Ama kweli mwenye macho haambiwi "tazama"...

Konakali

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
1,533
263
Hata bila kutumia miwani wala kufikiria, nashuhudia ahadi za CHADEMA zikianzishiwa michakato na mijadala ya kutekelezwa na serikali ya CCM, ilihali kati ya ahadi za CCM zipatazo takribani 86 sioni hata moja ikiwa kwenye mchakato wa kutekelezwa....! Baadhi za ahadi hizo ni kama ifuatavyo;

  1. Katiba Mpya: Na sote tunaelewa kwamba mchakato umeanza na sio kwa hiari ya serikali ya CCM, bali ni kwa msukumo wa CHADEMA na jamii kwa ujumla....!
  2. Elimu bure: Na swala hili limefikishwa mezani na baraza la madiwani huko Moshi, kujadili uwezekano wa Halmashauri kuwalipia wanafunzi ada katika shule za kata ndani ya Halmashauri hiyo...! Hata hivyo unaonekana kupingwa vikali na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, kitu ambacho inanifanya niamini kuwa huo ni mkono serikali ya CCM...!
  3. Kuwashughulikia mafisadi: Kila raia Mtanzania anaelewa kuwa mada ya CCM ya KUJIVUA GAMBA haikuwa kwenye fikra zao na wala sio hiari yao, bali ni kutokana na vuguvugu la CHADEMA, ilhali orodha inaongezeka...! Nazidi kuamini hivi kwa kuwa katika vyama vya upinzani zaidi ya 10, ni CHADEMA pekee ndio iliyowahi na inayoendelea kuanika majina ya mafisadi huku watajwa wakishindwa kujitetea....!
  4. Kuthibiti mfumuko wa bei ya vitu: Na ndio maana pamoja na kutochukuwa dola kwa namna moja ama nyingine, CHADEMA waliamua kuandaa maandamano kadhaa nchini iliyopelekea serikali ya CCM bila kupenda wametamka kuwa bei ya sukari iwe sh. 1,700/- kwa kilo badala ya kuendela kuuzwa kwa sh. 2,000/- na zaidi....!
Sasa binafsi najiuliza maswali yafuatayo;

  1. Je, CHADEMA ingechukua dola, ingekuwa vipi?
  2. Je, CHADEMA isingekuwepo kabisa, hali ingekuwaje?
  3. Je, ni lini basi CCM itaanza kutekeleza orodha ya ahadi zake zaidi ya 80?
Nawasilisha....!
 
Back
Top Bottom