Alshabab VS Tisa December

Malipesa

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
310
32
Ikiwa kutakuwa na taarifa za ki-intelinsia ya kuwepo uwezekano wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya sherehe ya Uhuru wa Tanganyika kushambilwa na Alshabab, basi polisi ipige marufuku kufanyika kwa mkusanyiko wowote mkubwa siku hiyo.

Ni maoni binafsi tu.
 
Hofu hiyo ipo,ndio maana jukwaa la katiba walizuiwa.Lakini sidhani kama ushauri wako utafuatwa.
 
Hao jamaa wanamtandao mkubwa na baadhi ya serikali za nchi za africa mashariki, kwa hiyo ni vigumu kujihusisha na serikali isipokuwa makundi mengine kama vyama vya upinzani. Tutegemee amani tele Tisa Decemba. Ila kama vyama vya upinzani, Jukwaa la katiba namakundi mengine yakitaka kufanya shughuli zao basi jamaa wanapewa ruksa.
 
kweli 9 dec polisi wasiruhusu mkusanyiko wowote uwanja wa uhuru!nime smell al shabab kufanya mambo
 
hakuna kitu kama hicho naomba tusitishwe
kwa sasa Al Shabbab nguvu yao imepunguzwa sana na majeshi ya watu Kenya hadi kufikia 9. Dec itakuwa imekwisha kabisa

Naomba wananchi tujitokeze kwa wingi kusherekea maadhimisho ya miaka 50 ya Tanganyika yetu

KARIBUNI SANA !!!!!
 
Hao jamaa wanamtandao mkubwa na baadhi ya serikali za nchi za africa mashariki, kwa hiyo ni vigumu kujihusisha na serikali isipokuwa makundi mengine kama vyama vya upinzani. Tutegemee amani tele Tisa Decemba. Ila kama vyama vya upinzani, Jukwaa la katiba namakundi mengine yakitaka kufanya shughuli zao basi jamaa wanapewa ruksa.

Du kweli huenda ruhusa wanachukua ruhusa
 
Policcm hapo watafanya vyovyote kuweka ulinzi ila kwa makusanyiko mengine hawapo tayari na garama itakuwa kubwa, ila kupambana na maandamano ya amani wana uwezo na garama yoyote watatumia. Kazi kwelikweli ukifuatilia siasa za Afrika hasa Tz
 
Usihofu mkuu.Tumezungumza na hao mashababi wasitishe maandamano, oooh sorry, wasitishe mashambulizi kwanza kipindi hiki tunapojiuliza katika jubilee hii tumefanya nini na kwa kiasi gani CCM wanamchango katika hilo. Ama maendeleo, au Umaskini. Lakini pia kwa taarifa yako tu, mashambulizi yao yako programmed kwa ajili ya maandamano tu.Hii ni kwa mujibu wa intel yenye jinsia.
 
inaonekana alshaabab na polisi wana mawasiliano zaidi maana ikiwa ni wapinzani tu basi wanaibuka lakini ikiwa serikali/ccm basi alshabab wanakua wako kwao wanakula mirungi

FUNNY!!
 
Mkuu naakubaliana na wewe kuwa Polisi wanamahusiano makubwa na hawa Al Shabab. Inabidi tujiulize, inakuwaje CCM wanavyotaka kuandamana Al Shabab hawa washambulii. Hivi majuzi NEC sijui CC wamefanya mkutano kibao Dodoma lakini hawakushambulia. Na ninaamini kuwa Al Shababu wanapenda sana dini zote, za kiislamu na za Kikristo. Nasema hivyo sababu, polisi hawajawahi kutoa taadhali kuwa kuna hatari kuwa Al shababu watawashambulia waumini wa dini hizo

Alshababu vilevile wanapenda sana michezo. Hatujawahi kusikia kuwa polisi wametoa angalizi kwa wapenzi na washabiki wa mpira wakati wanakwenda au kutoka katika viwanja vya mpira wajitahadhari

Al shababu wanapenda sana wanafunzi. Hatujawahi kusikia wakitaka kulipua mashule au mikusanyiko ya wanfunzi, iwe wa shule ya msingi au vyuoni

Al shababu pia wanapenda sana sherehe ya Uhuru wa Tanganyika. Al shababu wameruhusu Majeshi yetu (ya Polisi, magereza, JW nk.)wanakifanya magwaride kwa ajili ya maandalizi ya DEC 9, Hatujaambiwa kuwa magwarde hayatofanyika sababu ya tishio la Al shababu

Konklusheni; Al shababu hapendi vyama vya upinzani kufanya maandamano na hawapendi watu wote wanaotaka kufanya maandamano ya kupinga mswaada wa katiba. Kinachonisikitisha ni kuwa polisi hawataki kutuambia hilo kwa sababu , polisi wanapata taarifa zote za Al shababu juu ya mashambulizi yao. Kama una hamu ya kufanya maandamano jiunge na CCM
 
Umesahau moja, ALSHABABU WANAPENDA MBIO ZA MWENGE!!
 
Ikiwa kutakuwa na taarifa za ki-intelinsia ya kuwepo uwezekano wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya sherehe ya Uhuru wa Tanganyika kushambilwa na Alshabab, basi polisi ipige marufuku kufanyika kwa mkusanyiko wowote mkubwa siku hiyo.

Ni maoni binafsi tu.

Hakuna Al shabab wala mama yake Al Shabab ni usanii tu unaotumiwa na Serikali ya magamba kupitia kitengo chake kingine, vyombo vya dola, katika kuzuia maandamano ya shinikizo la kudai katiba mpya ambayo yanataka kufanywa nchi nzima.
 
Siku watakapo tinga hapa Tanganyika Al shabab ndio utakuwa mwisho wa Kova au kovu na ujinga wao na Intelejensia yao ya Kipumbavu kama wao wemyewe walivyo, Kova na Mwema kama wanawashwa waende wakawafuate huko Somalia kama vile mshikaji wa Magogoni anavyowafuta wakina Kamaeruni.
 
alishabaab are not aliens they are our kids or relatives and they live among us.wanaweza kulipua wakiamua ila hawana ugomvi na sisi
kama hakuna tishio na sherehe zitakwenda sawa sidhani kama watakuwa na kisingizio tena cha kuzuia maandamano
 
so our kids dont want new constitution, better life, facts and truth, wakisikia hayo tu wanaongea na kova kuwa watalipua

tunacheza kweli aisee

nahisi hao aishababu wa tanzania tumewaumba ili kutishia mdai haki yeyote yule kama USA walivyoumba WMD Irak ili wamuue saddam
 
Back
Top Bottom