Amnesty International: Kenya, Tanzania Miongoni Mwa Wakandamizaji Wapinzani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,886
Amnesty International: Kenya, Tanzania Miongoni Mwa Wakandamizaji Wapinzani
Februari 23, 2017
E0EC401A-F816-4CEE-A4B4-8C9BA61F06C0_w640_h360_s.jpg

Ripoti ya Amnesty International

Kenya na Tanzania zimetajwa katika jumla ya nchi za kiafrika ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuwakandamiza wapinzani na kunyongesha uhuru wa kujielezea.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, limesema mwaka 2016/17 uligubikwa na wimbi la uvunjifu wa haki za binadamu.

Pia limeeleza kuwa watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari, kwa mfululizo, wameendelea kukabiliwa na vitendo vya uvunjifu wa amani.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa haki ya uhuru wa kujielezea ilikabiliwa na mmomonyoko mkubwa pamoja na wimbi jipya la vitisho kutoka katika vyombo vya dola.

Kumekuwa na jaribio la kukandamiza wapinzani na kunyongesha uhuru wa kujielezea vilivyo jitokeza katika bara zima la Afrika, imesema ripoti hiyo.

Nchi nyingine zilizoorodheshwa katika ripoti hiyo na kuhusishwa na uvunjifu huo wa haki za binadamu ni pamoja na Botswana, Burundi, Cameroon, Chad, Côte d’Ivoire, Gambia,Mauritania, Nigeria, Somalia, South Sudan, Sudan, Togo and Zambia.

Ripoti imesema hayo ni kati ya zaidi ya matukio 177 ya watu binafsi waliouwawa kinyume cha sheria, wakati wakiwa mikononi mwa vyombo vya usalama kwa mwaka mzima (2016/17).

Nchi nyingine hizo 14 ziliorodheshwa ni kati ya zile zinazoongoza katika kukandamiza uhuru wa kujielezea na pia ukamataji wa kiholela na kuwaweka kizuizini wanachama wa vyama vya upinzani na makundi mengine.

Katika ripoti hiyo ya Amnesty International matukio mengi yameshuhudiwa katika maeneo ya pwani, na vitendo hivyo vya uvunjaji wa haki za binadamu vimekuwa vikitekelezwa kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na mashambulizi ya kundi la kigaidi la al-Shabaab.

“Kwa mujibu wa Haki Afrika, kikundi cha haki za binadamu, kulikuwa na mauaji 78 kinyume cha sheria na kutoweka kwa watu bila ya taarifa yoyote katika kaunti ya Mombasa katika miezi 8 ya kwanza ya 2016.
 
Bora wengine wamesema haya njooni mkanushe mlifikiri yanayofanyika ulimwengu hauoni?!
 
Hii ndio Africa!
Tutatofautishwa vipi na Mabara Mengine Duniani.?

Na Niukweli uliowazi kabisa Nchi hizi zimetubana Uhuru wa Kujieleza,hao hao viongozi Ndio tunawategemea watengeneze katiba Mpya na kupokezana Madaraka na Upinzani.

Siasa sio Uadui,lakini naona kwa Afrika yetu hii Siasa ni Adui wa paka na panya japo hawauweki wazi uadui huo.
 
Baada ya kufanya tafiti na kutoa matokeo, je wanatushauri nini au wanachukua hatua gani?
 
Kwahio wakisema Amnesty International tunaamini...yani tunasubiri mzungu atoke ulaya aje kufikiri kwa niaba yetu?

Hayo mashirika hayana internal democracy yatawezaje kutonyooshea kidole?
 
Bora na wenyewe wamwite dikteta ingawa ni indirectly lakini inasaidia.

Yeye aendelee kupotoshwa mwisho wa siku anakosa pa kujishika, si ndani wala nje.

Inaonekana ni mzito wa kuelewa na kubadilika kulingana na wakati ndio maana hawezi kujifunza kwa JK.
 
Kwahio wakisema Amnesty International tunaamini...yani tunasubiri mzungu atoke ulaya aje kufikiri kwa niaba yetu?

Hayo mashirika hayana internal democracy yatawezaje kutonyooshea kidole?
Mbona ni wazungu hao hao waliotoka ulaya wakawaletea dini, demokrasia, silaha, elimu n.k na mkawaamini?

Kwanini msiwaamini sasa hivi wanavyowaletea taarifa ya kuwepo udikteta nchini?
 
Mbona ni wazungu hao hao waliotoka ulaya wakawaletea dini, demokrasia, silaha, elimu n.k na mkawaamini?

Kwanini msiwaamini sasa hivi wanavyowaletea taarifa ya kuwepo udikteta nchini?
Hao wakina nani unaowazunhumza?

Mimi ndo nmetoa hoja angu...unajua nina dini au hapana?. Usiongee kiujumla jumla...
 
Kwahio wakisema Amnesty International tunaamini...yani tunasubiri mzungu atoke ulaya aje kufikiri kwa niaba yetu?

Hayo mashirika hayana internal democracy yatawezaje kutonyooshea kidole?
... Yaani kwa akili yako uzuie bunge live, uzuie mikutano ya kisiasa etc halafu wewe tena ndiyo useme nchi yako ina utawala bora na wa kidemokrasia!!!
 
Back
Top Bottom