kwa-muda
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 2,101
- 5,393
Samahani kwa picha zinazotisha ila hizi picha ni za mwili na damu ya Travis Victor Alexande baada ya kugunduliwa na rafiki zake pale walipoingiwa na mashaka baada ya kutomuona kwa siku tano. Chanzo cha kifo chake ni kutokana na wivu wa kimapenzi uliopelekea mpaka akauawa.
Mwanzo wa safari ya penzi la kifo
Penzi lililopelekea kifo cha Travis lilianzia mji wa Sin City huko Las Vegas mwaka 2006, Travis alikuwa ni mhamasishaji akiwa anahusika katika kutoa nasaha na mafunzo kwenye semina mbalimbali. Akiwa na rafiki yake aliyejulikana kama David, ambaye alikuwa ana rafiki yake wa jinsia ya kike ambaye alikuwa pia ni mwanamitndo akijulikana kama Joddi Arias. Joddi alikuwa hayuko kwenye mahusiano na kwakuwa David alikuwa akijua kwamba Travis naye hayuko kwenye mahusiano aliamua kuwakutanisha na wakaanza urafiki. Baada ya wiki moja tu walikuwa washaanza kufanya mapenzi kwenye gari.
Penzi lilishamiri haraka japo walikuwa wakiishi mbalimbali Joddi akiishi Palm Desert California huku Travis akiishi Mesa Arizona. Ila walikuwa wakitembeleana mara kwa mara, na kuwasiliana mara kwa mara. Joddi alikuwa akimpenda sana Travis hadi akaamua kubadiri dini kuendana na Travis ambaye alikuwa akiabudu katika dhdhebu la Mormon.
Kwa wenzao hasa washirika wenzao waliwaona kwamba ni watu ambao wameshika sheria na kanuni za kanisa hawashiriki kabisa tendo landoa kabla ya ndoa kama ambavyo kanisa linawakataza waumini kufanya hivyo. Kumbe hali haikuwa hivyo walikuwa wakifanya sana ngono tena ngono ile ya kama kwenye filamu za ngono.
Rafiki zake Travis walianza kumchukia Joddi wakawa wakimwona kwamba ana mambo na tabia ambayo ni ya ajabu. David ambaye aliwakutanisha anadai kwamba ilifika kipindi akawa hata hataki Travis akimtembelea aongozane na Joddi maana alikuwa anakosa uhuru akiwa karibu naye. David anadai kwamba Joddi alikuwa ana tabia ya kumfuatilia Travis kila anapokwenda mfano anakumbuka kuna siku Travis alikuwa kwa kaka yake wakizungumza huku pia akiwepo mke wa kaka yake Travis. Mazungumzo yenyewe yalikuwa yanahusiana na Joddi na walikuwa wakijaribu kumshawishi aachane na Joddi. Kumbe Joddi alikuwa dirishani akiwasikiliza pasipo wao kujua. Mara ghafla wakaona anaingia sebuleni akawa anawatazama kwa hasira kisha akamvuta Travis na kuondoka naye.
Katikati ya mwaka 2007, penzi lao lilianza kuyumba kwasababu ya wivu uliopitiliza ambao Jodii alikuwa nao hasa kwakuwa Travis alikuwa anaonyesha matamanio kwa wanawake wengine. Joddi alichukua simu ya Travis na katika kupitia msg aligundua Travis alikuwa na mahusiano mengine na wanawake mbalimbali na hapo hapo aliamua kwamba waachane. Kumbe wakati huo Travis naye alikuwa yuko mbioni kumuacha Joddi.
Japokuwa walianchana lakini waliendelea kutafunana (friends with benefits). Joddi alikuwa akipenda penzi analopewa na Travis kiasi kwamba aliandika hadi kwenye kitabu chake cha kumbukumbu jinsi gani ambavyo Travis anamburudisha kiasi kwamba hajui jinsi gani anavyoweza kumuacha kabisa na kumsahau.
japokuwa walikuwa wameachana ila wakitafunana tu kisela, Joddi hakuacha kumfuatilia Travis, alikuwa anafunga safari na kuanza kumwinda kujua yuko wapi anafanya nini yuko na nani. Kuna wakati ambapo Travis alikuwa akimpiga busu mwanamke mwingine mara Joddi akatokea na mambo mengi tu ambayo yalikuwa yakionyesha kwamba Joddi alikuwa akimfuatilia sana Travis. Kuna wakati hadi alidirika kutoboa tairi za gari la Travis, aliwahi kuhack Facebook account ya Travis, aliwahi kuvunja mlango na kuingia nyumbani kwa Travis akaiba diaries zake, yani alikuwa kachanganyikiwa kwa penzi la Bwana Travis.
Tarehe 4 mwezi wa sita mwaka 2008, Joddi alimtembelea Travis bila taarifa majira ya usku. Travis anamkaribisha wanalala wote na katikati ya usiku wa manane Travis anaamka na wanaanza kufanya mapenzi maana ndiyo ilikuwa burudani yao. katika kufanya mapenzi siku hiyo waliamua kujirekodi kabisa, huku wakipigana picha wakiwa uchi wa mnyama.
Travis anapatikana akiwa bafuni amekufa
Ilikuwa Jumatatu ya tarehe 9 mwezi wa sita mwaka 2008, hakuna ambaye alikuwa ameonana wala kusikia chochote kutoka kwa Travis kwa siku tano mfululizo. Rafiki zake kadhaa wakawa na wasiwasi hivyo wakaamua kuongozana kwenda kwake kumtafuta. Kwa bahati mmoja wao alikuwa akijua namba za siri za kufungua mlango wa sehemu ya kuegesha magari na wakapitia huko kuingia ndani. Wanakaribishwa na harufu mbaya ya uvundo . Ndipo wanapokutana na mwili wa rafiki yao akiwa kashaanza kuoza, mwili ukiwa umeegemea sinki la bafuni na damu ikiwa imetapakaa sakafuni na ukutani.
mara moja wanapiga namba ya dharura kutaarifu vyombo vya usalama. Mwili wake ulikuwa na matundu ya kisu 29, pia akiwa amachinjwa shingo kutokea sikio la kusho kupita shingo mpaka sikio la kulia. Pia alikuwa amepigwa risasi iliyopenya kwenye sehemu ya nyusi za jicho la upande wa kulia. Chumbani kwake kapeti pia lilikuwa limetapakaa damu na kulowa.
Rafiki zake moja kwa moja walikuwa washakuwa na mtu waliyehisi katenda uovu huo na waliwatajia makachero kuwa atakuwa Joddi.
Makachero wanapompigia simu Joddi anawakatalia na kusistiza kwamba yeye hakuwa katika mji wa Mesa na ana miezi kadhaa hajakanyaga mji huo. Alidai kwamba yeye na Travis walionana mara ya mwisho mwezi wa tatu na toka wakati huo hajawahi kuonana naye na wala kukanyaga tena katika mji wa Mesa.
Lakini makachero wanaweza kugundua kitu ambacho kiliwapa uhakika kuwa Joddi alikuwa na Travis kabla na baada ya kuawa kwake. Waligundua alama za kiganja cha Joddi katika mojawapo ya sinki na pia ile kamera waliyokuwa wakitumia kupiga picha wakati wakifanya mapenzi waliikuta ikiwa ndani ya mashini ya kufaua nguo ikiwa imedumbukizwa. Lakini kwa bahati nzuri memory card ya hiyo kamera ilikuwa haijaharibika na waliweza kutoa picha.
*********************************************************************************************************************************************************************************************************
Picha zilizokuwa kwenye memory card ziliweza kuwapa mpangilia wa muda na matukio jinsi yalivyo tokea.
Saa kumi na moja na nusu alfajiri Joddi alitumia kamera kumpiga picha Travis akiwa bafuni anaoga na hii ndiyo ilikuwa picha ya mwisho ya Travis akiwa hai. Makachero wanadai inaelekea kulikuwa na mapambano bafuni ambapo Joddi alimvamia Travis na kumchoma kisu kwa ghafla kisha Travis aliweza jinasua na kukimbilia chumbani ambako Joddi alimfuata huko.
Kutokana na maelezo ya makachero inaonekana Travis alikuwa akitambaa kwa magoti na mikono ambapo Joddi alimkalia mgongoni na kuzidi kumdunga visu vya mgongoni na kisha kumchinja shingo kuanzia sikio la kushoto kupita shingoni mpaka kwenye sikio la kulia almanusuru kutengengfanisha kichwa na kiwiliwili. Kisha inakisiwa aligeuzwa mwili waTravis akaulaza chali na kuuburuza kuurudisha bafuni.
Kuna picha ambazo makachero walizikuta na inaonekana zilipigwa bahati mbaya wakati wa mapambano ya Travis kujiokoa na Joddi kuua huenda walikanyaga kamera ikajifyatua ila zinaonyesha nusu kiwili wili kinachosadikika ni cha Joddi kikiwa juu ya mgongo wa Travis wenye damu.
Kukamatwa kwa Joddi
Makachero walimwomba Joddi afike kituo cha polisi kwa mahojiano pasipo kumwambia kwamba tayari wana ushahidi. Katika mahojiano Joddi aliendelea kukana kabisa kuwa hata hakuwa katika mji wa Mesa.
Kachero alipomuuliza itakuaje kama wakimuonyesha ushahidi kwamba alikuwa nyumbani kwa Travis, Joddi alijibu kuwa hakuwepo.
Kachero akamwambia inabidi awe mkweli, ila Joddi alizidi sisitiza kuwa hakuwa kwa Travis na ashawambia kuwa hakuwa eneo hilo.
Kachero akamwambia ulikuwa nyumbani kwa Travis, na mlifanya mapenzi tuna ushahidi wa picha.
Joddi akauliza una hakika hizo picha siyo za kipindi cha nyuma?
kachero akamjibu tuna uhakika usiyo na shaka ni za siku alipouawa Travis.
