Amini Usiamini....

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
Mwanaume mmoja wa nchini Italia ambaye alipigwa risasi ya kichwa mtaani amewashangaza madaktari dakika chache kabla ya kufanyiwa upasuaji baada ya kupiga chafya na risasi kutoka kupitia puani.
Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Cardo Sangermano mkazi wa mji wa Napoli, aliwahishwa hospitali baada ya kupigwa risasi ya kichwa na mtu asiyejulikana usiku wa mkesha wa mwaka mpya.

Wakati akiwa mtaani pamoja na mpenzi wake wakiungana na mamia ya watu kusherehekea kuingia kwa mwaka 2011, Cardo alipigwa risasi na mtu asiyejulikana.

Cardo aliwahishwa hospitali na mpenzi wake akiwa amepoteza damu nyingi. Wakati madaktari wakijiandaa kumfanyia upasuaji kuiondoa risasi kichwani mwake, Cardo alipiga chafya na kimaajabu risasi kwa kupitia kwenye pua yake ilitoka na kudondoka chini kwenye sakafu.

Madaktari walisema kuwa Cardo ana bahati sana kwani risasi iliingia kwa kupitia nyuma ya kichwa chake na huenda ilinasa kwenye mfupa wa tundu la pua yake.

Cardo hakuhitaji tena upasuaji wa kuiondoa risasi hiyo badala yake alipewa matibabu kutokana na madhara ya risasi hiyo kwenye jicho lake la kulia.
 

Hii Thready ungeipeleka sehemu yake kwenye JOKES! Lakini kama ni kweli basi Mungu ni mnene!
 
Kha hii imekaa kama habari nyepesi nyepesi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…