Analysis of South Africa after election

Comred Mbwana Allyamtu

Verified Member
Jun 28, 2016
262
500
"NKHOSI SIKELEI" NA AFRIKA KUSINI BAADA YA UCHAGUZI, ANC INAJIKONGOJA, EFF IKIIMARIKA NA DA IKIZIDI KUPOROMOKA.

Na.Comred Mbwana Allyamtu
Sunday -12/5/2019.
Marangu, Kilimanjaro- Tanzania

Taifa la Afrika kusini mnamo tarehe 8/5/2019 lilitekeleza wajibu wa kikatiba kwa mujibu wa katiba ya Afrika kusini ya 1994, kwa wananchi wake wenye sifa kupiga kura katika kuchagua wawakilishi wa Mikoa (Provincial legislature) pamoja na wabunge wa bunge la taifa hilo.

Zaidi ya raia million 17.76 sawa na 65.99% walipiga kura kati ya watu milioni 27.7 walio jiandikisha kupiga kura, upigaji wa kura ulifanyika katika mikoa yote ya nchi hiyo ambayo ni jumla ya mikoa 9. Hata hivyo karibu vyama 30 vilishiriki katika uchaguzi wa mikoa na jumla ya vyama 27 vilishiriki katika uchaguzi wa wabunge wa bunge la taifa hilo.

Uchaguzi ulifanyika kwa usalama na hakuna kitendo chochote kile cha uvunjifu wa amani kilicho ripotiwa, katika mikoa yote tisa ya nchi hiyo, ni mkoa mmoja tu wa Kwazulu Natal ndio ulioripotiwa kutokea kwa kitendo cha Mtu mmoja kupiga kura zaidi ya mara moja (double voting), huku maeneo mengine ya mkoa yakifanya uchaguzi kwa usalama na amani. Kwa mujibu wa maofisa wa tume ya uchaguzi ya IEC (Independent electoral commission) walisema kwamba kuna visa 30 dhidi ya watu walio shikiliwa kwa makosa ya kupiga kura zaidi ya mara moja Katika mkoa wa Kwazulu Natal.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ( The National election and independent electoral commission Act) ibara ya 5 Kifungu cha 56-59 ina kataza mtu mmoja kupiga kura zaidi ya mara moja na kutamka kuwa kitendo hicho ni jinai, Iwapo mtu atakutwa na kosa hilo anaweza kuhukumiwa Kifungo cha miezi sita au faini ya Rand 2000. Nje na hayo bado mchakato wa uchaguzi ulifanyika kwa Utulivu na amani karibu maeneo yote ya nchi hiyo.

Waangalizi mbali mbali kutoka jumuiya tofauti tofauti walituma waangalizi wao (Electoral observers) katika uchaguzi huo huku ECOWAS ilimteua raisi wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan kuwa mwangalizi huku Umoja wa Afrika (AU) ulimteua Dr Jakaya Kikwete rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania kuwa kiongozi wa jopo la waangalizi kutoka AU (head of African Union commission to South Africa general election observation).

Mchakato wa uhesabuji kura ulifanywa kwa mfumo wa Electonics (electronic counting vote) na iliichukua siku tatu yani toka tarehe 9-11 kwa tume ya uchaguzi ya IEC kuanza kuhesabiwa kwa kura na kuanza kutoa matokeo yote ya jumla kwa mikoa yote ya nchi hiyo pamoja na yale ya bunge la taifa hilo. Jumla ya kura million 17.76 sawa na asilimia 65.99% ya kula zote zilizopigwa zilihesabiwa na kati ya kura hizo ni asilimia 1.33% ya kura ndizo zilizoharibika (spoil vote).

Katika uchaguzi huu kama nilivyotangulia kusema hapo awali vyama karibu 30 vilishiriki katika uchaguzi wa mikoa (provincial legislature) katika mikoa tisa ya taifa hilo ambayo ni mkoa wa Western Cape, Eastern Cape, Northern Cape, Northern East, Free State, Kwazulu Natal, Gauteng, Mpumalanga na mkoa wa Limpopo. Katika mikoa hii vyama hivyo vilishiriki katika kutafuta viti katika mabaraza ya kutunga sheria ya mikoa (Provincial legislature) ili ziweze kuunda serikali za mikoa.

