kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajiwa kufanya Mkutano wake Mkuu Maalumu Jumamosi wiki hii mjini Dodoma, kwa lengo kuu la kubadilisha uongozi wa juu wa chama hicho tawala na kikongwe hapa nchini.
Mwenyekiti wa sasa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete anang’atuka na anatarajiwa kumkabidhi hatamu za uongozi wa chama hicho Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli mbele ya wajumbe wa mkutano huo zaidi ya 2,400.
Wajumbe wa mkutano huo wameshaanza kuwasili mjini Dodoma na tayari vikao vya awali kabla ya mkutano huo maalum vimeanza.
Vikao vinavyoanza leo na kuendelea hadi mwishoni mwa wiki utakapofanyika mkutano maalum ni pamoja na vya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, Mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Hakuna ubishi kwamba CCM ni chama kikongwe na chenye uzoefu wa kutosha wa masuala ya kisiasa na utawala wa nchi na kwamba orodha ya mikutano hiyo, kama inavyoainishwa ni ushahidi tosha kwamba chama hicho kinajua sawia kile kinachotaka katika ulingo wa kisiasa.
Sisi tunachukua nafasi hii kwapongeza wote wanaohusika na maandalizi ya mkutano huo mkuu na wa aina yake kutokana na unyeti wake wa kupata uongozi wa juu wa chama hicho.
Bila shaka wajumbe wa mkutano huo, watakuwa tayari kuonesha wenzao wa vyama vya upinzani kwa kuendesha shughuli hiyo nzito na ya kihistoria kwa amani, utulivu na mshikamano mkubwa hadi kufikia hatua ya kupatikana kwa safu mpya ya uongozi mpya bila kuleta vurugu na mifarakano.
Ni wakati mwafaka wa chama hicho, kutoa funzo la kuendesha masuala ya kisiasa kwa haki na ustaarabu unaokubalika kidemokrasia kwa kuhakikisha kwamba nguvu ya hoja, ndiyo inayotawala katika vikao husika na siyo hoja za nguvu, ambazo hatima yake huishia katika kuvuruga amani na utulivu wetu.
Sisi tunautakia mkutano huu maalumu wa CCM kila la heri kwa kuonesha ukomavu wa kisiasa, unaotarajiwa na Watanzania bila kuingiza matakwa binafsi, yatakayoweza kuharibu kazi nzuri inayoendelea kufanywa na chama hicho ya kulinda na kudumisha utamaduni wetu wa amani, utulivu na mshikamano.
Chama hicho pia kitekeleze majukumu yake katika mkutano huo bila kushabikiwa na masuala yanayoleta miparaganyiko katika nchi, kama vile ubaguzi wa rangi, ukabila, dini na ubaguzi wa kijinsia. Palipo na wengi pia huwepo mengi.
Hapa tungependa kuvikumbusha vyombo vya dola hususan vile vyenye dhamana ya usalama wa raia moja kwa moja kwa maana ya Polisi, kuhakikisha kwamba jaribio lolote la kuleta vurugu, lisipewe nafasi kwa kuhakikisha kwamba wahusika wanashugulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Mungu Ibariki Tanzania.