Android Development


Option mbona ipo lakini hamna hata Sh. 100/= nliyowahi kuipata.


elfu 50 mbali sana hata sh. 500 sijawahi kupata.


Ntafanya hivyo kama itatokea project nyingine. Lakini mimi huwa sipendi kumsumbua mtu na vi-message vya kumwambia atoe mchango yani inakuwa kama kero hivi wakati mchango ni hiari.

Mimi uwa natoa pesa pale nnapoweza ila mostly uwa najitolea kushiriki kwa maarifa niliyonayo kama mchango wangu kwenye project husika

Mchango wako ni zaidi ya pesa!

====================
Ila kusema kweli kufanya kazi ambayo inakuchukua muda, pesa na afya yako halafu unapata 0 inakuwa ni UPUUZI hivi. Domain inalipiwa, hosting inalipiwa, muda nao ni pesa bado afya. Sasa hivi macho yangu ndo hivyo tena naona kama ukungu ukungu. Sasa ya nini kujiumiza kwa kufanya kazi ya namna hii. Ntajitahidi kutoa update ya ESE Dictionary na nadhani hii ndo itakuwa product yangu ya mwisho then ntajikita kwenye masomo na profession yangu ya kufundisha kiswahili na linguistics kwa wanafunzi wa sekondari!!
 
ticha Nyasiro umekuwa kama mimi nimeamua nivae clinical coat yangu niwe full time pharmacist ila hivi vitu haviepukiki. Tunafanya kutoka moyoni. Kuna majamaa yana degree za computer science ila hayajui hata kudecompile app iliyokwisha tengenezwa. Ukipata spea time maana wanafunzi nao nistress tu. Tutengenezee vitu motomoto
 
Last edited by a moderator:
Tatizo developers bongo wana ile kitu kichwani ati kuna "Genius Developers" ambaye anaweza standalone na akatoa kitu kikakubalika worldwide, huu ni uongo mtupu, watu wanadhani watakua Zuckernberg kirahisi tu wanakaa wanajifungia hawataki kushirikiana na developers wengine wala nini, Zuckernberg mwenyewe facebook aliandika na watu wengi... Nothing will go kama kila kitu kinafanywa hivo.. Na bado wana ile kitu ya kujionyesha ati "mi mkali wa code" ushindani wa kijinga huo, unadhani kwa nini hujaona app yoyote toka bongo ambayo ina angalau UI nzuri... u can do the code, the graphics, the trials kila kitu mwenyewe... no one does that
 

Kweli wabongo wagumu sana kwenye kila kitu. Kudonate ishu hata kushea idea ni ishu. Miaka iyo kuna jamaa alikataa kunifundisha basic za photoshop sasa sikuelewa kwann alikataa. Tatizo tunaweka pesa mbele. Wakati project kibao zinaenda kwa nguvu za wanaojitolea.
 
Yeah, kabisa, wakat niko darasa la 6 (2007) , Bro wangu aliyemaliza diploma ya IT alikataa katakata kunifundisha kutengeneza calculator kwa visual basic, nikasema poapoa, sikuelewa kwa nn lakini baadae nilishukuru kwa kufanya hvyo, maana ilinipa morali ya kujifunza mwenyewe, nipo form 5 now na ninafanya C++ na Basic, yy anabaki kushangaa tu... Hahahahah, Nothing is hard once u understand it!, kuhusu ishu ya Donations aisee, hii ni kwel kabisa, mm mwenyewe ningeachaga kale ka tool kangu (unlimited) kawe bure, nisingepata hata cent...
 
Nimepitia comments , watu wana idea nzuri, ninaamini watanzania wanaweza, imefika kipindi hata wakenya wanatafuta web developers, programmers kutoka tz, kitu cha muhimu ni kusaidiana tunapoface challenges, watanzania tuondokane na hii tabia ya kusubiri kufanyiwa kila kitu bila kuweka jitihada ndio inayo tuangusha. Put your efforts at least kulingana na uwezo wako, ukikwama ndio uombe msaada. Ninaamini pia wakati mwingine kwamba watu wakikubania ujuzi ndio wanakuchochea kujifunza na kujua zaidi.
 

You don't give up that easy!
Nashauri ujifunze lugha mbili ambazo ni 1. Cross Platform Desktop/Mobile (C++/Java) 2. Web apps (PHP?)
Zina future kuliko MS Centric. Kuna issue tunakuja nayo na tutaitangaza soon ya kuwaweka developers pamoja.
Tuombeane uzima tu!

Hope mambo yataenda vema.
Again don't give up bro!
 
Nyasiro usife moyo kaka one day one time mambo yatajipa

mbuyu nao ulinza kama mchicha waswahili wanasema



last time niliona una ACSEE Division calculator this time piga mishe TRA wana excel shit unaitumia kucalculate ushuru wa GARI nahisi hii ukiweka ktk codes nahisi ukipiga nao mishe waweza kukupa mpunga fulani ni wewe kutafuta connections



http://www.tra.go.tz/calculators/RSP LIST AND CALCULATOR - VERSION 18.xls



or



Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools



kazi kwako kaka tafuta bepari mmoja uone kama atakuunganisha na hii issue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…