Anaandika Absalom Kibanda

Anaandika Absalom Kibanda

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,121
Reaction score
1,981
Rais Dk. John Magufuli akiwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa
NA ABSALOM KIBANDA |

NAANDIKA makala hii wakati Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, akiwa nyumbani kwao Chato ambako japo alik- wenda kwa sababu ya ma- pumziko mafupi, lakini amefikwa na msiba mzito wa kumpoteza dada yake, Monica.

Nina kila sababu ya kuungana na Wa- tanzania wenzangu, kumtumia salamu za pole Rais Magufuli kwa kumpoteza dada yake na hivyo kwa kiwango kikub- wa kusababisha alazimike kusitisha kwa muda majukumu yake mengine ambayo yumkini angeweza kuyafanya akiwa ma- pumzikoni. Msiba unaomkuta rais unali- gusa taifa.

Nilihitimisha andiko langu la wiki iliyopita linalotoka kila Jumatano katika gazeti la Mtanzania kwa kueleza namna fikra na tafakuri jadidi za mwanazuoni Issa Shivji, profesa wa Kigoda cha Mwal- imu juu ya taswira ya Chama Cha Mapin- duzi (CCM) katika mazingira na mfumo wa vyama vingi.

Hitimisho hilo, liligusia pia japo kwa muhtasari tu, ushauri adhimu wa mwa- nasiasa kijana, msomi, jasiri na mtukutu, Zitto Kabwe kwa Serikali ya JPM juu ya namna inavyoweza kuiendesha nchi kwa njia ya kumaliza vitendo vya uhasama, chuki, kuumizana na ukatili ambao kwa sehemu umehusisha vyombo vya dola, hususani Jeshi la Polisi.

Andiko langu lile ambalo kichwa chake cha habari kilikuwa ‘Kiporo cha fikra za Shivji na maarifa ya Zitto’ lilipokewa kwa namna na kwa hisia tofauti kutoka kwa wasomaji mbalimbali waliowasiliana nami.

Wako wasomaji wa makala ile wal- iokubaliana na tafakuri, wako wali- oshabikia na wako waliohoji na kutofau- tiana nami kwa maana ya kukosoa hoja mbalimbali ambazo zilibebwa na andiko lile. Bado nasubiri kusoma makala za wa- chambuzi wengine ambao waliahidi ku- jibu.

Andiko lile ukijumlisha na maoni na hoja mbalimbali zilizoibuliwa na miye mwenyewe na wasomaji wengine, ndio msingi mama wa andiko langu la leo, ni- kilielekeza kwa Rais wangu, Dk. Magufuli, ambaye bado naamini anayo hulka yake ile ile ya zama akiwa waziri, ya kufuatilia kwa kina na kwa ukaribu mkubwa maandiko ya namna hii.

Swali moja la msingi ambalo nime- kuwa nikijiuliza na limekuwa likiulizwa na watu wengine wengi, kabla na baada ya andiko langu lile ni; ‘Ni nini basi sisi kama taifa na Rais Magufuli, Mwenyekiti wa Taifa wa CCM-dola tunapaswa kufan- ya ili hatimaye tufikie ndoto za kuwa na Tanzania njema?’

Tanzania njema ninayoizungumzia ni ile ambayo kila Mtanzania atakuwa na wajibu wa kufanya kazi halali na ambayo kaulimbiu ya Rais ya “Hapa Kazi Tu’ ita- beba maana halisi ya wajibu wenye tija na faida kwa wafanyakazi, wakulima na wa- fanyabiashara.

Tutakuwa tukifanya masihara iwapo tutawaacha viongozi waendelee kuwaha- masisha Watanzania kufanya kazi katika mazingira yasiyo na tija wala faida.

Kuruhusu kuendelea kwa hali hii kunaweza kukasababisha kazi ikageuka laana na matokeo yake ule msamiati wa

‘Bongoland’ uliopata kumvuruga rais mmoja mstaafu ukarejea na kutamalaki katika maisha halisi ya leo na kesho.

Kwa sababu hiyo basi, Tanzania Njema ninayoizungumzia ni ile itakayotambua na kuheshimu utawala wa sheria na mis- ingi yote ya utawala bora kwa maana ya kutii mamlaka halali ya dola sambamba na wale walio na nafasi za uongozi kutambua kwamba wamepewa dhamana za uwak- ilishi na mamlaka ya uamuzi na utendaji ambavyo haviwapi uhalali wa kufanya lolote la kuhujumu au kuumiza wengine au kulihujumu taifa.