Katika mikoa yote chama cha ANC kilifanikiwa kuongoza katika mikoa nane huku chama cha DA kikifanikiwa kulikamata mkoa mmoja la Western Cape kwa ushindi wa 55.42% huku ANC ikipata 22.41% ikifatiwa na chama cha EFF kwa kupata 3.79% katika jimbo hilo la Western Cape na kukifanya chama cha ANC kuwa chama pinzani katika mkoa huo wenye wakaazi wengi wazungu, pamoja na ushindi huo katika uchaguzi huu bado unaonesha kuporomoka kwa chama tawala cha ANC kutoka 62.35% katika uchaguzi wa mwaka 2014, mpaka 57.8% katika uchaguzi huu wa mwaka 2019 ikionesha kushuka kwa karibu asilimia 5.19%.

Kwa upande wa upinzani pia imeonyesha kushuka kwa ushawishi wa chama DA ambacho ndio chama kikuu cha upinzani (Official opposition party) nchini humo kwa miongo kadhaa sasa, uchaguzi huu unaonesha kwamba chama cha DA kimeporomoka kutoka 22.32% katika uchaguzi wa mwaka 2014 mpaka 21.0% katika uchaguzi huu ikionesha kuwepo kwa anguko la 1.32%.

Mapema jana usiku majira ya saa 6:00 jioni kwa majira ya Afrika kusini mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya IEC bwana Gren Mashinini alipokuwa akitangaza matokeo ya uchaguzi huo alisema kuwa jumla ya vyama 27 vilivyoshiriki katika uchaguzi huu ni vyama 14 pekee vilivyofanikiwa kupata wabunge katika bunge la nchi hiyo, vyama hivyo vilivyopata wabunge katika bunge la SOZA ni ANC, DA, EFF, IFP, VF PLUS, COPE, AL JAMAA, ACDP,ATM,GOOD,PAC, NFP, UDM na AIC ,huku akiendelea kwa kusema kuwa kati ya vyama hivyo ni vyama vitano ndio vilivyounda "Top 5 party" ambayo ni ANC iliyopata 57.8%, DA 21.0%, EFF 11.79%, IFP 3.3% na VF Plus kikipata 2.5%

Katika matokeo hayo ya bunge (NATIONAL ASSEMBLY SEATS) chama cha ANC kilifanikiwa kutetea nafasi yake ya kuendelea kulidhibiti bunge kwa kupata jumla ya Seats 230, na kufanikiwa kuvuka idadi ya seats zinazoitajika (majority seats needed) ambazo ni jumla ya seats 201 ili chama kiweze kuunda serikali, upande wa pili uliongozwa na chama cha DA ambacho ndio kimeshika nafasi ya pili kwa kupata Seats 84, huku EFF nayo ikifanikiwa kupata Seats 44 huku IFP chama cha Chief Buthalezi kikipata Seats 14 na chama cha VF Plus kinachoongozwa na Pieter Groenwald kikipata seats 10.

Katika matokeo haya yanaonesha kwamba chama cha ANC imepoteza viti 19 katika uchaguzi huu kutoka viti 249 ilio kuwa ikivimiliki katika uchaguzi wa 2014 mpaka viti 230 katika uchaguzi wa mwaka huu. Huku chama cha DA pia ikipoteza viti 5 kutoka viti 89 ilivyo kuwa navyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2014 mpaka viti 84 katika uchaguzi wa mwaka huu, huku EFF ikionekana kuongeza viti kutoka viti 25 katika uchaguzi wa mwaka 2014 mpaka viti 44 katika uchaguzi wa mwaka huu. Nje ya kuongeza viti katika bunge la taifa pia chama cha EFF kimeonekana kuongeza nguvu katika utawala wa majimbo (provincial legislature) kwa kufanikiwa kuongoza kambi za upinzani katika majimbo matatu ya Mpumalanga provincial legislature kwa kushika nafasi ya pili nyuma ya ANC kwa kupata 13.79%, Northwest provincial legislature kwa kupata 18.64% na mkoa wa Limpopo provincial legislature kwa kupata 14.38%, na kutangazwa na tume ya uchaguzi ya IEC kuwa ndio itakuwa chama kikuu cha upinzani katika majimbo hayo matatu ( provincial legislature official opposition party) kati ya majimbo/mikoa 9 ya nchi hiyo.

