Aliyekuwa rais wa Marekani, George Bush alazwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Vyombo vya habari nchini Marekani vimesema kuwa aliyekuwa rais wa taifa hilo George Bush anapata matibabu katika hispitali moja ya Houston katika jimbo la texas.

Maelezo kuhusu hali yake hayajatolewa ,lakini mkuu wa wafanyikazi wake amenukuliwa akisema kuwa bw Bush aliye na umri wa miaka 92 yuko katika hali nzuri na kwamba huenda akatolewa na kwenda nyumbani katika siku chache zijazo.

Bush kama marais wengine wa zamani anatarajiwa kuhudhuria kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani Donald Trump katika sherehe itakayofanyika siku ya Ijumaa.
 
Bush kama marais wengine wa zamani anatarajiwa kuhudhuria kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani Donald Trump katika sherehe itakayofanyika siku ya Ijumaa.

Hapana.

Bush 41 hatahudhuria kwa sababu za kiafya.

Na hiyo ilitangazwa mapema kabisa.

Atakayehudhuria ni Bush 43.
 
Kwani Trump alitangaza kuwatumbua marais wa zamani waliotumia ofisi vibaya?! (Joke)
 
_93656412_4e239859-6892-4231-9051-d752ebe51b61.jpg

Rais mstaafu wa Marekani George HW Bush aliyekuwa amelazwa hospitalini huko mjini Texas tangu Jumamosi, amepelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Baada ya kutibiwa ugonjwa wa homa ya mapafu, Bush mwenye umri wa miaka 92 sasa anaendelea vizuri.

Mke wake Barbara, amelazwa katiaka hospitali hiyo hiyo kama tahadhari kwa sababu ya uchovu.
 
Bush ana miaka 92 na anaonekana amechakaa
Mzee Mwinyi ana miaka 911/2 lakini anaonekana bado yuko fit.
 
bush ndo kavimba hivi bujibuji?
 
Bush ana miaka 92 na anaonekana amechakaa
Mzee Mwinyi ana miaka 911/2 lakini anaonekana bado yuko fit.
Afya, uzima, umri, na siha ya binadamu viko mikononi mwa Muumba; binadamu hana control navyo hata chembe; ni majaliwa yake Mola. Hakuna "jitihada" alizofanya Mzee Mwinyi kuwa kama alivyo wala hakuna "kosa" alilofanya Bush kuwa kama alivyo. Ndio maana binadamu afe at 40, 50, 60, 70, 80, 90, 100, 110, or at any other age hakuna wa kulaumiwa wala kusifiwa kwa lolote - yote "anaachiwa" aliyeumba.
 
Ali Hassani Mwinyi huyu mzee Mmungu kampa umri wenye afya na siha njema kabisa.

Anaonekana ni mtu asiye na Majigambo wa maringo na mwenye kuridhika na hali yeyote....moyo wake upo na amani.... hana stress yyto na mweny kumhofu mmungu ...umri alio kuwa nao na hali aliye kunayo aziwiyani kabisa hii ni zawadi kutoka kwa GOD kwel kabisa 92yrs Old sio mchezo jamani ..
Mmung ampe Umri mrefu zaid na wenye Afya njema kabisa inshl.
 
Back
Top Bottom