Ameokoa Injini ya gari yangu

Jina hukuchukua, namba ya sim hukuchukua, hata namba ya gari lake hukukariri?
Kwa moment niliyokuwa nayo sikufanya hivyo mkuu, ila naamini kuna siku atapita katika uzi huu na kuni PM
 
Question:

Gari yako in Oil Pressure gauge?
tufanye inayo hiyo gauge inaathiri ama kubadilisha vipi dhamira ya uzi huu kuwa ni wa shukurani? Hata kama wewe ni fundi gereji, si lazima uonyeshe ujuaji pasipo na haja ya kufanya hivyo.
 
Watanzania wakarimu sana nchi za watu hata wakuone unaenda kufa wanakukaushia tu

Watanzania wa Karimu, kuna uzi nimesoma jamaa anasema watanzania wanapendana baada ya kusaidiwa Samna ya kwenda kugegeda mchina
 
tufanye inayo hiyo gauge inaathiri ama kubadilisha vipi dhamira ya uzi huu kuwa ni wa shukurani? Hata kama wewe ni fundi gereji, si lazima uonyeshe ujuaji pasipo na haja ya kufanya hivyo.

Jamaa ashafika siku nyingi kweli, sasa sijui anauliza ili iweje
 
Pole na hongera mkuu safarini lolote linaweza kutokea.Madereva ni vizuri kusaidiana barabarani.
 
Nimejifunza jambo hapa. Pamoja na kumshukuru huyo ndugu aliyemsaidia mleta mada, ni vema wenye vyombo vya moto msifanye service na kuanza safari ndefu immediately after. Ni vema uwe na muda wa kutosha kama siku mbili ama tatu baada ya service, kisha uanze safari yako. Hii itakusaidia kuyabaini makosa kama hayo. Pia endapo magurudumu yako yamefunguliwa kwa kubadilisha ama kuziba pancha, jitahidi wewe mwenyewe kuhakiki kama yamekazwa sawasawa, vinginevyo utashangaa tairi lako limetangulia mbele nawe ukabaki nyuma.
 
Nilijua utakuwa kama wale wasio na shukrani,ni Mimi Hugo ndugu ,kwakuwa nimepata no yako humu tutawasiliana
 
Shukrani zako nimezipata na mimi nashukuru kwa kunishukuru.
 
Umefanya jambo jema sana kushukuru pengine jambo la kujifunza ni kwamba next time ukiwa barabarani jitahidi kusikiliza pia honi za wengine zinaashiria nini, hongera sana kwa kuokoa gari
 
Ni kwasababu haikufikia level ya kuwasha taa, kifupi hata wasingekusimamisha taa ya oil ingewaka.
Mkuu heshima kwako.
Kweli taa ingewaka, lakini kutokana na sababu mbalimbali (ikiwemo stori ndani ya gari) huenda ningeiona baada ya dakika moja au mbili na wakati huo hali ingekuwa mbaya.

Hata hivyo niliaacha kukanyaga 'accelerator pedal' na kuangalia sehemu ya kuegesha, ila Jamaa alinisimamisha kwa bidii sana, nikasimama.
 

Abarikiwe sana msamaria mwema huyo team Opa mwenzangu!
 
Mkuu kumbe tupo wote hapa jukwaani! ! ! usijali nilikusaidia kwa moyo mmoja kwa kuamini kuwa tunainuka kwa kusaidia wengine, na pia bila kusaidia wengine huwezi kuthibitisha kama umekua. sikujua kama ulilala pale, ningekusaidia kutengeneza jioni ileile. na wale abiria nilijua ndugu zako. vinginevyo ningewasogeza.
 

Hee, Mkuu, ila na wewe una moyo mgumu sana. Mtu amesimama, akakuambia tatizo, mkajadiliana, aka-ofa kukuvuta, akakuvuta, akakuaga, hata jina hukukumbuka kumuuliza na mlikuwa naye muda wote huo? Naanza kuhisi una kau-bosi bosi fulani ambako kanakufanya usiwe na silka ya kuwa mwepesi wa kushukuru. Ni kama vile umezoea kufanyiwa vitu na watu unaowalipa ambao unaona huna haja ya kuwashukuru na ukajikuta na kwa huyu bwana umejisahau.
 

Nasikia ka-harufu ka utapeli hapa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…