Aliyempigisha ‘deki’ Mwalimu aigomea CWT

very sad sio haki kabsa hivo ni kumdharirisha mwalim
 
Walimu ni watu wa kuwaheshimu sana, wametutoa mbali, wamekubali ukweli kwamba wao ni madaraja ya kutuwezesha kwenda upande wa pili. Uzalilishaji wao sio jambo la busara, matukio tu kila kukicha kila mtu anajifanya Mungu mtu.
 
Tatizo nafasi hizi walizopewa hawa makada wenzangu zinawapwaya.Wanapenda kwenda na matukio,wanaiga mkubwa anachokifanya!!Wanafikiri kudhalilisha walimu ndio kuwawajibisha,kumbe kuna tofauti kubwa sana ya kuwajibisha na kudhalilisha.

Uwajibishaji kwa mtumishi wa umma unaendana na sheria,kanuni na taratibu,wakati kudhalilisha kunaendana na matamko,mihemuko na sifa za kijinga.Eliud hana uzoefu wowote wa kuwa mkurugenzi tena kwenye halmashauri kama ya Misungwi.

Nafasi za Ukurugenzi sio nafasi za u-DC,ambapo unaweza muokota mtu hata barabarani na ukampa hiyo nafasi.Ukurugenzi wa Halmashauri ni nafasi nzito,inayomtaka mtu kuwa na uzoefu usiopungua miaka 10 ndani ya utumishi wa Umma,ili kumfanya mtu awe mzoefu na kanuni,sheria na taratibu za kuongoza.

Eliudi aligombea ubunge wa CCM kura za maoni jimbo la Mbeya Mjini,kigezo chake ni ukada na si uweledi,asipokemewa kwa hili la kundekisha mwalimu,ipo siku anaweza fika Hospital ya Wilaya akamtaka nesi amchambishe....CWT mkomalieni huyu mpaka ajifunze.
 
Kunahaja ya walimu kujitathimini upya na kujua maagizo halari yanayotolewa na wakuu wao! Sidhani kama wanapaswa kutekeleza kila agizo. Hii ni ishara kwamba viongozi wa juu ktk halmashauri na manispaa ndani ya kada ya Elimu wanaweza hata kutembea na walimu kwani inaonekana siyo wanaheshimiwa tu bali wanaabudiwa!!
 

Mbona kawaida sana, angewekwa lokapu sibora kudeki kuliko kulala ndani?, watanzania bana mambo mengine tunayakuza kweli, ni adhabu kama adhabu zingine jamani.
 
Kisha pigiwa simu ya kupongezwa?
Lazima atakuwa amepigwa.Tutasikia mengi.Aliambiwa akisema aliowachagua ndiyo majembe,sijui yakukokotwa na Ng'ombe au mkono
 
Mbona kawaida sana, angewekwa lokapu sibora kudeki kuliko kulala ndani?, watanzania bana mambo mengine tunayakuza kweli, ni adhabu kama adhabu zingine jamani.

You are not serious.Kama Mzazi wako ni mwalimu akifanyiwa hivyo hope utajibu ulichojibu.Bila Mwalimu asingekuwa hapo alipo.Ukiona wateuliwa wanafanya mambo ya ajabu basi ujue ni replica ya aliyewateua
 
Mbona sasa waheshimiwa mawaziri hawatoi matamko na kuchukua hatua kama walivyofanya kwa walimu wale wa field walivyokiuka taaluma zao?Yuko wapi Joyce Ndalichako,yuko wapi Simbachawene,Mwigulu pia yuko wapi?Walimu nchi hii wananyanyaswa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…