Aloyce Tendewa: Shujaa wa taifa, mlinzi wa zamani wa Nyerere na Lowassa

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,369
8,072
Yuko wapi shujaa Aloyce Tendewa? na je sakata lake la kufukuzwa kazi liliishia wapi hasa baada ya habari hii ya mwaka jana iliyoeleza rais Magufuri hakurahishwa na suala la yeye kufukuzwa kazi, isome hapo chini:-

Aliyekuwa mlinzi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ofisa usalama mwandamizi, Aloyce Tendewa, ambaye amefukuzwa kazi, Sasa sakata la mlinzi huyo limefika mezani kwa Rais John Magufuli na kumweka wakati mgumu Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rashid Othuman.

Tendewa ambaye alikuwa mlinzi wa Lowassa katika kipindi cha miaka kumi, alifukuzwa kazi juzi jioni na mwajiri wake ambaye ni Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kwa kosa la kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kikazi.

Mbali na taarifa hizo, imeelezwa pia kuwa sababu nyingine ya kufukuzwa kwake kazi kwa mwanausalama huyo ambayo hata hivyo haijathibitishwa, ni madai ya kutoa taarifa za kubadilishiwa kituo chake cha kazi cha awali.

Taarifa za kuaminika kutoka serikalini ambazo mtandao huu umepenyezewa zinasema sakata la mlinzi huyo tayari limetinga kwenye ikulu ya Magufuli huku likimchukiza Rais na akataka apewe taarifa kamili kuhusu mlinzi huyo.

Kinachotajwa kumchukiza Rais Magufuli kuhusu hatua ya kufukuzwa Tendewa, huku akiwa na historia yake ya ufanyaji kazi wake kwaa uaminifu ndani ya serikali huku akishangaa kufukuzwa kwake kazi.

“Ndugu hili sakata sahivi limekuwa kuwa kubwa sana, hata ajira ya mkurugenzi wa Usalama ipo pamoto sana, maana hili suala la Tendewa limefika kwa Magufuli sahivi, tena Rais kachukia kweli maana mlinzi huyu anahistoria ya kutukuka ndani ya nchi kwahiyo kufukuzwa kwake kazi kama mtu wa aliyekuwa kibarua kumemchukiza Magufuli” akimesema Chanzo chetu hicho.

Sakata hili la Tendewa kufika kwa Rais Magufuli kuna kuja ikiwa ni siku tatu kupita baada ya vyombo vya habari nchini kuripoti juu ya kuondolewa kinyemela kwa mwanausalama huyo kumlinda Lowassa.

Tendewa alishirikiana na mwanausalama mwengine anaitwa Samson Machaba ambao wote kwa pamoja ndio walikuwa walinzi wa Lowassa takribani miaka kumi, ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya ofisi ya Lowassa zinasema kwa sasa Lowassa ameachiwa mlinzi mmoja tu ambaye ni Samsoni Machaba huku Tendewa akirudishwa serikali kabla ya kufukuzwa kazi kwake.

Kwa upande mwingine taarifa zinaeleza kuwa mpango wa kutimuliwa kwa Tendewa uliandaliwa kwa muda wa miezi kadhaa na barua ya kufukuzwa iliandikwa baada tu ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Kwamba, pamoja na sababu nyingine Tendewa anadaiwa kushindwa kuwasiliana inavyotakikana na viongozi wake kuhusu majukumu yake ya kiulinzi wakati akiwa mlinzi wa Lowassa.

Taarifa zinadai, kushindwa huko kwa Tendewa kuliwafanya viongozi wake kufikia uamuzi wa kumfukuza kazi na kwamba barua yake iliandikwa mapema Desemba mwaka jana, lakini hakukabidhiwa hadi hivi karibuni alipovujisha siri za kuhamishwa kwake kituo cha kazi.

Mmoja wa watoa habari aliyeko serikalini ameeleza kuwa Tendewa aliundiwa kamati ya kumchunguza kuhusu kushindwa kutekeleza majukumu sawasawa ambayo ilifanya kazi kwa muda wa wiki mbili na kuwasilisha ripoti yake makao makuu.

