Ameandika Mwanahabari Dotto Bulendu

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,427
32,196
Inawezekana waliotufundisha na wale tuliosoma nao ambao wana nafasi ya kusema na kushauri wameamua kukaa kimya.

Hivi hatuoni ama tunaona wachache ama tunaoona hatuoni vizuri?

1.Asilimia kubwa ya watumishi katika sekta binafsi nchini Tanzania sasa hawana uhakika na maisha,wengi wana zaidi ya miezi sita bila mshahara,hili halihitaji mjadala juu ya mwelekeo wa nchi yetu na namna ya kuinasua sekta binafsi?

2.Leo ukitembea mikoa yote mabango ya matangazo yapo matupu,yawezekana makampuni yamepunguza kwa kiwango kikubwa bajeti ya matangazo kutokana na mazingira ya biashara,hili halihitaji mjadala juu ya hali ya biashara nchini?

3.Makampuni kila kukicha yanatangaza kupunguza watu na hivi juzi shirika la umma(TTCL),limetangaza kupunguza watumishi wapatao 555,(kwa mujibu wa Tangazo lililoonekana mtandaoni),na tunaambiwa wanaopinguzwa eti hawajui kutumia teknolojia,hivi inaingia akilini?sekta binafsi ndiyo inapunguza kila kukicha huku ikisimama kuajiri,hili nalo halihitaji mjadala?ama sisi wengine tunatazama haya mambo vibaya?

4.Kundi kubwa la vijana waliohitimu elimu ya chuo,taasisi za juu na vyuo vikuu na bahati mbaya hata lile lililokwenda JKT baada ya kumaliza elimu ya juu,lipo mtaani linasubiri ajira kwa mwaka wa tatu sasa,hawa watu tunawapeleka wapi?hivi suala la ajira kwa vijana siyo mjadala?ama sisi wengine tunatazama mambo vibaya?

5.Walio kwenye ajira ndani ya sekta ya umma na binafsi karibu mwaka wa tatu sasa wanakilio cha nyongeza ya mishahara,hivi hili nalo siyo mjadala?tunajua athari za watu kukaa wakilalamika moyoni?

6.Tunaambiwa mpaka sasa viwanda zaidi ya 3000 vimejengwa nchini,tukiuliza viko wapi?maana vile alivyojenga Mwalimu kuanzia Tabora mpaka Mara,akaenda Mbeya Mpaka Kilimanjaro vingi bado ni maghala ya vyuma chakavu.Maana Mwalimu akijenga viwanda karibu mia nne na mashirika ya umma karibu 180,matokeo yake yalionekana kwa macho kila kona ya nchi,hivi elfu 3 na zaidi vipo wapi na vinafanya nini?Ama sisi hatutazami vizuri haya mambo?

7.Kuna watu walipotea(Ben Saanane,Azori Gwanda),mpaka leo hatujui wapo wapi?waziri wa Mambo ya ndani alipata kuulizwa kuhusu walipo watu hawa,akasema yawezekana wamekwenda kutembea!hivi kweli hili ni jibu sahihi?ama sisi wengine tunatazama mambo haya vibaya?

8.Juzi nilikuwa nasafiri kwa usafiri wa Anga,wakati natafuta tiketi nikashangaa kukuta ndege ya shirika la umma,bei zake ni juu kuliko ndege za makampuni binafsi?nikajiuliza mbona tulikubaliana ndege za serikali zitakuwa nafuu kwa kila mtanzania?au sisi tunatazama haya mambo vibaya?

9.Nenda leo vituo vya mafuta uine kasi ya upandaji wa bei ya mafuta,unajiuliza mbona zamani bei ilikuwa ikipanda tunasikia sauti za walaji na serikali inajibu?leo kila mtu anayasikilizia haya mambo moyoni.Au sisi ndiyo tunatazama haya mambo vibaya?

10.Haya tuliambiwa miaka mitano iliyopita kuwa Gesi ndiyo mwarobaini wa shida za watanzania,baadae Gesi si hoja tena sasa ni umeme wa maji,unajiuliza hivi uwekezaji wetu kwenye gesi umetupa faida ama lah?au sisi ndiyo tunatazama haya mambo vibaya?

11.Tukienda Halmashaurini tunaambiwa aaaah,siku hizi mambo yamebadirika kila kitu serikali kuu ndiyo maana mambo hayaendi,unajiuliza mbona hili halijadiliwi?ama sisi ndiyo tunatazama vibaya?

12.Jana Rais kauliza ipo wapi sekta binafsi?kwani zabuni zote alizotangaza sekta binafsi haikumudu,kama Rais anakiri kuwa sekta binafsi ni dhaifu na tuna sera ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi,kama sekta binafsi ni dhaifu je serikali izibeze ama ilikuze?

13.Uandikwaji wa katiba ama kutokuandikwa si matakwa ya kiongozi,chama ama kikundi cha watu,ni suala la mazingira,wakati na mabadiliko ya kifalsafa.

14.Sasa tunashuhudia baadhi ya wakuu wa Wilaya na mikoa wanatatua matatizo kwa njia ambayo unabaki kujiuliza hivi hii ni sawa?

15.Lissu alipigwa Risasi mchana katikati ya makao makuu ya nchi,Mohamed Dewji alitekwa na watu wasiojulikana,kila tukisubiri kuona watuhumiwa wanasakwa,wanakamatwa na kufikishwa mahakamani tunaona siku zinaenda,au sisi wengine hatutazami mambo sawasawa?

Haya mambo hayaaa?Nawaza sana mimi.

Ila napongezaFrederick Katulanda:
juhudi zote za ujenzi wa reli ya Kati ,tukifanikiwa masikini wengi watapata nafuu,ila ni vizuri tukafungua uwanja wa mjadala juu ya maendeleo endelevu ya taifa leo.

Nawaza tu baada ya kuutazama mjadala wa jana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
Siku jiwe akijichanganya afanyiwe interview na huyu Dotto Bulendu hapo ndiyo watanzania watajua jiwe ni mweupe yani hajui anachokifanya
Jiwe mwenyewe alikimbia mdahalo wakati wa uchaguzi, unafikiri sasa hivi atakua tayari kufanya interview na chombo chochote
 
Daaah huyu mwandishi ameandika vitu vya msingi sana lakini kwa kua nchi ishapata kisima chake cha maarifa haya kwa sasa sio kipaumbele
 
.Tunaambiwa mpaka sasa viwanda zaidi ya 3000 vimejengwa nchini,tukiuliza viko wapi?maana vile alivyojenga Mwalimu kuanzia Tabora mpaka Mara,akaenda Mbeya Mpaka Kilimanjaro vingi bado ni maghala ya vyuma chakavu.Maana Mwalimu akijenga viwanda karibu mia nne na mashirika ya umma karibu 180,matokeo yake yalionekana kwa macho kila kona ya nchi,hivi elfu 3 na zaidi vipo wapi na vinafanya nini?Ama sisi hatutazami vizuri haya mambo?
Ni viwanda vya matofali na vya kushonea nguo (vyerehani)! wewe ulitarajia kuona li- factory likubwa kama yale ya mwalimu Nyerere?
 
Mtu unakaa mwanza uje kuona viwanda vilivyoanzishwa na serikali ya jpm huku pwani kwl?yani uione cherehani lile dude is kufyatulia tofari wakati wewe uko mwnz sisi tupo pwani hahahaaaaaa bt huyu jamaa yuko vizuri sana bora umsikilize yeye kuliko wale maprofeseri wa juzi udsm
 
Hataki kuulizwa. Ila inabidi tubadilishe kitu, hatutafika mbali kwa namna hii
 
Au sisi wengine tunatazama vibaya? Zile Milion 50 kila kijiji ziko wapi au hatukusikia vizuri, Noah zetu vipi au pengine tunatazama vibaya?
 
Au sisi wengine tunatazama vibaya? Zile Milion 50 kila kijiji ziko wapi au hatukusikia vizuri, Noah zetu vipi au pengine tunatazama vibaya?
Kuna waziri alisema, "Lais arishazireta, kupitia miladi ya maenderewo"
 
Pamoja na yote hayo kwa nini sasa lichama lenu chadema linakufa? Kwa nini hampati sapoti ya Wananchi?
 
Back
Top Bottom