Ama kweli dunia tambala bovu, Aden Rage amepotea machoni na masikioni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,782
239,460
Wakuu, natanguliza salamu,

Kiukweli naomba nikiri kwamba sikutarajia CCM kumtelekeza mfia chama huyu kwa kiwango hiki.

Huyu ndio mbunge aliyeongoza kwa kugonga meza hata kwa hoja zisizo na mashiko kwenye bunge la 10 akifuatiwa kwa mbaaali na wabunge wa viti maalum (CCM).

Kila akinyanyuka bungeni ilikuwa ni kuponda wapinzani na kusifia ccm na kikwete tena katika lugha ambayo ni ya kuudhi na ya kichochezi, hakika malipo ni hapa hapa, leo Rage aliyekuwa tayari hata kuweka bastola kiunoni kwa ajili ya chama chake ni wa kutelekezwa namna hii jamani?

Haya tuachane na CCM, lakini hata mashabiki wa simba mbona hamumtajitaji , mmemsahau vipi mtu aliyeitajirisha timu yenu kwa mauzo ya Okwi? Huyu ndio alihakikisha kwamba dili la Samatta kwenda Mazembe linakamilika, je matunda yake hamjaona?

Ama kweli dunia ni Tambala bovu, hatimaye Rage amebaki kwenye vitabu vya Mahakama tu, kule ambako alihukumiwa kifungo baada ya makandokando yake FAT.
 
Ile ya bastola kiunoni ili nikumbusha sana movie za kina Giuliano Gema,Anthony Stephen na kina Terence Hill ile kuzungumza kwa jazba kukunja uso na kufoka ni gia tu zile hamna kitu, wachina wanakuambia chui wa makaratasi,sijui pengine chama chake kili nufaika naye ila sio timu ya simba zaidi ya kurudishiwa umeme tu ahadi nyingi za kabla ya siku mia hatukuziona mikataba fiksi ya ujenzi wa kiwanja tulisha sahau lakini,sina shaka atakua mitaa ya Rufita Tabora yuko vizuri tu.
 
Rage.jpg


Nasikia amekwenda kujiunga na ISIS
 
Back
Top Bottom