Salaam mwaka 1962 kanisani St. Joseph, ingawa sijui kwa nini haonyeshi tarehe wala mwezi :{Sir George, ISBN: 9787119062198, uk. viii}.

Kuna uwezekano mdogo kwamba “Askofu Edgar Maranta, OFM.Cap” ndiye alimpendekeza George Kahama kwani hakuwa ametimiza miaka mitano jimboni Dar es Salaam. Hivyo ni wazi kwamba Askofu Laurean Rugambwa wa Rutabo ndiye alimpendekeza kabla ya mwaka 1959.

Baada ya kuwa “knight”, je alistahili kuitwaje? Wengi wamekuwa wakimwita “Sir George Kahama”.

George Kahama aliingizwa ngazi ya “KCSG”. Hivyo, ulitakiwa kumwita “Sir George, KCSG”.Tumeona ndivyo hata askofu wa Mwanza unatakiwa kumwita yaani “Askofu Jude Thadaeus, OFM. Cap”.

Hayati George Kahama alikuwa ni mtanzania pekee aliyekuwa na haki ya kupita pale Vatican mbele ya kanisa la St. Peter akiwa amepanda farasi, kwa sababu alikuwa ni “Sir George, KCSG”.

Naamini makala hii imejibu swali “kwa nini George Kahama aliitwa “Sir””.

Sasa tuone nje ya Kanisa Katoliki mtindo wa“knight” unatumikaje. Ingawa Kanisa Katoliki halikuanzisha mfumo wa “knight” lilianzisha mfumo wa “order” nilioueleza humu.

Narudia, neno “order” lina nguvu sana kanisani na hata misa za wakatoliki huandikwa “Order of the Mass”, ukizihudhuria utaona jinsi zinavyoendeshwa kwa mpangilio maalumu.

Mataifa ya Ulaya yalipoliiga Kanisa Katoliki matumizi ya neno “order”, yakaweka “sovereigns” wao yaani wakuu wa mataifa hayo, wawe “Grand Master” wa “order” za mataifa yao.

Hivyo, duniani sasa zipo “order” za Papa kama alizowaingiza akina George Kahama na pia zipo za wakuu wa mataifa, tena karibu kila taifa lina “order” angalau moja.

Hata wewe unaweza kusimulia “order” ya taifa lolote, mimi humu nitaeleza ya Britain. Britain wanayo inayoitwa “Order of the British Empire” yaani “OBE”,ina madaraja yafuatayo, “MBE”, “OBE”, “CBE”, “DBE”, “KBE” na “GBE”.

Utaratibu wao ni tofauti, kwani wenzako wanaweza kukupendekeza na hata mwenyewe ukapendekeza uingizwe.

Malkia Elizabeth II aliwapa hadhi ya “knight” mwanamuziki “Elton John” na aliyekuwa meneja wa timu ya Manchester United, “Alex Ferguson”.

Hawa walipata ile ngazi ya “CBE”, hivyo unaweza kuwaita “Sir Elton” na “Sir Alex”, au kwa kirefu “Sir Elton John” na “Sir Alex Ferguson”, au “Sir Elton John, CBE” na “Sir Alex Ferguson, CBE”.

Ilifika mahala mataifa yakaanza kutoa hadhi ya “knight” hata kwa wasio wa taifa lao, na hata Kanisa Katoliki nalo sasa hutoa hadhi ya “knight” hata kwa wasio wakatoliki. Hadhi hii inapotolewa namna hii inaitwa “honorary knighthood”, yaani mtu amepewa "kwa heshima tu".

Wanaopata hadhi hii “kwa heshima tu” hawapaswi kuitwa “Sir” mfano ni Terry Wogan aliyekuwa mtangazaji wa BBC na raia wa Ireland. Malkia Elizabeth wa Britain alimpa hadhi ya “knight” Juni 11, 2005 katika ngazi ya “KBE”, hivyo hakuitwa “Sir” bali aliitwa tu “Terry Wogan, KBE”.

Baadaye Terry aliomba uraia wa Britain na alipopewa akawa na “uraia pacha” yaani wa Britain na Ireland alikotoka. Kitendo hiki cha kupata uraia wa Britain kikamfanya astahili kuitwa “Sir Terry Wogan, KBE” hadi kifo chake mwaka jana.

Malkia Elizabeth II pia aliwapa hadhi ya “knight” mmarekani Bill Gates na Mtanzania Jayantilal Keshavji Chande, maarufu kama “Andy Chande”. Wote Bill Gates na Andy Chande waliingizwa kwenye ngazi ya “KBE".

