Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 873
Good manners are of more importance than Laws
GS ni hivyo tu kwa sasa
Nikiwa nimekaa nyumbani kwangu jana usiku nikifuatilia tamthlia ya Ruby mara nikapata mgeni.Mgeni huyu ni jirani yangu.Akaniomba nitoke nje ili tukaongelee huko.Akanileleza habari yake kwa kirefu.Kifupi ni kwamba yeye ni binti wa miaka 33 ana mtoto aliyemaliza darasa la saba mwaka jana na mtoto huyo amechaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza hapa jijini Dar es salaam.Anasema kwamba mtoto huyu baba yake alimkataa tangu akiwa mimba hovyo kwa kipindi cha miaka yote hii amekuwa akimtunza yeye mwenyewe.Yeye anafanya kazi za kubahatisha.Baada ya mtoto wake huyu kufaulu anahitaji mahitaji mbalimbali ya kumfanya aweze kwenda shule na yeye uwezo hana.Baada ya kutafakari kwa kina akaona bora amtafute mwanaume fulani aliyekuwa akimtongoza siku za nyuma kwa lengo la kuomba msaada wa fedha ili mwanae aende shule.Jamaa akampa masharti huyu dada kwamba kama anataka kumsadia ni lazima akubali afanye naye mapenzi.Mdada hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali..Anasema baada ya kufanya mapenzi na bwana huyu,bwana huyu akaingia mitini bila kumpa dada huyu ujira wake..Hivi sasa dada huyu ni mjamzito na jamaa hapokei kabisa simu za huyu dada..Dada huyu kanifuata jana na kutaka nimpe hela ili aende akatoe mimba kwani anadai hawezi kuzaa mtoto mwingine asiye na baba.Imani yangu ya dini hairuhusu kutoa mimba wala mimi mwenyewe kama mwanaharakati siungi mkono suala la kutoa mimba..Nimemkatalia kabisa,najua ujirani wetu uko mashakani..Niko njia panda.
weee braza genekai si umeaga wee na tukakwambia tutakumiss,april fool nini?Umefanya vizuri sana mama endelea kushauri asitoe kabisa!
weee braza genekai si umeaga wee na tukakwambia tutakumiss,april fool nini?
mwambie azae kisha na amgawe mtoto....................nafikiri kuna watu kadhaa wa kadhaa waliokuwa wanatafuta watoto hawana.
hii habari imekosa nguvu ya ushawishi. tena sioni kama mleta habari alihitaji kuileta jamnvini. nadhani huyo dada kama kweli alitaka kutoa mimba asingekwenda kuomba pesa ya kutolea mimba- angeweza hata kudanganya shida nyingine kwa mtoa maada, apate pesa, ili mimba itoke. pili huyu dada wakati anatafuta ada ya mtoto hakuwai kumfuata mtoa maada na kuomba pesa ya ada? au kama si ada basi hata kutaka ushauri wa nani wa kumkopa???. miaka 33, unamfuata mwanaume ambaye unasemaanakutongoza humtaki- kwanini umfuate ukiwa na shida?? ktk mazingira haya, kipi raisi kuomba ada kwa mtoa maada au kuombapesa ya kutoa mimba???.tena dada ana shughuli zake ndogondogo ktk hizo shughuli hakuna watu wengine anawajua isipokuwa huyo mwanamme?? nadhani kwanza kabisa dada asingekwenda kukopa kwa mtu ambae walitofautiana ki-msimamo. kama ni kweli basi kuna cha kujifunza kuoka kwa huyo mama.