Kwa chama cha EFF katika uchaguzi huu imepata mafanikio makubwa ya karibu 90% kwa kupata jumla ya kura 1350,059 (1.35 Milioni), na karibu wabunge 44 katika bunge la taifa hilo Ikiwa ni pamoja na kuunda ngome kuu ya upinzani (official opposition party) katika karibu mikoa 3.Mafanikio haya ni makubwa ukizingatia na umri wa chama cha EFF ambacho kilianzishwa mwaka 2013, tofauti na chama cha DA ambacho kilianzishwa toka mwaka wa 1959 (kikitokana na chama tanzu cha Nationalist) lakini kikaja kubadilishwa jina ambalo inalitumia sasa la DA mwaka 2000 baada ya kuungana vyama viwili vya nationalist na chama cha Liberal. Pia utofauti wa mafanikio ya EFF ni tofauti na chama cha ANC kilicho anzishwa toka mwaka 1901.

Chama cha DA ni chama chenye base yake Katika maeneo yanayokaliwa na jamii za watu weupe hasa katika mikoa ya Western Cape, Northern Cape na mkoa wa Free State, chama hichi kimekuwa na nguvu dhidi ya ANC kutokana na sababu za kihistoria kwa kuwa chama cha DA ndio chama tanzu cha chama cha nationalist chama ambacho kilikuwa ni chama cha wazungu ambacho ndio chama kilichoendesha sera ya ubaguzi wa rangi miaka ya 1957-1994. Hivyo wao ni chama chenye pesa, na rasilimali nyingi kulinganisha na chama cha EFF cha Malema.

Mbali na DA pia chama cha ANC ndio chama tawala nchini Afrika kusini toka uchaguzi wa kwanza wa mwaka 1994, hivyo ni chama chenye pesa na miundombinu kadhaa katika nchi hiyo ukilinganisha na chama cha EFF, lakini pamoja na hayo chama cha ANC bado kimeendelea kupoteza mvuto katika uchaguzi huu, takwimu inaonesha kwamba chama cha ANC kimekuwa kikiporomoka kwa kila baada ya uchaguzi tangu uchaguzi wa kwanza wa mwaka 1994, takwimu hizo zinaonesha kuwa ANC imekuwa ikipungua kwa kasi ya 4%-5% katika kila uchaguzi mkuu unapofanyika.

Huku chama cha DA kikiporomoka kwa 2-3% (slide of 2%-3%) toka uchaguzi wa 2014 baada ya kuundwa kwa chama cha EFF. Hata hivyo chama cha EFF ndio chama pekee katika uchaguzi huu ambacho kimepata mafanikio (growing up) kwa ongezeko la 5% kutoka 6.35% katika uchaguzi wa mwaka 2014 na hatimaye kufikia 11% katika uchaguzi huu Ikiwa ni ongezeko la 5%-6%. Kutokana na takwimu hizi inakifanya chama cha EFF kuwa ndio chama pekee kilicho kuwa na kuimalika katika uchaguzi huu.

Uchaguzi huu wa Afrika kusini unafanyika kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo Kifungu cha 4, Sehemu ya 85 (Section 4 Cap 85) inaelekeza kwamba "kutakuwa na uchaguzi wa bunge na mabunge ya mikoa (provincial legislature) kila baada ya miaka 5, na kupitia uchaguzi huo rais wa jamuhuri wa Afrika kusini atachaguliwa na wabunge wa baraza la taifa (National Assembly), kutoka Bunge la Afrika Kusini, na kwamba rais atatokana na chama chenye majority vote/seats katika bunge hilo". Kwa mujibu wa katiba hiyo kiongozi wa nchi hiyo atatokana na chama kitakacho pata viti vingi zaidi bungeni(kilichopata viti zaidi ya 201).

Uchaguzi huu ni wa sita toka kumalizika kwa utawala wa kibaguzi toka mwaka 1994 na kupitishwa kwa azimio la amani na maridhiano iliyofuatiwa na mkataba wa uhuru (Freedom Charter), na Rais wa kwanza kuchaguliwa chini ya mkataba huo na katiba mpya alikuwa Nelson Mandela, katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia wa mwaka 1994, ambaye alirithiwa na Thabo Mbeki mwaka wa 1999 ambae aliyetawala mpaka mwaka 2008 alipo jiuzuru kufatia mzozo wa kisiasa ndani ya chama chake cha ANC, kisha akafuatiwa na Kgalema Motlanthe mnamo Septemba 2008 na kisha Jacob Zuma mnamo Mei 2009 mpaka mwaka jana alipojiuzuru kufatia mgogoro na chama chake na kurithiwa na Cyril Ramaphosa.

Ikumbukwe kuwa Afrika Kusini ni taifa linalotumia mfumo wa bunge (Parliamental system) katika kuundwa kwa serikali yake, Bunge la nchi hiyo (SOZA) linajumuisha jumla ya wabunge 400 wanaochaguliwa moja kwa moja na wananchi (direct vote) kwenda kuwa wawakilishi wa wananchi wa Afrika kusini.

Katika mfumo wa bunge nchini humo limegawanyika pande mbili katika kuundwa kwake, upande wa kwanza ni bunge linaundwa na Wabunge mia mbili (200) ambao huchaguliwa kutoka katika miji ya nchi hiyo na wengine 200 ambao wanachaguliwa kutoka katika mikoa (Majimbo) kati ya mikoa tisa ya nchi hiyo. Baada ya uchaguzi kumalizika na wabunge kupatikana ndipo Rais wa Afrika Kusini anachaguliwa na Bunge baada ya chama kitakacho ongoza kupata viti vingi vya wabunge vinavyohitajika kwenye Bunge ili kuunda serikali ambayo ni lazima chama hicho kifikishe viti 201 (Seats needed for a majority) ili kiteuwe rais atakae idhiniswa na bunge.

Katika Bunge la mkoa (NCOP), ambalo hutofautiana kwa ukubwa na bunge la taifa, pamoja na kupeleka wabunge Katika bunge la taifa kutoka kwenye mikoa ambayo huwa na wabunge 30 hadi 80, kutegemea na idadi ya kila mkoa katika kutoa wakilishi wa kawaida kutegemea idadi ya asilimia ya kila chama ilichopata. Wawakilishi wa kila jimbo (Mkoa) watachaguliwa na bunge husika za mikoa huku baraza kuu la Taifa ya Mikoa (NCOP - National Council Of Provincial legislature) ina wajumbe 90, kumi kutoka mikoa yote tisa ya nchi hiyo, ambao wanachaguliwa na kila bunge la mkoa.

Nje ya hayo uchaguzi huu kumekuwepo ya ongezeko la wapiga kura kwa asilimia 14% kutoka uchaguzi wa mwaka 2014. Kwamujibu wa tume ya uchaguzi ya EIC imesema kuwa wapiga kura wa mwaka huu ni milioni 27.7, huku Wapiga Kura wa ndani (Local Voters) wakiwa ni milioni 26.15 na Wapiga Kura wa nje (International Voters) wakiwa ni 171,134.

Kufatia matokeo haya kuipa ushindi chama cha ANC kwa kujizolea viti 230 na ushindi wa asilimia 57.8% (Majority seats needed) inayo kifanya kuunda serikali siku zijazo za usoni. Kikatiba na Kikanuni rais wa sasa Ramaphosa anatazamiwa kuendelea na muhura wake wa pili , hivyo anasubiri kuidhinishwa na bunge na baadae kuapisha kuwa raisi wa awamu ya tano wa taifa hilo toka lijipatie uhuru wa wengi mwaka 1994 baada ya kuangushwa kwa utawala wa kikaburu.

Cyril Ramaphosa ambae atakula kiapo cha urais mapema tu baada ya shughuri za bunge la nchi hiyo kuanza, Alizaliwa katika kitongoji cha Soweto, jijini Johannesburg katika mkoa wa Gauteng, mwaka 1952. Mwaka 1974 akiwa na umri wa miaka 22 aliwekwa kizuizini mpaka mwaka 1976 kwa makosa ya shughuli za kupambana na ubaguzi wa rangi wakati huo akiwa mwana chama wa chama cha ANC katika tawi la vijana la Youth league ANC.

Alianzisha muungano wa kitaifa wa wafanyakazi wa migodi ulio kuwa chini ya chama cha ANC mwaka 1982, na baadae kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya mapokezi ya taifa yaliyoandaa kumpokea Nelson Mandela kutoka gerezani mwaka 1990.