Hivyo ukiandika “Sir Bill Gates” au “Sir Andy Chande”, ni makosa makubwa, kwa sababu Bill Gates ni Mmarekani na “Andy Chande” ni Mtanzania.

Hivyo, hawa wawili hawaitwi “Sir”, bali wanaishia tu kuitwa “Bill Gates, KBE” na “Andy Chande, KBE”.

Hata Nelson Mandela, hakuwa Mtanzania, lakini Machi 07, 1990 “sovereignty” ya Tanzania ilimuingiza kwenye “order” iitwayo “Order of the Torch of Kilimanjaro of the Second Class”.

Vile vile “sovereignty” ya Tanzania inayo “order” yenye hadhi ya juu kupita zote iitwayo “Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere” ambayo hadi sasa wamo watu watatu tu yaani Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa walioingizwa kwenye hii “order” Desemba 09, 2011.

Nafahamu umelazimika kuelewa maneno “knight” na “order” ambayo hayakwepeki unapotaka mtu aelewe maana ya “Sir” kama ilivyotumika kwa hayati George Kahama.

Mwandishi wa makala haya Joseph Magata, ni msomaji wa Raia Mwema anapatikana 075-4710684, barua pepe: josephmagata@yahoo.com

Mhhh
Sijaelewa..yaani kuhamia Dar kutoka Bukoba ndio apewe u Sir ? Hapo umetupiga changa la macho.
Kahama alikua muumini mzuri wa kanisa katoliki na alitumika sana kuliunua kabla na baada ya uhuru. Alitumika pia baada ya uhuru kuwakilisha serikali huko vatican.....kwa ufupi mchango wake ndio ulomfanya kupewa heshima hio...
Na sir Chande amepewa heshima hiyo kwa mchango wake mkubwa kwa humanity kutoa ajira na charity zake kwa jamii.
Mchango wake ni mkubwa ambao kila rais wa nchi hii kuanzia Mwalimu mpaka Kikwete waliuthamini sana.
Hivyo mchango wake kwa jamii ukathaminiwa na Queen akampa heshima hio ya knight na kuwa Sir.
Mwandishi hakumpa haki yake Sir andy chande kwa vile ni muhindi.....
Ukiangalia u sir wa kahama ni ukereketwa wa udini...ila sir chande u sir wake unatokana na kusaidia jamii ya watanzania bila kujali kuwa yeye ni hindu
 
  • Thanks
Reactions: tz1
Mhhhh! Haya bana tutafanyaje sasa ni kumeza Kama ilivyoandikwa na Tabibu
 
Umeelewa nikuulize Maswali au ndio kuitikia tu usionekane kilaza?
You must be having a bad dreams old man. What time is it there?

It seems you have risen from deep sleep and you don't know what you type really.

Dumbass biiiiiiiitcch.
 
Chande alipewa jiyo hadhi na Malkia wa uingereza wanajuana wao kwenye mambo yao ya kupaa angani huko jinsi gani ni mtaalamu kwenye hayo mambo yao ya secret society mpaka kamwita hivo
 
Asantee
 
Makosa haya hufanyika bongo tu. Marekani wanaelewa, hukuti mtu anamwita Billy Gates eti "Sir Billy Gates", kila mmoja atakuona kituko.

Magazeti yote ya Jumanne yaliandika "Sir Andy Chande" kwenye headlines zao.

Wabongo muwe mnasoma muelewe maana ya mambo diniani.
 
Mhhh
Sijaelewa..yaani kuhamia Dar kutoka Bukoba ndio apewe u Sir ? Hapo umetupiga changa la macho.
Kahama alikua muumini mzuri wa kanisa katoliki na alitumika sana kuliunua kabla na baada ya uhuru. Alitumika pia baada ya uhuru kuwakilisha serikali huko vatican.....kwa ufupi mchango wake ndio ulomfanya kupewa heshima hio...
Na sir Chande amepewa heshima hiyo kwa mchango wake mkubwa kwa humanity kutoa ajira na charity zake kwa jamii.
Mchango wake ni mkubwa ambao kila rais wa nchi hii kuanzia Mwalimu mpaka Kikwete waliuthamini sana.
Hivyo mchango wake kwa jamii ukathaminiwa na Queen akampa heshima hio ya knight na kuwa Sir.
Mwandishi hakumpa haki yake Sir andy chande kwa vile ni muhindi.....
Ukiangalia u sir wa kahama ni ukereketwa wa udini...ila sir chande u sir wake unatokana na kusaidia jamii ya watanzania bila kujali kuwa yeye ni hindu

Mkuu, mbona vigezo vyako vimekaa kisharishari tu? Je, nchi zote duniani walioepeleka uwakilishi huko Vatican, George Kahama aliwazidi nini hao wawakilishi wenzake hadi yeye tu apewe "u-Sir" na wengine wote dunani wasipewe?