Tendewa amefukuzwa kazi akiwa amebakiza mwaka mmoja kustaafu utumishi wake katika Idara ya Usalama wa Taifa

UTATA KUHUSU SAINI YA MTU ALIYEMFUKUZA KAZI
Licha ya kupewa barua juzi jioni kutoka ndani ya (TISS) hata hivyo barua ya kufukuzwa kazi Tendewa imeibuka utata juu ya nani aliyesaini barua hiyo kwakuwa ingetakiwa kusainiwa na mkurugenzi mkuu lakini jambo la ajabu imesainiwa na mtu wa chini.

HISTORIA YA TENDEWA
Rekodi za utendaji kazi wa Tendewa zinaonyesha kuwa baada tu ya kuajiriwa na TISS, alipelekwa katika kikosi cha walinzi wa hayati Mwalimu Julius Nyerere na kutokana na uhodari wake aliaminiwa na Mwalimu.

Aidha, rekodi hizo zinaonesha kuwa Tendewa ni miongoni mwa wana usalama wachache waliopigana vita ya kumng’oa aliyekuwa Rais wa Uganda, Fashisti Iddi Amini Dada mwaka 1978 na 1979 na akiwa vitani alitekwa na kwenda kuzuiliwa nchini Sudan.

Historia hiyo inaonyesha kuwa Tendewa aliokoka kuuawa kwa risasi akiwa mateka muda mfupi baada ya kurejeshwa nchini kutoka Sudan siku chache baada ya Rais Yoweri Museveni kushika madaraka ambapo mmoja wa walinzi wanawake wa rais alimuona na kumtambua kuwa alikuwa mmoja wa wapiganaji hodari wa Tanzania na si muasi kama ilivyokuwa ikidhaniwa hivyo alirudishwa Tanzania.

Baada ya kurejeshwa nyumbani alipewa jukumu la kuwa mlinzi wa Mwalimu Nyerere na hata alipong’atuka madarakani aliendelea na kazi hiyo hadi Mwalimu alipofariki dunia katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas London nchini Uingereza.

f1e7f1a6e329f8e93494a1147d434e52.jpg

ee9e541e313fe203bb7c436576883bee.jpg

0b3f64f8bb750f4135c331ec6cce50f0.jpg
 
We unapenda kumuandama mzee wa watu kweli tangu mwaka jana unae tu daah, sijui unamtafutia nini
 
yuko wapi shujaa Aloyce Tendewa? na je sakata lake la kufukuzwa kazi liliishia wapi hasa baada ya habari hii chini:-

Aliyekuwa mlinzi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ofisa usalama mwandamizi, Aloyce Tendewa, ambaye amefukuzwa kazi,
Sasa sakata la mlinzi huyo limefika mezani kwa Rais John Magufuli na kumweka wakati mgumu Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rashid Othuman.
Tendewa ambaye alikuwa mlinzi wa lowassa katika kipindi cha miaka kumi,alifukuzwa kazi juzi jioni na mwajiri wake ambaye ni Idara ya Usalama wa Taifa (TIS) kwa kosa la kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kikazi.

Mbali na taarifa hizo, imeelezwa pia kuwa sababu nyingine ya kufukuzwa kwake kazi kwa mwanausalama huyo ambayo hata hivyo haijathibitishwa, ni madai ya kutoa taarifa za kubadilishiwa kituo chake cha kazi cha awali.
Taarifa za kuaminika kutoka serikalini ambazo mtandao huu umepenyezewa zinasema sakata la mlinzi huyo teyari limetinga kwenye ikulu ya Magufuli huku likimchukiza Rais na akataka apewa taarifa kamili kuhusu mlinzi huyo,
Kinachotajwa kumchukiza Rais Magufuli kuhusu hatua ya kufukuzwa Tendewa ,huku akiwa na historia yake ya ufanyaji kazi wake kwaa uaminifu ndani ya serikali huku akishangaa kufukuzwa kwake kazi.
“Ndugu hili sakata sahivi limekuwa kuwa kubwa sana,hata ajira ya mkurugenzi wa Usalama ipo pamoto sana,maana hili suala la Tendewa limefika kwa Magufuli sahivi,tena Rais kachukia kweli maana mlinzi huyu anahistoria ya kutukuka ndani ya nchi kwahiyo kufukuzwa kwake kazi kama mtu wa aliyekuwa kibarua kumemchukiza Magufuli”akimesema Chanzo chetu hicho.
Sakata hili la Tendewa kufika kwa Rais Magufuli kuna kuja ikiwa ni siku tatu kupita baada ya vyombo vya habari nchini kuripoti juu ya kuondolewa kinyemela kwa mwanausalama huyo kumlinda lowassa,
Tendewa alishirikiana na mwanausalama mwengine anaitwa Samson Machaba ambao wote kwa pamoja ndio walikuwa walinzi wa Lowassa takribani miaka kumi,ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya ofisi ya lowassa zinasema kwa sasa lowassa ameachiwa mlinzi mmoja tu ambaye ni Samsoni Machaba huku Tendewa akirudishwa serikali kabla ya kufukuzwa kazi kwake.
Kwa upande mwingine taarifa zinaeleza kuwa mpango wa kutimuliwa kwa Tendewa uliandaliwa kwa muda wa miezi kadhaa na barua ya kufukuzwa iliandikwa baada tu ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Kwamba, pamoja na sababu nyingine Tendewa anadaiwa kushindwa kuwasiliana inavyotakikana na viongozi wake kuhusu majukumu yake ya kiulinzi wakati akiwa mlinzi wa Lowassa.
Taarifa zinadai, kushindwa huko kwa Tendewa kuliwafanya viongozi wake kufikia uamuzi wa kumfukuza kazi na kwamba barua yake iliandikwa mapema Desemba mwaka jana, lakini hakukabidhiwa hadi hivi karibuni alipovujisha siri za kuhamishwa kwake kituo cha kazi.

