Ambitions za watoto wa Tanzania ya leo!

Ambitions za watoto wa Tanzania ya leo!

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,828
Miaka ile ya themanini na ushee mambo yalikuwa hivi...

Baba:Mwanangu unapenda kufanya kazi gani ukiwa mkubwa?

Mtoto:Nataka kuwa dokta au nesi au rubani

Baba:Jitahidi usome sana mwanangu!

Miaka ya elfu mbili mwanzoni

Baba:Mwanangu unapenda kufanya kazi gani ukiwa mkubwa?

Mtoto:Nataka kuwa mtaalamu wa kompyuta!

Baba:Jitahidi kusoma lakini bahati mbaya sina uwezo wa kukununulia kompyuta ya kufanyia mazoezi.

Mtoto:Usihofu baba,nimeshajiunga na yahoo ukipenda nitakufungulia email account!

Baba:safi sana mwanangu una akili sana!nitakupa mia tano kila siku ya kwenda internet cafe!

Mwaka 2014

Baba:Mwanangu ungependa kuwa nani baada ya kumaliza masomo?

Mtoto:Mwanasiasa au waziri

Baba:mbona ukoo wetu hakuna talanta za uongozi?isitoshe mimi baba yako sina mchongo wowote kwenye kamati ya chama.

Mtoto:Usihofu baba kwanza nimeshajifunza matusi ya kutosha,pili nina mpango wa kupiga kadiploma kangu ka mwaka mmoja halafu najiunga na uvccm tawi la lumumba buku 7...au kama vipi najiunga na clauds fm!

Baba:safi sana mwanangu kwa sababu watangazaji wa TBC nafahamiana nao.Halafu fani ya kutangaza football haina watu kabisa.nitakufundisha michongo ya kifisadi,huu ndio mpango mzima...mambo ya kukomaa na masomo ya miaka mingi ni ufala halafu unazidi kuniletea umasikini!
Ngoja nimwambie mama yako tumeshatoka kimaisha!
 
hakika ndo hali halisi mtoto wa leo siosawa na wazamani,hadi walimu wa waleo wanaitwa walimu wa google vilevile wanafunzi wa google,je tutafikia malengo na mipango mizuri aliyotuachia mwalim?
 
hii nchi inasikitisha eti mwigulu, nkamia mawaziri....amabao wanataka kuleta maendeleo kwa taifa....kweli
 
Analogia to digitali.....!!! Big result now
 
hakika ndo hali halisi mtoto wa leo siosawa na wazamani,hadi walimu wa waleo wanaitwa walimu wa google vilevile wanafunzi wa google,je tutafikia malengo na mipango mizuri aliyotuachia mwalim?

chakushangaza wana google lkn bado wanafeli mitihani
 
BRN itaruhusu watoto/wanafunzi kuingia na iPad kwenye mitihani kwani kigoogle nako kunahitaji ujuzi
 
hii nchi inasikitisha eti mwigulu, nkamia mawaziri....amabao wanataka kuleta maendeleo kwa taifa....kweli

hawa vilaza wote cjui watatufikisha wap? Na ndo walikuwa wanakoma bunge lipitishe sheria kandamizi ya vyombo vya habar
 
Back
Top Bottom