Acheni hoja zinazozalisha maswali zaidi yasiyojibika hata kwa unayeleta hoja?
 
Hata mimi kule Facebook wananiita 'Sir'.

Na pia mashuleni kwetu tulivyokuwa tunawaita Walimu wetu wa kiume 'Sir' tulikuwa tunakosea?
 
Mhhh
Sijaelewa.
Mkuu hapa ulipo sema "Sijaelewa .." ndio utakuwa umeshajijibu maswali yako yaliyofuata baada ya maneno niliyo kunukuu. Kwanini George Kahama aliitwa Sir George Kahama , na kwanini Andy Chande alikuwa hastahili kuitwa Sir Andy Chande. Nikusaidie tu hawa walipata order tofauti ambazo zina sheria na mashariti tofauti. Mmoja (George kahama) ni toka Vatican kwa Papa ambayo sheria na mashariti yake ni tofauti na ya mwenzie (Andy Chande) ambae alipewa na Malkia wa Uingereza yenye mashariti tofauti na ile ya kwanza. Wa kwanza hakupata kwa upendeleo kama unavyojaribu kutuaminisha, na yule wa pili alipewa order lakini kwa mashariti ya waliompa order haruhusiwi kuitwa Sir kwa sababu sio raia wa uingereza. Usiweke hisia zako za kisiasa au za kidini kwa vitu vilivyo na vigezo na mashariti yaliyo wazi kabisa. na mfano umepewa na mwandishi wa chapisho kuhusu yule raia wa Ireland aliepewa order sawa na Andy Chande ingawa alikuwa mzungu hakuitwa Sir hadi pale alipopata uraia wa Uingereza (UK). Jifunze kusoma na kuelewa habari (reading and comprehension of respective stories or articles).
 
...Hivyo ukiandika “Sir Bill Gates” au “Sir Andy Chande”, ni makosa makubwa, kwa sababu Bill Gates ni Mmarekani na “Andy Chande” ni Mtanzania.

Hivyo, hawa wawili hawaitwi “Sir”, bali wanaishia tu kuitwa “Bill Gates, KBE” na “Andy Chande, KBE”....

Acheni kujifanya wajuaji. Mbona Sir Dauda Kairaba Jawara ni Mgambia na sio Mwingereza?

"...Jawara was knighted by Queen Elizabeth II in 1966..."
 
  • Thanks
Reactions: OTG
Mnao support kuwa Andy Chande hakupaswa kuitwa "Sir" eti kwa kwasababu hakuwa mwingereza mtafakari vizuri maana hawa wahindi hawaaminiki unakuta mhindi bongo ana uraia hata wa nchi tatu na bado mkamuona ni mwenzenu kumbe anawachora tu
Hili nalo ni jibu zuri. Inaweza kuwa jamaa alikuwa na dual citizenship kwa siri.
 
  • Thanks
Reactions: OTG
Acheni kujifanya wajuaji. Mbona Sir Dauda Kairaba Jawara ni Mgambia na sio Mwingereza?

"...Jawara was knighted by Queen Elizabeth II in 1966..."

Mkuu,

Umefanya research lakini unatakiwa masahihisho kidogo tu.

Rais Dawda Jawara wa Gambia naye hapaswi kuitwa "Sir" kwa sababu na yeye amepewa "Honorary Knighthood" kwenye order nyingine kabisa iitwayo "Order of St Michael and St George" nayo ya hukohuko Uingereza lakini ni tofauti na "Order" ya Andy Chande na Billy Gates".

Hii "Order of St Michael and St George" aliyopewa Rais Dawda Jawara wa Gambia ndiyo ileile ambayo pia ilimpa "Sultan Jamshid wa Zanzibar" hadhi ileile na ndiyo maana wanaokosea kumwita Dawda Jawara kama "Sir Dawda Jawara" ndiyo walewale wanaokosea na kumwita sultan aliyepinduliwa Zanzibar kama "Sayyid Sir Jamshid bin Abdullah of Zanzibar".

Kinachoamua uitwe au usiitwe "Sir" ni masharti ya "Order" unayoipata. Maelezo mazuri ameyatoa Titicomb hapa chini.

Back
Top Bottom