Amuua mumewe kisa amewahi kuingia bafuni

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Mgini Aron (37), mkazi wa Magunga Wilaya ya Butiama Mkoani Mara, amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mkewe Jeni Mwenda (25) kwa sababu ya wivu wa mapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Jumatatu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafari Mohamed alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 30 majira ya saa 11:15 jioni katika kitongoji cha Kitaramanka, Kata ya Mirwa.

Alisema baada ya marehemu kutoka matembezini alifika nyumbani moja kwa moja na kuingia bafuni kitendo kilichomkasirisha mkewe akidai kwanini amerudi na kuingia bafuni moja kwa moja.

Kamanda Mohamed alisema kuwa baada ya marehemu kuambiwa hivyo walianza ugomvi na mpenzi wake huyo, katika purukushani za hapa na pale ndipo Jeni alipomchoma na kitu chenye ncha kali upande wa titi la kushoto na kusababisha kifo chake.

Kamanda alisema mtuhumiwa ameshakamatwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa uchunguzi zaidi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kama ni Mkurya Haishangazi.
 
Khaaaa jela hiyo...
Ugali wa uraiani ulivyo mtamu...Asante Mungu kwa kunipa hofu ya kupigana
 
Mi nilijua mumewe kawahi kufika kileleni, kumbe bafuni - ujinga mtupu.
 
Mwanamke ni haki aulize kwa nini mmewe afike usiku apitilize bafuni kuoga, halafu anajibiwa shombo. Halafu inaonekana kulikuwa na ugomvi wa mda marefu kuhusu kuchepuka kwa mwanaume, siku iyo uvumilivu ulimshinda. R. I. P
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…