ALWATAN KIZIGO
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 539
- 642
SIKU chache baada Waziri wa nchi anayeshughulikia maafa Jenista Mhagama kujionea adha ya wananchi wa Kitongoji cha Kibundugulu kijiji cha Mbaka ya kuvuka mto kwa kutumia kamba kama alivyoombwa na Mbunge wa Rungwe Sauli Amon, Serikali imeanza kuwajengea daraja kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi.
Wananchi wa kitongoji cha Kibundugulu wamekuwa wakipata adha hii kwa muda mrefu ya kuvuka kamba ama wengine kulazimika kupiga mbizi ili kwenda kupata huduma muhimu za kijamii ikiwemo matibabu na elimu, ambapo hivi karibuni Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu anayesughulikia maafa Jenista Muhagama, alitembelea eneo hili na kujionea hali ilivyo, akiahidi serikali kulitafutia ufumbuzi wa haraka.
Amos Makalla ndiye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, ametembelea daraja hili na kudai kuwa serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya gharama za ujenzi, lakini pia akapiga marufuku tabia ya wananchi ya kuvuka mto huu kwa kamba na kwamba wanahatarisha usalama wa maisha yao.