Kuna jamaa ana baa hapa mtaani. Kila siku anabadilisha wahudumu. Sasa hivi kaleta vitoto tupu kwenye baa yake, vinadanganya kuwa vina miaka 18 lakini ni wazi kuwa vinadanganya ili watu tusishangae, vinaweza kuwa 15 hivi. Alivichukua makwao kwa gea ya kuwa vinakuja kuuza maduka yake, kwamba anayo kadhaa hapa mjini (Dar). Sasa kamoja kwenye kukauliza uliza kanasema jamaa anakachukia kishenzi na la kufanya hakana kwa sababu nauli ya kurudi kwao Tanga hakana. Haka kadada kanasema tajiri amekachukia kwa sababu alitaka kukala tigo kakakataa. Mwenzie alikubali akijua ataliwa kawaida jamaa akamgeuzia kibao kuwa anataka tigo kwa sababu mbele mkewe anampa kila siku. Eti wahudumu wote anawala (tigo) halafu mwisho wa mwezi hawalipi wanaondoka kwenda kutafuta kazi sehemu nyingine au kurudi makwao. Anaowatoa mbali wanasotaga kishenzi, mmoja nimewahi kumpa nauli na alirudi kiijini kwao siku hiyohiyo (huwa nawasiliana naye) Kinachonishangaza ni kuwa huyu jamaa ni kiongozi kanisani ninakosali. Hii dunia imekwisha. Na ukimwona pale mbele makeke yake utasema mtu wa mungu kweli. Tatizo kwangu ni hiyo dhuluma anayowafanyia hawa wadada na hawana cha kumfanya kwa sababu jamaa is a big fish in town. Hivi hakuna watu wanaoweza kuwasaidia hawa wandugu? Tanzania kuna ajira za kutosha ila nadhani hakuna sheria nzuri za kusimamia. Hizi baa zote ni sehemu za ajira, kinachofanya ziwe nyingi sana ni kuwa wenye nazo wanawanyonya sana wahudumu. Kwa sababu huduma ya vinywaji inahitajika basi tuifanye kazi ya uhudumu iwe na maslahi. Ndio maana hawa wahudumu wanaishia kuwa malaya kwa sababu hawalipwi. Mbona nchi zilizoendelea bar maid ni mtu anayeheshimika kama wengine? Maana yangu ni kwamba tukiweza kufanya ajira zote ziheshimike, basi tatizo la ajira litapungua kwa kiasi kikubwa.