Amemaanisha mimi KITORA au NINA GUNDU?

Tit4tat

Member
Joined
May 31, 2022
Posts
58
Reaction score
171
Habari wanajukwaa,

Leo asubuhi imetokea sitofaham nilipoenda mashinen kusaga nafaka..

Niliishiwa unga ghetto nikaenda mashnen kusaga mahindi, nilipofika tu msagaji akaniulza utasaga kg ngapi nikamwambia tano tu. Mahindi yanauzwa hapo hapo.

Jamaa akanambia wiki ilopita nilipokuja kusaga hakupata hela, yaani hakupata wateja wa kununua Mahindi na kusaga.

Kwaiyo biashara nkiifungua mimi atakosa wateja wa kutosha kwa sababu siku niliyoanza kuhudumiwa mimi hakupata hela.

Kiukweli nilijisikia vbaya, akasema nkihtaj nikanunue Mahindi sehem nyingne halaf yeye atanisagia, binafsi nikaona kanidhalilisha nikaenda kusaga sehem nyingne sikurud tena kwake.

Wafanya biashara(walimwengu) hii imekaaje, siku ya leo nimekosa amani kabsa kutokana na tukio hilo..

NB: Jamaa wa mashnen sina utan nae hata kidogo ni mtu mzima (40-50 miaka).

Najiulza kaniona mi KITORA au NINAGUNDU?
 
Hayo mambo yapo sana sana na kama ilitokea hivyo kweli basi huwa anaweka kumbukumbu za mteja wa kwanza
 
Uwe unaoga mkuu na kupiga mswaki kabla ya kutimba kitaa, watu wa type yako mnatuletea gundu kwenye harakati zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…