Hiki kipindi ilikuwa ni mwezi wa saba ndipo aliitwa kufanyiwa mahojiano, na Joddi alikuwa bado amengángánia kuwa hakuwa kwa Travis na mara ya mwisho walionana mwezi wa tatu.
Baada ya kugundua kuwa kuna ushahidi wa picha Joddi alijua kuwa kabambwa.
Kachero akamwambia umekamatika la kufanya ni kutwambia ukweli.
Joddi akajibu ukweli ni kwamba sikumdhuru Travis.
Kachero alimuacha Joddi kwenye chumba cha mahojiano na katika hali ya kushangaza wakiwa wanamtazama kwenye TV walimuona ameanza kufanya mazoezi ya Yoga huku akiimba mle chumbani.
Kwa muda huo Joddi alikuwa hajawekwa chini ya ulinzi alikuwa kaja kwa ajili ya mahojiano, ila makachero waliporudi walimkamata kwa kosa la kufanya mauaji ya Travis. Kesho yake alivyorudishwa katika chumba cha mahojiano Joddi sasa alibadirisha maelezo na kudai ya kwamba wakati akiwa na Travis walivamiwa na watu wawili ambao walianza kumshambulia Travis naye alishambuliwa akaumizwa kidole. Akiwa kalala kwenye sakafu akaona Travis anachomwa mara kadhaa kwa kisu. Akadai kuwa Travis alikuwa akipiga kelele akimwambia Joddi akimbie aende kwa majirani kuomba msaada.
Akadai kwamba hao wavamizi walibishana baina yao kuhusu kumuua Joddi ama kumacha hai.
Kachero alipomuuliza kwanini watake kukuua?
Joddi alijibu kwakuwa alikuwa shuhuda
Kachero akamuuliza shuhuda wa nini?
Jodi akajibu wa mauaji ya Travis.
Hii hadithi mpya ya Joddi alienda mbali zaidi kwa kuipeleka kwenye mahakama ya huruma ya raia miezi miwili mbili wakati akifanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha habari.
Alidai ya kwamba alishuhudia Travis akiwa anachomwa visu na avamizi ambao hawafahamu. Alizidi kudai hata polisi walipomletea picha ajaribu kuchagua watu hao anaodai walimuua Travis hakuweza kuwangámua. katika mahojiano hayo pia alidai kwamba anajua mahakama haiwezi kumkuta na hatia. Mtangazaji alipomuuliza kwanini, Joddi alijibu kwakuwa hana hatia na mtangazaji atakuwa shuhuda wa hiki anachokisema.
Kesi ya kuua dhidi ya Joddi
Mwaka 2010 miaka miwili baada ya mauaji ya Travis, wanasheria waliokuwa wanamtetea Joddi walifungua jarada lenye utata lilionyesha kwamba Joddi alikuwa aataka kubadiri taarifa yake ya awali aliyotoa juu ya ni nini kilitokea juu ya Travis. Katika ripoti hiyo Joddi alikubari kuwa alimuua Travis lakini alimuua katika harakati za kujilinda kakuwa Travis alikuwa anataka kumuua.
Lengo la mawakili wake ilikuwa ni kujaribu kuondoa mashtaka kuwa Joddi alipanga amuaji hayo ila aliua pasipo kukusudia wakati akijilinda. Mawakili wake walizidi kudai kwamba Joddi wakati huo ilimpasa afanye maamuzi ambayo matokeo yake ilikuwa kuishi au afe kwa kuawa na Travis.
Kama mjuavyo katika kesi ya mauaji, muaji anachotaka ni kupata huruma, ateke hisia za watu na mahakimu waone hakuwa na jinsi zaidi ya kutenda alilotenda hii husaidia sana katika mahakama kufikia uamuzi ambao utamnufaisha mshtakiwa. Na mara nyingi hutumika njia ya kumtupia lawama marehemu na kutengeneza taswira mbaya juu yake.
katika hii kesi upande wa utetezi ulianza kwa kubomoa taswira ya Travis aliyokuwa kaijenga kwenye jamii kwa kuleta shahidi ambaye ni binti aliyekuwa ni muumini na rafiki wa Travis.
Swali la kwanza aliloulizwa na wakili wa upande wa utetezi ni kwamba, Je katika imani yenu kufanya mapenzi kabla ya ndoa kunaruhusiwa?
Binti akajibu Hapana.
Kaulizwa, je Travis alikuwa akidai kwamba yeye ni bikra?
Binti akajibu, Ndiyo
Binti akaulizwa, Je alikuwa akijivunia kuwa bikra?
Akajibu ndiyo.
Hii yote ilikuwa ni kuonyesha jamii kuwa Travis hakuwa mtu yule ambaye alikuwa akijipambanua kwa jamii kuwa mcha Mungu alikuwa ana maisha yenye pande mbili
......................Itaendelea................
Mwenye kutaka kujisomea just Google Joddi Arias au Travis murder