Amatus Liyumba ashinda kesi

Amatus Liyumba ashinda kesi

Eberhard

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
1,151
Reaction score
809
Amatus Liyumba.
MKURUGENZI wa zamani wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ameshinda kesi ya kukutwa na simu gerezani iliyokuwa inamkabili hivi punde katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Liyumba ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa Jamhuri na mchunguzi wa kesi hiyo kushindwa kuithibitishia mahakama kuhusu tuhuma hiyo. Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando kuanzia saa 3:30…

Amatus Liyumba.
MKURUGENZI wa zamani wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ameshinda kesi ya kukutwa na simu gerezani iliyokuwa inamkabili hivi punde katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Liyumba ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa Jamhuri na mchunguzi wa kesi hiyo kushindwa kuithibitishia mahakama kuhusu tuhuma hiyo. Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando kuanzia saa 3:30 mpaka 4:20 asubuhi.
 
huyu jamaa kinachomsumbua ni fitina za watu.....ila huwa nina amini kwamba adui yako ndie anayetengeneza future yako.....
 
Umewahi kusikia mtu aliyeiba mabilioni akifungwa? Ila aliyeiba kuku, shingi laki, n.k.
 
huyu jamaa kinachomsumbua ni fitina za watu.....ila huwa nina amini kwamba adui yako ndie anayetengeneza future yako.....
kwa kuiingiza hasara serikalina watanzania tsh. bil 220. you are not serious.
 
kwa kuiingiza hasara serikalina watanzania tsh. Bil 220. You are not serious.

tatizo mbona wengine wamepona? Au yeye ni mbuzi wa shughuli? Au alikuwa mnoko? Au alidhulumu mgao?....ndo maana narudia kusema kinachomsumbua ni fitina za WATU........ungejua watu hupiga bao kiasi gani hiyo BIL 220 isingekushangaza....hii ndo TZ......
 
mzee wa totoozi yupo huru,sijui ataendeleza libeneke lake au kaishiwa! ila hawa wazee hatari kwa visichana kuna mkurugenzi mkuu wa bank moja maarufu hapa mjini,nipo naye mtaa mmoja anashughulika na vitoto mpaka aibu.
 
Karibu uraiani tena Mzee wa RAV4 nyekundu.
 
Huyu jamaa mbishi sana yy anakula vitu ya wazee anategemea nini na akome
 
Clarification required...

Kesi ya kukutwa na simu gerezani sio kesi iliyomtia hatiani hata awe gerezani. Kwa hiyo sidhani kwa kushinda kwake kesi ya kutuhumiwa kuwa na simu gerezani kumemfanya kuwa huru?? Wataalamu wa maswala ya kimahakama tujuzeni...

PP
 
vibinti vitafanya sherehe mtaani predeshee wao katia timu
 
Hii miaka sita mpaka nane imekuwa shubiri kwa Mzee Liyumba. Popote alipo au atakapokuwepo, anajua fika sasa, cheo ni dhamana tu na there is thin line between love and hate!
 
hii sio sababu ya huyu mtu kufungwa.
okay, asante kwa kukiri kuwa jamaa alituingiza mkenge wa bil 220.
haya sasa hebu niambie mimi na wengine wasiojua kama mimi sababu ya liyumba kufungwa.
 
tatizo mbona wengine wamepona? Au yeye ni mbuzi wa shughuli? Au alikuwa mnoko? Au alidhulumu mgao?....ndo maana narudia kusema kinachomsumbua ni fitina za WATU........ungejua watu hupiga bao kiasi gani hiyo BIL 220 isingekushangaza....hii ndo TZ......
okay, asante kwa kukiri kuwa jamaa alituingiza mkenge wa bil 220.
haya sasa hebu niambie mimi na wengine wasiojua kama mimi sababu ya liyumba kufungwa. tafadhali hebu nitajie hao wengine. maana ninachojua ni kuwa kweka alionekana hahusiki.
 
Clarification required...

Kesi ya kukutwa na simu gerezani sio kesi iliyomtia hatiani hata awe gerezani. Kwa hiyo sidhani kwa kushinda kwake kesi ya kutuhumiwa kuwa na simu gerezani kumemfanya kuwa huru?? Wataalamu wa maswala ya kimahakama tujuzeni...

PP

Mkuu,

Alishamaliza kutumikia adhabu yake ya miaka miwili jela kuhusiana na ubadhilifu wa fedha katika ujenzi wa Twin Towers. Yupo huru kitambo.
 
Clarification required...

Kesi ya kukutwa na simu gerezani sio kesi iliyomtia hatiani hata awe gerezani. Kwa hiyo sidhani kwa kushinda kwake kesi ya kutuhumiwa kuwa na simu gerezani kumemfanya kuwa huru?? Wataalamu wa maswala ya kimahakama tujuzeni...

PP
si alishamaliza kifungo?yuko huru
 
Ulisha sikia fisadi amefungwa hapa Tanzania? Sana sana wanaofungwa ni wezi wa kuku
 
Back
Top Bottom