Baadae aliteuliwa kuwa mbunge na mwenyekiti wa mkutano wa kikatiba wa mwaka 1994, Mwaka 1997 aliamua kujihusisha kikamilifu na biashara kwa muda mwingi na kuwa moja wa matajiri wakubwa nchini Afrika kusini. Ramaphosa amewahi kuteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya Lonmin wakati wa mauaji ya wachimba mgodi wa Marikana mwaka 2012 Ramaphosa ni mtu anayependa sana michezo ya magari yaendayo kwa kasi, pia ni mtu anayependa mvinyo ulio ghali hasa katika maeneo ya starehe, lakini pia ni mvuvi na mkulima wa mashamba makubwa ya kibiashara.

Cyril Ramaphosa amewahi kuwa makamu wa raisi wa Afrika Kusini chini ya serikali ya Jacob Zuma toka mwaka 2014 mpaka mwaka 2019 alipo chukua nafasi ya urais wa taifa hilo baada ya Zuma kulazimishwa kujiuzulu urais baada ya kile kilichoitwa "mgogoro wa Zuma ndani ya chama" Ramaphosa ni mwanasiasa mwenye nguvu ndani ya Afrika kusini huku akiwa ni moja ya wanasiasa kutoka ANC wenye ukwasi mkubwa wa utajiri akiwa na utajiri wa kiasi cha dola za kimarekani 450 milioni (£340 milioni)

Katika miaka ya 1980 Ramaphosa aliwahi kuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi wa vyama vya ushirika, kipidi hicho alikuwa ni alama ya watu weusi katika kukabilina na ubepari na ubaguzi wa rangi kabla ya ANC kuchukua nchi mwaka 1994, Cyril Ramaphosa aliamua kuingia moja kwa moja kwenye siasa kwakua biashara haikuwa kipaumbele chake. Chaguo lake la kwanza lilikuwa ni siasa na alikuwa na matarajio ya kuwa makamu wa kwanza wa rais chini ya serikali ya Nelson Mandela, rais wa kwanza mweusi nchini Afrika ya kusini.

Mandela alipomkataa kuwa makamu wake alishikwa na hasira na kuamua kutohudhururia kuapishwa kwa Mandela kama rais wa kwanza wa nchi hiyo. Na pia alikataa kuchukua nafasi yoyote ya uongozi serikalini. Badala yake, Bwana Ramaphosa ambae pia ni mwanasheria akajikita kuwa mwakilishi na mwenyekiti wa mkutano wa kikatiba, akiwa na jukumu la kuandaa katiba ya Afrika kusini baada ya kupita kipindi cha miaka mingi ya ubaguzi wa rangi.

Ramaphosa aliwashangaza wananchi wengi wa Afrika Kusini ambao walimwona kama mwanasiasa wa kuaminika zaidi wa kizazi cha baada ya Mandela, alipoamua kuachana na siasa na kuwa mfanyabiashara.Wakati huo, haikuwa kawaida kwa watu weusi, kuwa katika sekta ya biashara iliyokuwa inaongozwa na watu weupe.

Ramaphosa ambae historia ya Afrika kusini inamkumbuka kwa kuitisha mgomo na maandamano makubwa ya wafanyakazi wa madini mnamo mwaka 1980 pale alipo andaa mgomo mkubwa wa madini katika historia ya Afrika Kusini. Alijiingiza kwenye biashara na wafanyabiashara wenye asili ya weupe walijaribu kumtumikia Bwana Ramaphosa ambae alipata hisa katika karibu kila sekta muhimu za uchumi nchini Afrika kusini kuanzia kwenye kampuni ya simu na vyombo vya habari, mpaka kwenye vinywaji na makampuni ya kupika chakula cha haraka (fast food) aliwekeza kwenye mahoteli ya Marekani ya McDonalds nchini Afrika kusini, yaliyo muingizia pesa nyingi kwa muda mfupi.

Pamoja na Ramaphosa kuwa bepari wa kutupa bado aliendelea kuwa mwanachama wa ANC, akiwa kiongozi mkuu wa kamati ya utendaji ya Taifa, nafasi ambayo, wakosoaji wake wanasema ilimpa habari za ndani za chama. Ramaphosa akiwa katika nafasi hiyo nyeti ndani ya chama alitumia nafasi hiyo ya utawala wake kujijenga kibiashara na kujiimalisha zaidi.

Ramaphosa akiwa ni mkurungezi wa Lonmin kampuni ya kimataifa inayomilki mgodi huo huko Marikana, alituhumiwa kwa kuwasaliti wafanyakazi ambao kwa wakati mmoja aliwatetea na kuwa upande wao, Mashtaka haya yalikuja baada ya polisi kuwaua wachimba mgodi 34 wakiwa kazini mwezi wa Agosti 2012 katika mgodi wa Marikana, huku hili likiwa ndio tukio baya kuwahi kushuhudiwa tangu kumalizike kwa utawala wa wazungu mwaka 1994. Uhusika wake ulianza kupata nguvu baada ya kuzuka kwa barua pepe zinazo muonyesha Ramaphosa kuwa ndie aliye toa amri ya kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya wachimba mgodi kwa kushiriki katika 'mgomo kali' mgomo ambao uliokumbwa na ghasia.

Japo kuwa baadae uchunguzi wa tume maalumu iliyoundwa na raisi Zuma ulimsafisha Ramaphosa dhidi ya kesi ya mauaji ya huko Marikana. Lakini Mpaka sasa kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighter (EFF) Julias Malema anasisitiza kuwa Ramaphosa alihusika na mauaji ya Marikana na kumtaja Ramaphosa kama kibaraka wa watu weupe.

Hata hivyo, Ramaphosa, ambae anatajwa na jarida la uchumi la Forbes kuwa mmoja wa wafanyabiashara wakubwa mwaka 2014 aliamua kuachana na biashara baada ya kuchaguliwa kuwa makamu wa rais wa nchi hiyo, baada ya kuteuliwa kuwa makamu wa raisi wa nchi hiyo aliamua kuachana na shughuli za kibiashara na kuingia kwenye siasa tena, gazeti la kifedha la kimataifa la Forbes, lilimnukuu akisema, "aliachana na shughuli zake za biashara ili kuepuka migogoro ya kiutawala" huyu ndie Cyril Matemela Ramaphosa, raisi wa awamu ya tano wa taifa la Afrika kusini.

Mungu ibariki Afrika kusini, Mungu ibariki Afrika......"Nkhosi Sikelei"

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copy rights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu

Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
IMG_20190513_215633_241.jpeg
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,585
2,000
Tunashukuru mkuu kwa uchambuzi wako ila naona kuna biasness chache katika bango lako kwa kujaribu kuonyesha hasa DA imeshuka sababu ya uwepo wa EFF

1. Kwanza voter turnout ya uchaguzi huu ni ndogo kuliko ya uchaguzi wa 2014 hasa maeneo ya upinzani hivyo hii nayo imeathiri kura za upinzani hasa DA.

2. Chama kilichokua zaidi sio EFF ni FF+ maana kilikuwa na kura laki 1 na sasa kina kura karibia laki 5 hivyo kimeongeza wabunge hadi kufika 10 yaani ukuaji wao ni zaidi ya 400%.

3. Moja ya lengo la chama cha DA ni kuongeza kura za watu weusi na kimefanikiwa kwani katika uchaguzi huu DA kimepata kura nyingi zaidi katika maeneo ya watu weusi kuliko uchaguzi wowote ule sasa utasemaje hakijakuwa?

4. DA kilikuwa na mgogoro huko western Cape ambalo ndio ngome yao kuu. Aliyekuwa mayor wao akajitenga na kuanzisha chama cha GOOD ambacho kimechangia kugawa kura za DA kwa % kadhaa ndio maana wameshinda hiyo province ila kwa kura pungufu.

5. Pia wapiga kura wengi wa DA hasa wazungu walipigia kura zaidi FF+ na kuitosa DA na hivyo kuchangia kupunguza kura za DA lakini hakuna connection yoyote ya kushuka kwa DA kuchangiwa na uwepo wa EFF.

Kweli EFF kimekua ila sababu kimeongeza voters base yake hasa maeneo ya ANC but isiwe chanzo cha kuweka connection kwamba kimekwapua kura za DA kama chama kikuu cha upinzani hilo halina uhalisia maana DA imeumizwa sana na vyama vidogo kma IFP,FF+ na GOOD ambapo kama wapiga kura wake wasingeenda huko kingekua na zaidi ya 22% ilizopata 2014 na sio sababu ya EFF.

Haya ni maoni yangu

Cc Malcom Lumumba
 

Comred Mbwana Allyamtu

Verified Member
Jun 28, 2016
262
500
Tunashukuru mkuu kwa uchambuzi wako ila naona kuna biasness chache katika bango lako kwa kujaribu kuonyesha hasa DA imeshuka sababu ya uwepo wa EFF

1. Kwanza voter turnout ya uchaguzi huu ni ndogo kuliko ya uchaguzi wa 2014 hasa maeneo ya upinzani hivyo hii nayo imeathiri kura za upinzani hasa DA.

2. Chama kilichokua zaidi sio EFF ni FF+ maana kilikuwa na kura laki 1 na sasa kina kura karibia laki 5 hivyo kimeongeza wabunge hadi kufika 10 yaani ukuaji wao ni zaidi ya 400%.

3. Moja ya lengo la chama cha DA ni kuongeza kura za watu weusi na kimefanikiwa kwani katika uchaguzi huu DA kimepata kura nyingi zaidi katika maeneo ya watu weusi kuliko uchaguzi wowote ule sasa utasemaje hakijakuwa?

4. DA kilikuwa na mgogoro huko western Cape ambalo ndio ngome yao kuu. Aliyekuwa mayor wao akajitenga na kuanzisha chama cha GOOD ambacho kimechangia kugawa kura za DA kwa % kadhaa ndio maana wameshinda hiyo province ila kwa kura pungufu.

5. Pia wapiga kura wengi wa DA hasa wazungu walipigia kura zaidi FF+ na kuitosa DA na hivyo kuchangia kupunguza kura za DA lakini hakuna connection yoyote ya kushuka kwa DA kuchangiwa na uwepo wa EFF.

Kweli EFF kimekua ila sababu kimeongeza voters base yake hasa maeneo ya ANC but isiwe chanzo cha kuweka connection kwamba kimekwapua kura za DA kama chama kikuu cha upinzani hilo halina uhalisia maana DA imeumizwa sana na vyama vidogo kma IFP,FF+ na GOOD ambapo kama wapiga kura wake wasingeenda huko kingekua na zaidi ya 22% ilizopata 2014 na sio sababu ya EFF.

Haya ni maoni yangu

Cc Malcom Lumumba
Maoni mazuri mkuu labda nikusahihushe kidogo...

Sio FF Plus ni VF Plus... Lakini ukuwaji wa VF ni tofauti sana na EFF....

Pia EFF umechukia ngome muhimu za DA Kama official opposition party unasemaje aijakuwa kizingiti kwa DA?
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,585
2,000
Maoni mazuri mkuu labda nikusahihushe kidogo...

Sio FF Plus ni VF Plus... Lakini ukuwaji wa VF ni tofauti sana na EFF....

Pia EFF umechukia ngome muhimu za DA Kama official opposition party unasemaje aijakuwa kizingiti kwa DA?
For clarification... FF plus ni kwa kiingereza Freedom Front Plus ila VF plus ni kwa Afrikaan ikimaanisha VryheidsFront Plus so ni tafsiri tu haina shida.

Naposema EFF haijaaffect DA siongelei kura za EFF kuizidi DA katika maeneo bali naangalia je wapigakura wa DA 2014 walimpigia nani 2019??

EFF imepata kura nyingi kutoka kwa wapiga kura wa ANC wenye hasira..... Ila DA imepoteza kura nyingi kwa vyama vidogo zaidi kama IFP huko kwazulu natal, GOOD na FF/VF Plus huko western cape,Eastern etc. Na ndio maana kura zao hazina tofauti sana na uchaguzi wa 2014.

Kwahiyo EFF imeathiri zaidi ANC kuliko DA. Hayo majimbo ambayo EFF imekuwa official opposition ni sababu ya kura za ANC kuhamia kwao na sio kuitikisa DA.

Huo ndio mtizamo wangu mkuu ila bottom line EFF na DA inatakiwa zishirikiane kama kipindi wanamtoa Zuma ili waunde coalition kubwa ya kuing'oa ANC kwenye majimbo makubwa otherwise majority ya ANC itaendelea kutawala milele.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom