Amenichumbia lakini hataki Ndoa

Mekuelewa
 
Kwani akikuoa nini kinaongezeka?
Kashalipa mahari, na wewe tayari unatumikia majukumu ya ndoa, shughuli imeisha hapo.
Subiri siku ya siku usikie kaoa mwanamke mwingine, utupiwe virago.
Sasa huoni sio kitu kizuri mkuu
 
Kama mnaishi wote haraka ya nini?
Kasema ajipange..kama kwenu Wana haraka wawe tayari kugharamia harusi
Sli la nyumbani naloulizwa ni kama jamaa amekua teyari mpk kulipa mahari kwanini amekua mzito kwenye kumalizia ndoa hata kama kwa sherehe ndogo tu ya watu wa karibu ameamua kukaa kimya
 
Sio lazima harusi wanaweza funga ndoa bila sherehe. Muhimu kile cheti kuna leo na kesho. Mara aje kusikia huyo kaka ameoa atapeleka ushahidi gani kua yeye ni mke halali?
Unanielewa kweli shoga yangu na me hofu yangu ipo hapa amepewa mpk option ya kufanya sherehe moja nikimaanisha me nisifanye sendoff wala kitchen party lakini still amekua mgumu
 
Maji yameshamwagika mkuu nini unanishauri
 
Sasa huoni sio kitu kizuri mkuu
Ni kweli. But u are between a hard rock and a stone right now. Uko kwenye position mbaya sana. I wish ungekuja kuomba ushauri kabla ya kuanza kuishi nae (baada ya mahari). Mimi ningekushauri kwa herufi kubwa; USIANZE KUISHI NAE,HADI BAADA YA KUAPA KANISANI.
Ila sasa umeshakosea pakubwa sana. Yaani ulipo sasa ni kuomba Mungu tu hilo la kwenda kuoa mwingine lisitokee, you dont have much to do zaidi ya kusubiri "neema" zake huyo mwanaume awiwe kukuoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…