Ninahitaji mtu mwenye sifa zifuatazo kwa ajili ya kusimamia shughuli za Kilimo katika Shamba binafsi Mkoani Lindi:
Awe na ufahamu na maarifa juu ya kilimo cha mazao ya biashara ya muda mfupi na ya muda mrefu kama vile Ufuta, Korosho na Alizeti
Awe na uzoefu katika kusimamia kazi za kilimo cha mazao ya biashara ya muda mfupi na ya muda mrefu kama vile Ufuta, Korosho na Alizeti
Ajue kuandaa mpango na bajeti ya kazi za shamba, kugawa kazi na kusimamia na kuhakikisha mpango kazi unatekelezwa kikamilifu na kwa wakati ndani ya bajeti iliyoidhinishwa
Awe na historia ya kusimamia kikamilifu na kwa mafanikio vijana wa shamba au watumishi wasiopungua 10 chini yake
Asiwe na historia ya wizi, udokozi au udanganyifu katika kazi na jamii anayotoka.