PostGE2025 Aliyeshauri Watu kuuliwa bila sababu za kueleweka ni nani?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

je parle

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
2,090
Reaction score
4,060
Tangu internet imeachiwa sijapata hisia za mwanamke kabisa yani Kila nikiona hizo videos mtandaoni watu wamekufa kama mbuzi yan

Sikudhani kama ingefika siku watanzania tukafanyiana vitendo vya kinyama kiasi hiki.?

Unaua tu hata kama umetumwa lakin pia askari muwe mnatumia hata akili za kawaida basi

Kwahiyo mkipewa tu amri piga huyo unapiga kama zezeta

Nimeumia mno. Nafikiria kudhani kuwa mh.alifanyiwa figusu ili achafuke kimataifa ,huenda kulikuwa na mpango mkakati wa kampa stress kama hizi ili a give up na kukaa pembeni kwa lazima

Kwa mana watu walikuwa wanauliwa bila sababu yan kuna gari maalumu zilikuwa zinapita na kupiga watu Risasi tena wala hawapo katika maandamano ni kuwa tu fujo zimeanza watu wanafunga biashara zao basi wao wanakulenga kwa kusudi tu.

Kama huku kwetu kuna gari ya polisi ilikuwa kazi yao ni kuua tu hata kama unafanya shughuli zako.

Ndio maana nasema huu ulikuwa mpango wa watu fulani kumchonganisha mh. Namba 1 na wananchi na umefanikiwa kwa 101.%
Mana mpaka sasa lawama zote zinapelekwa kwake na wakati yeye alikuwa ni mgombea kama wagombea wengine

Mheshima alipakwa mavi mheshimiwa alipakwa matope ili anuke Kila mahali

Waasisi wachama walitukosea watanzania kwa kuweka sera zao na maslahi yao tangia miaka ya 60 huko ila Athari yake tunaipata Leo

Kingine nimegundua sumu kubwa sana kwa watanzania bara kuwabagua wanzanzibar katika angle zao na linapokuja suala la maslah ya bara.

Wanzanzibar wanachukuliwa kuwa hawastahili kuwepo katika muungano huu.

Ilihali hata wao hawataki muungano na wanalazimishwa na pia walishawai pewa kesi za ugaidi na kuja kutumikia vifungo bara. Kama segerea na keko .Lakin Leo mzanzibar akipata nafasi kwa tanzania bara inakuwa nongwa kwa wenzetu upande wa pili. Lakin mzanzibar kutumikia kifungo segerea ni sawa.

Yote kwa yote mauaji ya Aina yoyote Yale hayafai tusichague vita ya kupigana.
 
Aliyeshauri watu wauwawe kwa kupigwa risasi na Samia Suluhu ambaye alikuwa akitamba siku zote kuwa yeye ñdiye Amiri Jeshi Mkuu.
 
elimu elimu elimu, hakikisha watoto unatoa elimu inayokidhi vigezo, hakuna kitu muhimu kama elimu
 
elimu elimu elimu, hakikisha watoto unatoa elimu inayokidhi vigezo, hakuna kitu muhimu kama elimu

..ukiwapa watoto elimu ya uhakika wakajitambua itakuwa shida kwani watakuja kuwindwa, kutekwa, na kupotezwa.

..Na ukiwaacha wasijitambue ndio wanaangukia katika kundi la watekaji, na wanaopoteza wenzao.
 
Unauliza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…