Katika hili, watawala na watawaliwa, wote tunao wajibu wa kutimiza wajibu wetu.

Mkwepa kodi, mfujaji wa mali ya umma na mwizi ni mhalifu kwa kiwango kilekile cha uhalifu alichonacho kiongozi muuza nchi, mbinafsi na fisadi anayetumia wadhifa kama fursa aliyonayo kujinufaisha binafsi kwa gharama za kuumiza wengine.

Tanzania Njema ya ndoto za waasisi wa taifa hili, ni ile inayoheshimu haki ya kila mmoja kuishi, kutoa maoni na mawazo yake pasipo kutishwa au kuhofia kuporwa haki za msingi kama uhuru na maisha yake.

Kwa mfano, hatuwezi tukasema tuna- lo taifa huru, la kidemokrasia na linalo- heshimu haki za binadamu wakati kukiwa na Watanzania wenzetu wa aina ya Tundu Lissu, Ben Saanane, Azori Gwanda na kabla yao, Dk. Steven Ulimboka na Daudi Mwangosi, ambao ama waliumizwa, ku- toweka na wengine kufa katika mazingira yanayoshawishi kuwapo bayana kwa jiti- hada za baadhi ya watu au makundi ya kihalifu ndani ya nchi yaliyojipa uhalali wa, kuwaziba wengine midomo kikatili na hata kuamua hatima zao.

Matukio ya namna hii si tu yanaishia katika kuchafua taswira ya kihistoria na mtaji mama wa utanzania wetu unaotumi- wa kujitangaza ndani na nje ya nchi yetu, kwamba tunaishi katika taifa linaloenzi amani, umoja na mshikamano kama tunu za kipekee, bali pia yanajenga msingi wa chuki ya kudumu, hulka za kulipa kisasi na kutoaminiana miongoni mwa Watanzania wenye nafasi mbalimbali katika jamii.

Yanapotokea matukio ya kuogofya ya aina hiyo na watu wakabaki vinywa wazi wakishangaa huku wengine wakibakia kuwa ama na majeraha ya kudumu mioy- oni au mwilini pasipo kujua kwa uhakika ni akina nani hasa wako nyuma ya ukatili wa namna hiyo, ndoto ya Tanzania njema inakuwa ni mbali sana kufikiwa.

Tutakuwa tunajidanganya wenyewe, iwapo tutaendelea kujiaminisha au kuji- danganya kwa sababu tu ya ulevi wowote wa kifikra, kwamba watu au dunia itasa- hau vitendo vya ukatili dhidi ya wanad- amu wengine kadiri muda unavyosonga mbele.

Watanzania tunapaswa kujifunza ku- tokana na siasa za ushindani na wakati mwingine za kisasi za kule Zanzibar, am- bazo kwa takribani miaka 54 sasa, watoto, wajukuu na vitukuu bado wanaendelea kubeba kumbukumbu ya mema na ma- jeraha yale yale ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na yale ya kabla ya hapo.

Kwa namna ile ile ambayo CCM in- ajivunia urithi wa kihistoria wa waasisi wake akina Julius Nyerere, TANU na ASP ya Mzee Abeid Amani Karume, ndivyo ambavyo matendo mengine mabaya ya kihistoria kama yale yanayohusishwa na kile kinachoonekana kuwa uporaji wa kura kule Zanzibar, tangu mwaka 1995, yanaendelea kubakia kuwa katika vichwa vya watu pasipo kukoma.

Kwa sababu hiyo basi, Tanzania njema ya ndoto zetu inapaswa kuanza kujengwa sasa kwa viongozi na watawaliwa kuanza kuonesha kwa vitendo kukerwa na ku- kataa hulka za ‘u-Mungu mtu’ wa mtu mmoja au kikundi cha watu fulani, au chama cha siasa, kujiona kuwa wenye dhamana isiyohojiwa au kukosolewa juu ya maisha ya Watanzania na hatima ya ke- sho na keshokutwa ya taifa letu.

Iwapo kwa sababu zozote zile tuna- pata shida kujifunza kwa makosa yetu wenyewe, basi viongozi wetu wa kisiasa, kisheria na kijamii wanapaswa kujifunza hata kwa makosa yaliyopata kufanywa na ama majirani zetu, marafiki zetu au mataifa mengine.

Afrika Kusini inaweza ikawa darasa zuri la kuponya majeraha yetu, hata kama ukubwa wa vidonda vyetu haufanani na makali na machungu waliyopitia akina Nelson Mandela, Oliver Tambo, Chris Hani, Winnie Mandela, ANC na PAC nyakati za udhalimu wa sera katili za uba- guzi wa rangi.

Shinikizo kubwa dhidi ya ukaburu lililoanzia ndani ya taifa hilo kabla ya ku- ungwa mkono na jumuiya ya kimatafa, liliwalazimisha makaburu kusalimu amri na hatimaye kumtoa kifungoni Mandela, baada ya jitihada za kumfunga jela kwa miaka 27 ili asahulike kushindwa.

Mandela alipotoka jela na baadaye akafanywa kuwa Rais wa Afrika Kusini, alibaini ukubwa wa majeraha na machun- gu waliyokuwa nayo ulikuwa hauwezi ku- malizwa na rangi na urais wake.

Mara moja aliunda Tume ya Ukweli na

Maridhiano iliyoongozwa na Askofu Des- mond Tutu, mtu aliyeonekana kukubalika zaidi na watu wa rangi na makundi tofauti.

Tume hiyo ilichimba hadi katika kiini cha machungu na majeraha ya watu mbal- imbali na ikahitimisha kazi yake kwa ku- patikana mwafaka wa kitaifa.

yaliyoibuliwa na Tume ya Askofu Tutu, yalikuwa yakitosha kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria, makumi au mamia ya raia wa nchi hiyo, ambao wakati wa utawala wa makaburu walikiuka sheria na haki mbalimbali za utu na ubinadamu.

Orodha ya watu ambao makosa dhidi ya ubinadamu waliyofanya wakati wa uta- wala wa makaburu, iliwagusa watu wengi mashuhuri waliokuwa ndani ya chama cha ANC, ambacho kilikuwa kinara wa mapambano ya kuung’oa ubaguzi wa ran- gi nchini humo, akiwamo Winnie Man- dela ambaye hadi wakati Mandela anatoka jela alionekana kuwa mwanamke aliyesta- hili kuvikwa taji la ‘Mama wa Taifa la Af- rika Kusini’. Yaliyofuata baada ya hapo ni historia.

Tukirejea hapa nyumbani, naweza ni- kasema, kwamba nilikuwa ni miongoni mwa Watanzania tuliokuwa na imani kub- wa na JPM alipoingia Ikulu ya Magogoni katika siku zake 100 za kwanza madara- kani.

Hatua mbalimbali alizochukua au ku- tangaza zilionesha bayana kwamba hatimaye taifa lilikuwa limepata Mandela wake, ali- yekuwa ‘amefungwa’ katika gereza la CCM- dola kwa miaka 20 akiwa waziri.

Wakati alipoanza kuunda serikali yake na baadaye akalihutubia Bunge, fikra zangu zilinifanya nifikie hatua ya kumwona pia akibeba zaidi taswira ya Askofu Tutu, hasa baada ya kuonesha aliingia madarakani ak- iwa amebeba mabegani mwake ajenda ya kuwa kinara wa maridhiano ya kitaifa.

Nachelea kusema moja kwa moja leo iwapo bado naendelea kumwona Mandela yule yule na pengine Askofu Tutu wa ndoto zangu ndani ya Rais JPM.

Hata hivyo, wakati nikijua kwamba, JPM amefikia nusu ya muhula wake wa urais, bado naamini anao muda wa kuchukua hatua mahususi kuweka kila kilichoharibika kabla mwisho hau- jafika.

Akiwa kiongozi ambaye kwa hulka ni mcha Mungu na mso- maji mzuri wa Biblia nina kila sababu ya kumshawishi rais wangu akatae kupoteza ‘upakwa mafuta’ kama ilivyokuwa kwa mfalme Sauli na pengine aanze kuchukua hatua za kuepuka ku- kutana na mwisho wa Mfalme Daudi.

Ninayasema hayo kwa kuwa, nimekuwa mwanahabari mwe- nye imani na pengine shabiki mkubwa wa Magufuli tangu aki- wa Naibu Waziri wa Ujenzi mwaka 1995 -2000.

Bado kumbukumbu zangu ni mbichi ninapokumbuka namna ilivyokuwa wakati Magufuli aliposhinda ubunge kule Bihara- mulo, tena akipita bila kupingwa mwaka 2000.

Wenye kumbukumbu kama zangu na hususani wanasiasa wa upinzani wa zama zile waliokuwa bungeni, kama Mabere Marando wanaweza wakawa mashahidi wazuri kwamba JPM alikuwa mmoja wa naibu mawaziri vijana maarufu zaidi wakati huo.
Tukio lake la kupita bila kupingwa kama ilivyokuwa kwa William Lukuvi, ambaye naye pia alikuwa naibu waziri, lilipokewa kwa bashasha na aliyekuwa Rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa.

CCM, nadhani kwa maelekezo ya Mwenyekiti wao, Mkapa, iliwaandalia vijana wake JPM na Lukuvi sherehe za pongezi kwa

kuiletea heshima Serikali na chama chao.
Shamrashamra hizo hatimaye zilihitimishwa na Mkapa mwe-

nyewe kuwapandisha vyeo na kuwafanya mawaziri kamili il- ipoundwa serikali mpya Novemba 2000.

Haikumpa shida Mkapa kumrejesha Magufuli katika wiz- ara ile ile ya Ujenzi na kabla ya kumtaja kuwa miongoni mwa mawaziri hodari katika serikali yake aliowapa jina maarufu zama zile ‘askari wa miavuli’.

Miaka mitano ya kazi akiwa Wizara ya Ujenzi (2000 -2005), ilikuwa ni ya kazi na mafanikio makubwa kwake mwenyewe JPM na hususani serikali nzima ya Mkapa.

Alikuwa ni Magufuli aliyeanza kwa kusimamia kikamilifu na kwa mafanikio makubwa kazi ya kutandaza barabara za lami katika maeneo mbalimbali ya nchi wakati wa Mkapa.

Ni kipindi hicho akiwa waziri zama za Mkapa ndiye hasa aliyekuja na wazo ambalo lilipata upinzani mkubwa la kutumia fedha za ndani kujenga baadhi ya barabara za lami.

Uhodari wake kazini na uwezo wake wa kujibu maswali bun- geni kwa takwimu, ulimfanya awe miongoni mwa wanasiasa wenye ushawishi na umaarufu mkubwa.

Itoshe kwa leo kusema, umaarufu huo uligeuka mwiba kwa baadhi ya mawaziri wenzake na harufu yake ikagusa hata hisia za urais kwa mara ya kwanza mwaka 2005.

Ni wazi kwamba mbegu ya uongozi ndani ya JPM ilipandwa na Mkapa kwa muda wa miaka 10 kati ya 1995-2005.

Bado naamini kwamba ili JPM aweze kuifinyanga vyema visheni ya urais wake na hatimaye kufikia kile alichopata kukisema kuwa ni matamanio ya kuja kuwaongoza malaika siku Mungu wake atakapomwita, basi atalazimika kuanza pale alipofundwa na ‘mentor’ wake Benjamin Mkapa.

Itaendelea Jumatano ijayo…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania tuliwekeza imani yetu kwa mtu badala ya kuwekeza kwenye MIFUMO, kama anaipenda Tanzania huyu bwana atusaidie kuweka mifumo akianza na katiba mpya.Uongozi nafikiri huleta ulevi, JPM yule waziri amebadilika sio huyu Rais, kumbuka alikuwa shabiki wa katiba ya Warioba kaingia akasema si kipaumbele

Magufuli hawezi kubadilika, MAGUFULI Ni prentenda Ni mtu mwenye kupenda kulipa visasi. Ni mtu asiesamehe, Magufuli hawezi kubadilika mpaka siku atakapowekwa ndani au kuzungukwa na watanzania kwa mabaya aliyoyafanya. Magufuli ataaribu yote mazuri aliyoyafanya. Sifa, Kiburi Kiburi kujiona kuwa yeye Ni mkubwa kuliko MUNGU. Magufuli anajiona hawezi kufa, anajiona ataishi milele na kuongoza milele. Magufuli Hana akili ya kujua dunia inaenda wapi na tuko wapi, Magufuli anaangalia ya sasa. Hana upeo wa kusoma nyakati kujua dunia inaenda wapi. Magufuli atakuja kupata tabu na mtayasahau yote aliyoyafanya na hawa wanaomwabudu na kumtumikia kwa kuua watu watamkana. Muda unakuja na Wala siyo mbali
 
Hiki Cheo kimemzidi uwezo ndo maana amebadirika kiasi cha kila mtu mwenye akili kumshangaa
 
Magufuli hawezi kubadilika, MAGUFULI Ni prentenda Ni mtu mwenye kupenda kulipa visasi. Ni mtu asiesamehe, Magufuli hawezi kubadilika mpaka siku atakapowekwa ndani au kuzungukwa na watanzania kwa mabaya aliyoyafanya. Magufuli ataaribu yote mazuri aliyoyafanya. Sifa, Kiburi Kiburi kujiona kuwa yeye Ni mkubwa kuliko MUNGU. Magufuli anajiona hawezi kufa, anajiona ataishi milele na kuongoza milele. Magufuli Hana akili ya kujua dunia inaenda wapi na tuko wapi, Magufuli anaangalia ya sasa. Hana upeo wa kusoma nyakati kujua dunia inaenda wapi. Magufuli atakuja kupata tabu na mtayasahau yote aliyoyafanya na hawa wanaomwabudu na kumtumikia kwa kuua watu watamkana. Muda unakuja na Wala siyo mbali
i second this comment, ndo maana 95% tunafikiria madaraka yetu kupitia ccm na uchaguzi and 5% nchi
 
Watanzania tuliwekeza imani yetu kwa mtu badala ya kuwekeza kwenye MIFUMO, kama anaipenda Tanzania huyu bwana atusaidie kuweka mifumo akianza na katiba mpya.Uongozi nafikiri huleta ulevi, JPM yule waziri amebadilika sio huyu Rais, kumbuka alikuwa shabiki wa katiba ya Warioba kaingia akasema si kipaumbele

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo la Tanzania ni ccm,2010 ccm walituambia tuchague chama baada ya wao kuona Slaa wa upinzani alikuwa bora kuriko JK,CCM hiyo hiyo 2015 wakaja na chagua mtu sio chama? na kwa kuwa % kubwa ya watanzania akiwemo Magufuli wameshasahau kuwa chama ni kikundi cha watu kadhaa tu,basi wao wanaamini bila ccm hakuna Tanzania. Am so sorry for my country-Magufuri anapenda ccm si Tanzania na ni ngumu sana kutumikia ccm na Tanzania maana interest zao ni tofauti
 
Magufuli hawezi kubadilika, MAGUFULI Ni prentenda Ni mtu mwenye kupenda kulipa visasi. Ni mtu asiesamehe, Magufuli hawezi kubadilika mpaka siku atakapowekwa ndani au kuzungukwa na watanzania kwa mabaya aliyoyafanya. Magufuli ataaribu yote mazuri aliyoyafanya. Sifa, Kiburi Kiburi kujiona kuwa yeye Ni mkubwa kuliko MUNGU. Magufuli anajiona hawezi kufa, anajiona ataishi milele na kuongoza milele. Magufuli Hana akili ya kujua dunia inaenda wapi na tuko wapi, Magufuli anaangalia ya sasa. Hana upeo wa kusoma nyakati kujua dunia inaenda wapi. Magufuli atakuja kupata tabu na mtayasahau yote aliyoyafanya na hawa wanaomwabudu na kumtumikia kwa kuua watu watamkana. Muda unakuja na Wala siyo mbali
Maneno ya ukweli sana haya japo umejaribu bila mafakio kuificha hasira yako juu ya magu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magu anaitumikia ccm na anaamini ili uwe mtanzania ni lazima uwe ccm. Huwa namshangaa akisema hiyo miradi watatumia watanzania wote. Je kuna mradi gani ukikamalika watanzania hupata huduma hiyo bure? Hizo ndege ni nani anapanda bure? Kuna tofauti gani na ndege za mashirika binafsi? Kwani hizo za watu binafsi hawapandi wenye vyama na wasio na vyama?
 
Magufuli hawezi kubadilika, MAGUFULI Ni prentenda Ni mtu mwenye kupenda kulipa visasi. Ni mtu asiesamehe, Magufuli hawezi kubadilika mpaka siku atakapowekwa ndani au kuzungukwa na watanzania kwa mabaya aliyoyafanya. Magufuli ataaribu yote mazuri aliyoyafanya. Sifa, Kiburi Kiburi kujiona kuwa yeye Ni mkubwa kuliko MUNGU. Magufuli anajiona hawezi kufa, anajiona ataishi milele na kuongoza milele. Magufuli Hana akili ya kujua dunia inaenda wapi na tuko wapi, Magufuli anaangalia ya sasa. Hana upeo wa kusoma nyakati kujua dunia inaenda wapi. Magufuli atakuja kupata tabu na mtayasahau yote aliyoyafanya na hawa wanaomwabudu na kumtumikia kwa kuua watu watamkana. Muda unakuja na Wala siyo mbali
Sidhani kama watakuelewa....madaraka yanalevya sana.
 
Back
Top Bottom