Anaumbuka mtu mbele ya wakijiji

BJBM

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2011
Posts
664
Reaction score
606
Padre mmoja mzee alistaafu na wanaparokia walimfanyia sherehe kubwa ya kumuaga. Katika sherehe hiyo, mbunge wa eneo hilo alipangwa kutoa hotuba ya shukurani ya kumuaga padri huyo kwa niaba ya wanaparokia wote. Bahati mbaya, mbunge alichelewa kufika .... Mc akamwomba padri aseme machache wakati wanamsubiri mheshimiwa mbunge. Padri hakujipanga kusema kitu lakini kwa kujitahidi, aliongea:. "Wapendwa, naikumbuka sana siku nilipofika katika kanisa hili kwa mara yakwanza, ila nilipata mshangao siku nilipoanza kuungamisha. Mtu wa kwanza kabisa kumuungamisha alinishangaza sana." Akameza mate kisha akaendelea, "Mtu huyo alipokuja kuungama alisema amemwibia bosi wakeTV, amemwibia ndugu yake pesa za urithi, akiwa shuleni aliwahi kukojoa kitandani akamsingizia mwenzie, amezini na mke wa jirani yake, na pia alimlazimisha house girl wake kufanya nae mapenzi. Nikapata picha kuwa kumbe watu wa kanisa hili ndivyo walivyo, nikasikitika sana..... Lakini baadae nikakuta kumbe watu wa hapa ni wazuri sana na hawatendi dhambi mara kwa mara. Yule muumini wa kwanza aliyekuja kutubu alitaka kunifanya niwafikirie vibaya kumbe nyie ni watu wema. Yule alikua na dhambi zake mwenyewe..." Wakati Padri akiongea hayo mara Mheshimiwa Mbunge akawasili, Padri akakatisha maongezi na mbunge akaanza kuhutubia. Akaanza kwa kusema:-"Ndugu wapendwa, naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kwani nilikuwa na majukumu makubwa ya kiserikali.... Kisha akaendelea... "Pia ninayo furaha kubwa kwa kunipa nafasi hii kuhutubia kwa niaba yenu. Mimi nina bahati sana kwani Padri huyu alipokuja hapa, mimi ndiye nilikuwa muumini wa kwanza kabisa kwenda kutubu kwake..." Kanisa zima vicheko...!! Tunajifunza nini!?: Tujifunze kuwahi kwenye matukio kwani huwezi kujua umuhimu wa lililokupita.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…