Habari za mchana,
Nimezaa na kijana mmoja ambaye alinitelekeza toka niko mjamzito.Nilimove on na maisha yangu nikalea mimba haadi mtoto akazaliwa,hajawahi hudumia huyu mtoto tangu mimba hadi leo ana mwaka sasa.
Siwajui ndugu zake na wala kwao haijulikani kama hata ana mtoto kwani hajawahi hata mpeleka mtoto kwao,mtoto alipozaliwa nilimsihi amtaarifu japo mama yake aje kumwona mjukuu wake akakataa.
Leo nikiwa katika pilika za maisha nimekutana naye,baada ya salamu,akanambia nipe mtoto wangu au kama hutaki endelea kunilelea akikua nitakuja nikulipe gharama zako nimchukue,siko tayari kumpatia mwanangu kwani hakuna gaharama ya kufidia uzazi na malezi ya mwanangu.
Je inawezekana mtu kumnyanganya mtoto ambaye ulimtelekeza toka mimba? Nifanyeje?Nimetumia muda na rasilimali zangu kumlea mwanangu halafu leo mwanaume anakuja na kauli ya vitisho kutaka kuchukua mwanangu.