Amekuwa na mahusiano na Boyfreind then Mchumba wake kwa miaka minne na nusu. Kwa mara ya kwanza amemkamata akicheat. Anasema boyfriend wake alikuwa amuelewielewi kwa siku mbili hivi, akaamua kufanya ambushi usiku wa saa tano kwa mchumba wake. Looh!! akamkamata mpenzi wake na msichana mwingine live bila chenga. Aligundua pia mchumba wake na huyu mfumaniwa walikutana wiki moja iliyopita. Mchumba wake alimwalika mfumaniwa waspend usiku huo. Kwa hasira mdada akavunja mahusiano na jamaa mda uleule kwa hasira na kusepa.
Sasa imepita wiki mbili, jamaa anaomba msamaha na kuomba msamaha kwa second chance. Kitu ambacho kinamuumiza sana ni kwamba msichana aliyemfumania yupo tofauti sana na yeye. Mfumaniwa kwa kweli kakamilika kila idara, namba nane Yeye wa kawaida sana.
Amesema Mchumba wake amemwambia kosa hilo amefanya kwa mara ya kwanza, mdada amekubali kuwa ni kweli anaamini ni mara ya kwanza. Mchumba wake anataka waende mbele na plan yao ya kufunga ndoa.
Nimemuongelea hapa kwa wana MMU ili mimi niprint the best advice, japo mimi nami nimesha mpa ushauri wangu ila hapa MMU funga kazi.
Madada kama wewe umevaa viatu vyake utafanya nini? Utamsamehee a cheat?