Anayeweza kupambana vizuri na dawa za kulevya ni Serikali na si mtu mmoja

Mwene chungu

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
915
752
ac10fd083f63419c514ce4f6c0e77515.jpg

Makonda ajiuzulu kupisha uchunguzi,hata kama rais kasema we fanya kazi...

Nimekuwa nashindwa kuelewa dhana ya Makonda na dawa za kulevya,na wengi wanaomtetea mh.Makonda wanadai amepambana na madawa ya kulevya kuliko mtu mwingine yeyote kitu ambacho sio kweli,Yeye alitaja majina ya watu kadhaa walioshutumiwa kutumia,kusambaza au hata kujua wanao husika na madawa.

Na kwa bahati mbaya sana hadi sasa kati ya waliotajwa hakuna ambae mahakama nchini haithibitisha juu ya upatikanaji na hatia.

Na hii nadhani ni kwa sababu ya mbinu iliyotumika,haikulenga kutatua tatizo bali kudharirisha baadhi ya watu;wanaowachukia hao waliodharirishwa wameona kama Makonda amefanya kazi kubwa sana eti kutaja tu majina ya watu ambao hata mahakama imeshindwa kuthitlbitisha juu ya shutuma zao.

Zoezi hili lingekuwa na nia ya kuwakamata wauza madawa lingeenda kimyakimya ili mwishoni tuje tupewe mrejesho kuwa Mtu X amekamatwa ni mhusika wa madawa hata mahakama ithibitishe mim kwa hapo ningemuona Makonda "Noma"..

Wengi wetu kwa sasa tunamuona alifanya kazi kwa sababu aliwataja wahasimu wetu wa kisiasa;sawa na nyie ndio maana mkaona amefanya kazi nzuri(kwa kifupi ni sababu za kisiasa)ndio zinatufanya tuone tatizo la kutokuwa na vyet harisi ni dogo na wakat yeye pia ameshindwa kabisa kujitetea...

Yote kenda,kumi Je, kama makonda alichokifanya ni kizuri hii imemfanya yeye awe juu ya sheria?..

Mungu huwainua watu wanaowainua wenzao,lakini Pia huwaumbua wanoumbua wenzao,ndio maana sio kila mtu anaweza kufanya kazi hizi lazima awe ni mtu asie na MAWAA KWA JAMII.

JE , KUTOKUWA NA VYETI HARISI KUFAUATILIA MADAWA KUNAVIFANYA vigeuke kuwa VYETI HALISI?...

Inamaana serkali haina mtu mwingine kabisa anayeweza kufuatlia hili?...na kama yupo(wapo) kwanini makonda asijiuzulu kupisha uchunguzi wa shutuma zinazomkabili,akikutwa mtu safi arudi nadhan hio ndio dhana ya uwajibikaji...
 
Back
Top Bottom