Ukimkosoa utaambiwa kwani Lowassa angeweza kufanya hili au lile? Mara mabadiliko hayakuwa kuzungusha mikono mara kejeli hizi na zile. Wanachosahau ni kwamba sisi ambao hatukumchagua kumkosoa tunamsaidia sana badala ya kumpigia vigelegele. Sisi hatujuti hata kidogo kumchagua huyo tuliyemchagua hata kidogo
Ndiyo! Tujute kwa nini? Kwa vile sukari inapatikana na kwa bei ya chini? Au kwa vile ametumbua watumishi hewa? Alafu? Nafuu iko wapi baada ya zoezi hilo? Au kwa sababu waziri mkuu alitumbua watu bandarini? Hivi mnajua kwamba mpaka leo kuna maroli ya watanzania wenzetu 23,000 yamepaki kwa kukosa mizigo? Na mnajua magari 23,000 ukihesabu dereva na utingo wake tu umesimamisha ajira za watu 66,000?
Au tujutie kutomchagua wakati watalii 8,000 wamekatisha ziara ya Tanzania kwa sababu serikali wameongeza kodi! Ni vijana wangapi watakosa ajira kwa sababu ya uamzi huo? Hivi aliposema anatetea wanyonge anamanisha nini? Au hajui wanyonge ni kina nani?
Hivi wale watoto wa UDOM hawakuwa wannyonge? Mimi nawajua wanane wanyonge kabisa! Mbona tuliambiwa waliokuwa na sifa watafanyiwa utaratibu? Ni wakati wa matokeo ya wenzao wa kidato cha sita, waziri si awaunganishe na hawa kama halikuwa changa la macho?