Ambao hatuna Magari tukutane hapa!

Ambao hatuna Magari tukutane hapa!

Africa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
1,504
Reaction score
2,275
Vipi wakuu mko poa?
Makonda wa daladala wanasemaje.....Mnadai mia au mnapotezea?

Haya turudi hapa

Leo asubuhi nilienda dukani, mara baada ya kuhudumiwa nikawa nasubiri mkate wangu wa chai anikabidhi....Akaja mama mmoja hivi anagari moja hivi nyeusi kali imepanda hewani, Tairi zake zote nne zipo juu juu yaani inanesa nesa tu

Mama akashuka na kuja dukani huku gari inakimuungurumo fulani hivi cha chini chini wamiliki wanasema "sailensa"

Mama kajifunga kitenge na kisuruali mbano kipo ndani cheupe daah lahaula.....

Moyo umeniuma sana kwanini watu wanamagari mimi sina ...Nitawaeleza nini watoto

Je waliyonayo wamefanya vipi ili kuyapata!? Je wote wamekopa? Je kwa biashara zao wafanyazo? Ni zipi hizo!? Je mitaji ya biashara hizo walitoa wapi? Urithi au waliuza mali za familia?

Na sisi ambao hatuna magari tufanyaje ili tumiliki ndinga kali? Huwa unajisikiaje unakula lifti kwa mshkaji aliyekuzidi umri na ana ndinga kali wakati ww pia unanguvu zako?

Embu tujadiliane hapa, mbinu njia au ubunifu wowote utakao tusaidia kumiliki ndinga bhana

Nawasilisha mheshimiwa spika!!
 
Back
Top Bottom