Mmoja wa watoa habari aliyeko serikalini ameeleza kuwa Tendewa aliundiwa kamati ya kumchunguza kuhusu kushindwa kutekeleza majukumu sawasawa ambayo ilifanya kazi kwa muda wa wiki mbili na kuwasilisha ripoti yake makao makuu.

Tendewa amefukuzwa kazi akiwa amebakiza mwaka mmoja kustaafu utumishi wake katika Idara ya Usalama wa Taifa
UTATA KUHUSU SAINI YA MTU ALIYEMFUKUZA KAZI.
Licha ya kupewa barua juzi jioni kutoka ndani ya (TIS) hata hivyo barua ya kufukuzwa kazi Tendewa imeibuka utata juu ya nani aliyesaini barua hiyo kwakuwa ingetakiwa kusainiwa na mkurugenzi mkuu lakini jambo la ajabu imesainiwa na mtu wa chini.
HISTORIA YA TENDEWA.
Rekodi za utendaji kazi wa Tendewa zinaonyesha kuwa baada tu ya kuajiriwa na TIS, alipelekwa katika kikosi cha walinzi wa hayati Mwalimu Julius Nyerere na kutokana na uhodari wake aliaminiwa na Mwalimu.

Aidha, rekodi hizo zinaonyesha kuwa Tendewa ni miongoni mwa wana usalama wachache waliopigana vita ya kumng’oa aliyekuwa Rais wa Uganda, Fashisti Iddi Amini Dada mwaka 1978 na 1979 na akiwa vitani alitekwa na kwenda kuzuiliwa nchini Sudan.
Historia hiyo inaonyesha kuwa Tendewa aliokoka kuuawa kwa risasi akiwa mateka muda mfupi baada ya kurejeshwa nchini kutoka Sudan siku chache baada ya Rais Yoweri Museveni kushika madaraka ambapo mmoja wa walinzi wanawake wa rais alimuona na kumtambua kuwa alikuwa mmoja wa wapiganaji hodari wa Tanzania na si muasi kama ilivyokuwa ikidhaniwa hivyo alirudishwa Tanzania.
Baada ya kurejeshwa nyumbani alipewa jukumu la kuwa mlinzi wa Mwalimu Nyerere na hata alipong’atuka madarakani aliendelea na kazi hiyo hadi Mwalimu alipofariki dunia katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas London nchini Uingereza
f1e7f1a6e329f8e93494a1147d434e52.jpg

ee9e541e313fe203bb7c436576883bee.jpg

0b3f64f8bb750f4135c331ec6cce50f0.jpg
ndo hali halisi siyo hapo tu hata huku kwa walala hoi uonezi umekithiri
 
Kwani Rashidi Othumani bado ndiye bosi kubwa Tiss?,si alishastafu kwa mujibu wa sheria?,hii kazi ya ushushushu ni ngumu mno kwa kweli!..
 
Back
Top Bottom