Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
ANA MAZONGE MFALME.
Mfalme ana tenge, leo nawapa hadhari,
Ndimi zenu muzichunge, hizi zama za hatari,
Lakini musimvunge, kwa kupamba taksiri.
Mfalme ni mazonge, chukuweni tahadhari,
Mamboye musiyapinge, ila sifiche dosari,
Mulimzoea kenge, huyu nyoka wa hatari.
Mfalme ana singe, naomba mujihadhari,
Kwa panga siwacharange, thama kutibu nasuri,
Rasini analo nunge, mpungufu wa nadhari.
Mfalme ana chonge, vidolevye kama suri,
Akiyamega matonge, nguruwe na kachumbari,
Simtolee manenge, na kusambaza habari.
Kiza ndani ya msonge, na chawaka kibatari,
Una ndwele wenu mwenge, yataka mutafakari,
Aula mambo mupange, mpate nuru kwa nari.
1 February 2017 Jumatano
Mashairi yangu mengine hapa Jf.
Mfalme wetu ropokizi
MUNGU, KIZA NA ULIMWENGU.(100)
Leo nawatukana!
Hii chini page yangu fb.
Mashairi Ya Rangimoto | Facebook
Dotto Rangimoto Chamchua.(Njano5)
Call/whats app 0622845394 Morogoro.