Mapengo 17
R I P
- Mar 28, 2014
- 1,228
- 618
Mimi ni kijana (28) sijaoa ninajishughulisha na kazi za kawaida zinazoniingizia kipato. Awali nilikuwa naishi Arusha,nilikuwa na binti tuliyeanzisha naye mahusiano kwa zaidi ya miaka minne na mahusiano yetu yalianza wakati nikiwa chuoni mwaka wa tatu ambapo pia nilikuwa nafanyakazi sehemu.
Binti anatokea Kanda ya Ziwa, pia niko Imani moja na yeye (Mkristo) ni mcha Mungu kama mimi. Wakati nakutana na yeye alikuwa na mahusiano na kijana mmoja ambaye alikuwa Kigoma (alikuwa mwalimu) kutokana na umbali waliachana na huyo jamaa kwa madai kuwa jamaa umri umeenda sana.
Tulipoendelea watu walokuwa wanamfuatilia aliwatolea nje kwasababu yangu (binti anaourefu wa wastani na amejaliwa umbo hususani mguu), nilikuwa na access ya kujua anachokifanya bila yeye kujua, baada ya muda nikagundua wakati wa likizo binti anataka kwenda likizo kwa shemeji yake aliyemuoa Dada yake mtoto wa Mama mkubwa.
Aliyekuwa anaishi huko Ngaramtoni Arusha, nilimuambia poa, kumbe huko alikokuwa anataka kwenda alikuwa anaajenda ya siri (walikuwa wapenzi kwa muda mrefu sana) walikuwa wanaongea kinyumbani hata sms za kawaida (nilikuwa naelewa baadhi ya maneno) na alikuwa anatumiwa hela kadha wa kadha sikuweza kumuuliza kwamba ni kwanini anatumiwa hela na huyo mtu kwasababu nilijua ni shemeji yake.
Kabla sijamuuliza kuhusu hilo, shemeji yake akanipigie simu nikiwa kazini na kunieleza kuwa ameunganisha namba ya binti kwa kuwa ni mchumba wake (shemeji yake anawatoto wawili wakubwa walioko Kahama Shinyanga) nikamuomba radhi nikaachana na bwana shemeji nikaamua kumuita binti nilivyorudi kazini, nilivyomuuliza akakataa akasema shemeji yake anamtaka tu, nikamwambia poa.
Nilikuwa na rafiki yangu anafanya kazi kwenye makampuni ya simu nilivyomuelezea akaniambia atanifanyia printing out (alinielekeza namna ya kuipata kwasababu inatolewa kwa kibali maalum na nilivyofanya hivyo nikaipata) nikaelewa yote, nilishindwa kuelewa kuwa huko nyuma aliwahi kukutana naye kimwili au la! Kwasababu bado alikuwa hajaenda likizo japokuwa inaonyesha kulikuwa kuna mchezo mchafu wakati binti anaishi kwake kipindi cha miaka iliyopita.
Nikaachana na binti,wakati huo tuna miezi 6 kwenye mahusiano, baadae tulisuluhisha mambo yakaisha, siku zikaenda na nilikuwa naishi kwenye chumba kimoja hadi nikaamua kuchukua vyumba viwili kwasababu ya kipato kuongezeka na yeye akawa sehemu ya familia kwamaana ndugu wa pande zote wakajua kuwa tuko wote.
Kila baada ya wiki moja au mbili lazima Mama yake aongee na me, lakini binti alikuwa amewazoea wazazi wangu sana na wao walikuwa wanampenda. Nilipata kazi yenye maslahi na ninayoipenda nikahamishiwa mkoa mwingine na kampuni tofauti na ile niliyokuwa ninaifanyia awali.
Binti nilimpangia chumba wakati anaingia mwaka wa pili chuoni yeye akawa anatoa nusu ya hela na me nikaamua kumuongezea (haikuwa hivyo nililipa yote tangu mwaka 2012 hadi mwaka jana Disemba, 2014) kama mnavyojua ukimthamini mtu unayetegemea kuja kuishi naye pia gharama ndogo ndogo za field, mara nguo mara nimekwama nataka kuchukua kitu flani kwasababu familia yake ina uchumi wa kati, nilimpa alipohitaji kadri nilivyobarikiwa.
Mungu alivyonisaidia nilipopata hiyo kazi ili nihame kule Arusha, binti nilimwachia kila kitu nilipokuwa nimehamia (kutoka chumba kimoja hadi viwili), nikaanza maisha upya kwenye kituo changu kipya cha kazi. Sikuweza kuyapa nafasi mambo niliyokuwa naambiwa na marafiki zake kwasababu niliamini yeye ni mtu maalumu kwangu na anajua udhaifu wangu na me najua wake (Ili kuepusha ugomvi).
Udhaifu wa binti
Akifanya jambo na nikimuuloiza alianza kuacha kuniweka wazi, nikamuacha tu nikawa nafanya safari za kushtukiza kumfuata nikaingia mashaka ila kilichotokea ni kwamba mwaka jana mwezi wa 3 hadi 11 akinikosea kitu nikawa namchukia sana kwasababu ya uchungu niliokuwa nao na upendo wangu kwake, (yalitokea baadhi ya mambo nikaamua kuachana naye) hadi sasa sijaamua kuwa na mpenzi mwingine kwasababu maalum.
Baada ya ugomvi, tarehe 17, Mei, 2015 nilipata taarifa kwamba anataka kuuza vitu nilivyomuachia kutoka kwa marafiki zake, nikajiandaa kisaikolojia ili nimuulize, nilipomuuliza alikiri kuwa anataka kuviuza na ataniambia ni kitu gani nitachukua (kumbuka nilikuwa naishi kwenye vyumba viwili na palikuwa pamejaa kila kitu) nikamuuliza kwanini anataka kufanya hivyo akasema anataka arudi kwao.
Katika uchunguzi wangu nilibaini kuna kijana wa Mwanza aliyempata na kuingia naye katika mahusiano kati ya mwezi 3-4 mwaka huu (Aliuza vitu ili aende kwake kwanza) ambaye ni ndugu yake na yule kijana aliyekuwa mwalimu huko Kigoma, nikamuambia binti kwasababu tumeachana nitajua ninampa nini na sio yeye anipangie kuwa atanipa nini…Tarehe 21, Mei, 2015 nikapata taarifa kuwa ameviuza nikamuagizia ndugu yangu kwake alipofika alikuata kitanda na godoro tu na kimeza nilichokuwa nawekea ndoo za maji.
Nilimuuliza kwanini alifanya vile hakunipa jibu linaloeleweka nikamuambia rafiki yake kuwa atafute ukweli wa hilo jambo aliambiwa ni kweli vitu vimeuzwa labda nitoe hela ya kuvikomboa (thamani ya vitu kwaharaka haraka ni vya milioni 7 kasoro (ameuza milioni 2 kwa maelezo yake).
Hadi sasa inaniuma sana kwa kitendo cha binti kuuza vitu bila kunisikiliza kuwa tugawane vitu kwasababu nilivipata nikiwa na yeye ingawa yeye hakuchangia hata silingi kumi.
Nimfanyeje huyu binti?nimfuate ili nimshawishi/nimforce avirudishe ili nivichukue nijue navipeleka wapi au nimuache tu?niwaambie ndugu zangu kuwa ameuza vitu vyangu au ninyamaze tu? (hadi sasa binti hajaondoka yuko Arusha).