Amuua mwanafunzi mwenzake kwa kumkata na wembe

Amuua mwanafunzi mwenzake kwa kumkata na wembe

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,486
RPC%20Mtwara.jpg

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Henry Mwaibambe


Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Mtwara Ufundi mkoani Mtwara, Tawfiq Hamisi (17), amefariki dunia baada ya kukatwa na kiwembe katika mkono wake wa kulia na mwanafunzi mwenzake Issac Yohana (16).

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe, amesema kabla ya kifo hicho kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mtuhumiwa ambaye ni Isaac anayedaiwa kuficha kiatu cha mwenzie ambapo baada ya mzozano akaamua kumkata na kiwembe mwenzie chini ya bega lake la kulia.

Ameongeza kuwa marehemu ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga huku mtuhumiwa ni mwenyeji wa wiayani Newala mkoani Mtwara, na kwamba taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka kwao zinafanywa na uongozi wa shule, huku mtuhumiwa akishikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Ligula, Dkt. Mdoe Mhuza, amethibitisha kupokelewa kwa mwili wa marehemu majira ya saa 11 alfajiri na kudai kuwa bado uchunguzi zaidi unaendelea kwa ajili ya kuweza kubaini chanzo cha kifo chake.


Chanzo:
IPP Media
 
16 years maskeen alafu anaenda kuzeekea jela.. Jamani vijana tuweni makini. Mungu atunusuru
 
duh inasikitishasana,
pole kwa familia za hao vijana.
 
Dah sasa wanasema yupo chini ya ulinzi kwa ajili uchunguzi! upi sasa,,?
 
Kiwembe cha aina gani hicho. Uchunguzi wa kina ufanyike. Mtu anapigwa risasi tumboni au kukatwa na panga kichwani anapona; huyo wembe tu!!!!!! Allah ailaze roho yake mahali pema peponi. Inallilah wa ina ilayh rajiuun
 
Jamani wembe umesababishaje kifo? Naomba wataalamu mtujuvye. Kavuja damu sana ukizingatia na hospitali za mashenzini hazina huduma? Kapata infection kidonda kikawa septic na hatimaye kushindikana? Kafa kwa maumivu makali au nini? Wembe umebakia mwilini na kufanya sumu? Wembe ulikuwa na sumu? Au ni nini? Hii habari inahitaji ufafanuzi ili tuongeze maarifa.
 
duuh nikisikia hivi nakumbuka siku nilipokua namsaidia mdogo wangu asipigwe jamaa katoa kisu kanichana kwenye mkono wa kulia mpaka leo kovu ninalo daah aisee hasira mbaya hasira hasara
 
Inna Lillah Wainna Ilayhi Raajiuun.

Inasikitisha kwa kweli
 
Jamani wembe umesababishaje kifo? Naomba wataalamu mtujuvye. Kavuja damu sana ukizingatia na hospitali za mashenzini hazina huduma? Kapata infection kidonda kikawa septic na hatimaye kushindikana? Kafa kwa maumivu makali au nini? Wembe umebakia mwilini na kufanya sumu? Wembe ulikuwa na sumu? Au ni nini? Hii habari inahitaji ufafanuzi ili tuongeze maarifa.
Mi mwenyewe najiuliza angekuwa mtoto mchanga sawa mtu mzima ishhhh!Its so weird.
 
Back
Top Bottom