Anaomba ushauri Tafadhari msaidieni

Anaomba ushauri Tafadhari msaidieni

Mtamile

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
2,838
Reaction score
1,274
Duh nimeisoma barua hii kwenye gazeti moja jamaa anaomba ushauri, kaandika hivi;

Aunty Fatu, tafadhali nipe ushauri katika hili tatizo langu. Mi nadhani mke wangu si muaminifu, anafanya kazi katikati ya jiji, huwa anachelewa kurudi nyumbani na kila siku anarudi na taxi, wiki iliyopita nilijaribu kugusa simu alikuwa mkali kwelikweli.

Ni kweli sijawahi kumuuliza kuhusu wasiwasi wangu, lakini jana nilamua kumfuatilia wakati anatoka kazini, nikajificha mahala ambapo ntamuona anapotoka kazini, kweli nikamuona anatoka na mwanaume mmoja simfahamu, wakapanda taxi nami nikawafuata na wakaishia kuingia kwenye gest moja pale Kinondoni, nikaona ni vizuri niangalie saa nijue ni saa ngapi wameingia mle kwani itanisaidia katika ushahidi wakati wa kesi hapo baadae, si ndio nikagundua saa yangu imesimama, saa hii ni Rolex na nilipewa na bosi wangu mzungu kazini alinunua kwao huko Uswisi, na ni expensive sana, sasa je, unanishauri nimrudishie bosi akaitengeneze kwao?

Au ninunue nyingine?
 
Me naona kama anapenda saa kuliko mke mwache akaitengeneze au kma vp akanunue au amrudishie boss wake ila mm cngesubiria mambo ya saa ilee wanaingia tu chumbani ndani ya dk3 nawatimbia humo humo
 
me naona kama anapenda saa kuliko mke mwache akaitengeneze au kma vp akanunue au amrudishie boss wake ila mm cngesubiria mambo ya saa ilee wanaingia tu chumbani ndani ya dk3 nawatimbia humo humo

kikubwa alichokuwa anataka kwanza ni saa ili ajue wametumia mda gani mle guest
 
Angeweka pose kama refaree afe akashughulikia saa ikishakuwa poa anawaambia waendelee ili arekodi muda umsaidie kwenye kesi, mi nadhani ingekuwa poa zaidi mkuu au we unaonaje.?
 
Duh nimeisoma barua hii kwenye gazeti moja jamaa anaomba ushauri, kaandika hivi;

Aunty Fatu, tafadhali nipe ushauri katika hili tatizo langu. Mi nadhani mke wangu si muaminifu, anafanya kazi katikati ya jiji, huwa anachelewa kurudi nyumbani na kila siku anarudi na taxi, wiki iliyopita nilijaribu kugusa simu alikuwa mkali kwelikweli. Ni kweli sijawahi kumuuliza kuhusu wasiwasi wangu, lakini jana nilamua kumfuatilia wakati anatoka kazini, nikajificha mahala ambapo ntamuona anapotoka kazini, kweli nikamuona anatoka na mwanaume mmoja simfahamu, wakapanda taxi nami nikawafuata na wakaishia kuingia kwenye gest moja pale Kinondoni, nikaona ni vizuri niangalie saa nijue ni saa ngapi wameingia mle kwani itanisaidia katika ushahidi wakati wa kesi hapo baadae, si ndio nikagundua saa yangu imesimama, saa hii ni Rolex na nilipewa na bosi wangu mzungu kazini alinunua kwao huko Uswisi, na ni expensive sana, sasa je, unanishauri nimrudishie bosi akaitengeneze kwao? au ninunue nyingine?

duh huyo alikuwa alipata zero kwenye pepa
 
Yaani hii kitu nimecheka san hadi ikabidi niwashirikishe wengine tena wazee waliokuwa karbu yangu ili nisionekane chizi kwa kucheka peke yangu, nao hawakusita kuvunja mbavu. Jamaa alivobadilika kutoka kwenye machungu ya mke ghafla kuikomalia saa yake! Imeniacha hoi sana. Jf burudani tosha, stess zote tupa kule.
 
Angeweka pose kama refaree afe akashughulikia saa ikishakuwa poa anawaambia waendelee ili arekodi muda umsaidie kwenye kesi, mi nadhani ingekuwa poa zaidi mkuu au we unaonaje.?

Nazani huu ushauri utamfaa sana huyu jamaa
 
Wacha ujinga wewe!!
Katengeneze saa usije ukapoteza ushahidi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom