mdaumzalendo1
Member
- Feb 2, 2018
- 76
- 50
Habari wadau;
Kuna binti hapa mtaani amejifungua siku za karibuni.Huyu binti alihamia hapa mwaka juzi na jamaa mmoja ambaye alikuwa akimpa mapenzi sana na kwa kweli tulipenda couple yao.Binti alikuwa mdogo na jamaa pia alikuwa mdogo na walikuwa na maisha ya kawaida ya upendo.Kuna wakati huyu bwana hakuwa akilala hapa au alikuwa anaondoka jioni lakini hatukujali tukafikiri ni mambo ya kazi.
Baadaye ndo tukagundua kuwa huya kijana tayari ana mke na watoto tena sio mbali na hapa.Tulimweleza huyu binti lakini hakutuelewa inaoneka alikuwa amelewa.Mapenzi yaliendelea vizuri tu.Hali ilianza kubadilika mwanzoni mwa 2017.Kwanza huyu bwana alitaka binti aondoke,kwa madai ya kukosa uaminifu.Kesi ilifika mpaka serikali ya mtaa binti akisema mume wako anataka kumfukuza nyumbani.Yule bwana akamwambia poa kaa.Hawakutupa taarifa hasa za tatizo lakini baadaye tuligundua kuwa kumbe yule binti hapo kati alichepuka na jamaa akapata ushahidi wa picha ndio kiini cha ugomvi wao
Basi wakiendelea kuwa pamoja ingawa hali ilikuwa tofauti kidogo.Mwezi wa nne yule bwana akasimamishwa kazi na baada ya hapo alihama kabisa kwa yule binti akawa anakuja mara moja moja.Akamwacha yule binti peke yake bila matumizi wala kumlipia kodi.Akawa anakuja tu mara akae siku mbili na kuondoka.
Baadae tukagundua kuwa yule binti ni mja mzito na yuko peke yake.Kwa kweli aliishi maisha magumu sana peke yake kwa miezi tisa kisha akajifungua salama na sasa mtoto ana miezi miwili na huyo bwana hajatokea bali binti anasaidiwa na majirani na ndugu na binti hataki kuhama hapa kwa sababu anamsubiri mume wake na anadaiwa kodi ya miezi minne sasa.
Mwenye nyumba amekwama kwani akimpigia yule bwana anamwambia tu kuwa atakuja kulipa ila hatokei na binti yuko na mtoto mchanga hana kazi yoyote.
Nimewaza tu na kujiuliza hivi kweli huyu bwana atarudi tena kwa huyu binti?na je kweli huyu binti atakuwa na tatizo gani mpaka akubali kuteseka kiasi hiki akimsubiri mwanaume tena mume wa mtu?Au kuna dawa huyu bwana amempa
Tujadili kwa uwazi na tujifunze.Hii ni true story