Amchoma kisu mkwewe, utumbo nje- Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amchoma kisu mkwewe, utumbo nje- Mbeya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 31, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MSENEGALI Mwakalambile [38] mkazi wa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, amejichukulia sheria mikononi kwa kumchoma kisu cha tumbo mkwe wake na kusababisha kumuacha utumbo wake ukiwa nje na kupeleka kifo chake.
  Mkwe huyo alitambulika kwa jina la Ponali Mwalingo aliuawa kwa kile kilichodaiwa kutokea kwa ugomvi wa kindoa, tukio hilo la mauaji lilitokea Mei 29 , mwaka huu majira ya jioni wilayani humo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Bw. Advocate Nyombi alisema, mtuhumiwa alikwenda kwa marehemu huyo kwa lengo la kwenda kumchukua mke wake aliyefahamika kwa jina la Bertha Ponali (36) ili aweze kurudiana nae baada ya kutengana kwa muda mrefu kutokana na ugomvi kati ya wanandoa hao.

  Katika tukio hilo mtuhumiwa mara baada ya kukatazwa kwa maneno asiondoke na mke huyo alichukua kisu na kumchimba nacho tumboni mkwe wake na kusababisha utumbo wake kumwagika chini dakika hizo hizo. Mkwe wake alifariki dunia dakika chache baadae.

  Katika tukio hilo mtuhumiwa pia alimjeruhi mke wake huyo na mara baada ya hapo alitoweka na hajulikani alipokwenda na jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo.
   
 2. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mbona wanandoa wanachinjana sana cku hz?
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bila shaka hili ni suala la mapenzi! Siasa haina nafasi na wachagga hawahusiki kabisa!
   
Loading...