GE2025 Ally Makame: No Reforms, No Election ni kauli ya kukwepa wajibu wa kisiasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADA-TADEA, Ally Makame, ameikosoa vikali kauli ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya No Reforms, No Election, akidai kuwa ni jaribio la kujipa mamlaka ya kipekee kisiasa na kupotosha mwelekeo wa taifa kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza katika mahojiano na Wilberforce Ngoto wa Jambo TV kupitia kipindi cha Maswali na Majibu, Makame amesema kuwa madai ya CHADEMA kwamba ni lazima kufanyike mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla ya kushiriki uchaguzi ni ya kibeberu na hayana msingi wa kidemokrasia.

Makame ameeleza kuwa hali ya sasa ya kisiasa nchini ni tulivu, na kwamba uchaguzi ujao unatarajiwa kufanyika kwa amani na utulivu bila masharti ya kisiasa yasiyo ya lazima.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akisisitiza umuhimu wa ushiriki wa vyama vyote kwenye mchakato wa uchaguzi, Makame amesema kuwa mageuzi ya kisiasa ni muhimu lakini hayawezi kuwa kisingizio cha kugomea chaguzi.

Kwani Tanzania uchaguzi inafanyika au kinachofanyika ni kupiga kura na siyo ichaguzi
 
Kitu wanachokitaka chadema ni sahihi ila kwa wakati mbovu mana watanzania pamoja na baadhi ya viongozi ni wajinga, kama ilivyo kwa JPM alikuwa rais sahihi kwa wakati mbovu mana watanzania na baadhi ya viongozi ni wajinga.
 
Si wanadi sera zao sasa, waachane na sera ya wenzao...wasimamie zao jamani haaa😛
 
Siasa za Tanzania ni za kipuuzi sana 😂

Chadema wanapambana na ccm, vyama vingine vinapambana na chadema, hapo anabaki ccm pekee yake hana vita mana ana turufu ya serikali hvy ni kama hana mpinzani anabaki kucheka tuu wapinzani wanavyoparuana.
 
N kama chadema tuu wanavyowaongelea ccm na kuacha sera zao
Vyama vya upinzani vyote..adui yao ni ccm wanatakiwa waelekeze mishale yote ccm😄 na sio upinzani kusengenyana wao kwa wao....adui yao ni yule aliyeshika Dola. Kama hawaelewi wanapigana na nani?.. chadema kidogo wanatambua...adui wao mkuu ni yule aliyekabidhiwa aongoze serikali ndio maana vita zote ni wao na serikali ya ccm😆
 
Tatizo la vyama vya upinzani ukimtoa chadema wao wanataka wapate huruma ya ccm ndo mana wanapambana na chadema na sio ccm.

Sasa na chadema ndo hvy hvy, badala ya kuongelea sera zao wao wanabaki kusukuma malengo ya ccm.

2020 yule Queen Sendiga aligombea urais kupitia ADC, unadhani lengo lake n kuwa rais? Huu ukuu wa mkoa ndo lengo lake na amefanikisha hilo.
 
Kweli ..
 
Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADA-TADEA, Ally Makame, ameikosoa vikali kauli ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya No Reforms, No Election, akidai kuwa ni jaribio la kujipa mamlaka ya kipekee kisiasa na kupotosha mwelekeo wa taifa kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza katika mahojiano na Wilberforce Ngoto wa Jambo TV kupitia kipindi cha Maswali na Majibu, Makame amesema kuwa madai ya CHADEMA kwamba ni lazima kufanyike mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla ya kushiriki uchaguzi ni ya kibeberu na hayana msingi wa kidemokrasia.

Makame ameeleza kuwa hali ya sasa ya kisiasa nchini ni tulivu, na kwamba uchaguzi ujao unatarajiwa kufanyika kwa amani na utulivu bila masharti ya kisiasa yasiyo ya lazima.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akisisitiza umuhimu wa ushiriki wa vyama vyote kwenye mchakato wa uchaguzi, Makame amesema kuwa mageuzi ya kisiasa ni muhimu lakini hayawezi kuwa kisingizio cha kugomea chaguzi.

Haya mambo ya ajabu sana.

Yaani hao hao waliofungwa miguu, mikono na midomo ndiyo wanapoteza muda kuwaongelea?

Wangekuwa makini wangejikita zaidi kwenye kuelezea sera zao ili wapate kueleweka na kuchaguliwa dhidi ya wenzao wanaoshiriki huo unaoitwa uchaguzi.

Hakuna sababu ya kupoteza muda kuongelea wale ambao hawashiriki kinachoitwa uchaguzi na pia wamefungwa midomo ili hata wasijibu chochote kinachosemwa kuhusu wao.

Ni aibu, ni wazi hawako tayari kwa ajili ya kulisimamia taifa.

They're not focused. 😞
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom