Ama kweli ukipenda boga, penda na ua lake!

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Wakuu Salam kwenu,

Nimelazimika kuupa huu uzi kichwa hicho kutokan na story niliyopewa na mfanyakazi mwenzangu.Nirafiki yangu sana tangu alipoajiriwa kwenye taasisi hii miezi9 iliyopita.

Dada huyu amenieleza kuwa alikutana na mumewe miaka kadhaa nyuma nakufanikiwa kuzaa mtoto mmoja kabla ya ndoa.

Anadai wamebariki ndoa yao(sio kufunga) December mwaka jana .
Baada ya ndoa jamaa kaamua amletee huyu dada wanae wa4 alozaa nawanawake tofauti kabla yakuoana na huyu alienae.

Wakuu,huyu dada anadai kwa kuwa ameamua kumpenda huyu jamaa inabidi akubali pia kuwalea Hawa watot alioletewa japo anakiri kuwa nikazi ngumu kwake.

Mdada huyu ana miaka30 saivi Ila watoto alioletewa wote niwakubwa kwani mmoja yupo kidato Cha kwanza, wawili darasa la7 na waliobaki darasa la5 na la6.

Jamaa yake ni baba wanyumbani ambae kila kitu anamtegemea huyu mdada,kuanzia kula,kuvaa na pakulala.
Kuna wakati anaonekana mwenye mawazo Sana huku akionekana kujutia maamuzi yake yakuwakubali hao watoto.

Nimejaribu kumtia moyo kuwa pamoja naugumu wa maisha Ila ajitahidi hivyo hivyo kuwalea kwani Kama nikosa alishalifanya baada yakukubali kuwapokea.

Naomba kuuliza,ni idadi gani yawatoto upo tayari kuivumilia punde mwenzi wako anapokuletea nyumbani ili kuwalea?

Wasalaam!
 
Atakua anamkuna vizuri tu hapo nothing else!!
Huyo mwanaume si akatafute kazi Mbona nyingi sana jamani!!
Huyo Dada anapenda vibaya!
 
Hapo na yeye apambane na ujinga wake
Kwanini amekubali kuolewa na mwanaume suruali
Basi tusikufuru kumlelea hao watoto hata nayeye analelewa jamanimbona hatari sana hio Uwiii!!
Kamuona huyo mwanamke ni zuzuu!! kupenda gani hukoo!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom