Aliyekuwa Mhasibu Tabora kukiona | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyekuwa Mhasibu Tabora kukiona

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 10, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeuagiza mkoa wa Tabora kumtafuta aliyekuwa mhasibu mkuu wa mkoa huo katika kipindi kilichoishia Oktoba 30, mwaka jana ili aweze kuadhibiwa na ikiwezekana kushushwa cheo kutokana na kuacha hesabu kiholela.

  Mwenyekiti wa kamati hiyo, John Cheyo ametoa agizo hilo kwa Katibu Tawala wa mkoa huo wa Tabora (RAS), Kudra Mwinyimvua, na amekataa kupokea hesabu za mkoa huo na kuagiza ifikapo Oktoba 31, mkoa huo uwe umewasilisha maelezo ya kina kuhusu fedha zote zilizotumika bila kuwa na maelezo ya kujitosheleza.

  “Nawaagiza huyu mhasibu ambaye nasikia amehamishiwa Lindi atafutwe na kuwajibishwa na ikiwezekana pamoja na kushushwa cheo alipe fedha zote ambazo hazina maelezo ya kuaminika, na hili tunataka liwe fundisho kwa wahasibu wote wanaoharibu katika eneo moja na kujiiificha katika kivuli cha uhamisho, kamwe hatutawavumilia tutawafuata huko huko waliko,” amesema Cheyo.

  Amesema, hesabu za mkoa huo za mwaka wa fedha wa 2010/2011 kwa mujibu wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Kanda ya Magharibi, fedha nyingi zimeonekana kutumika bila kuwa na maelezo ya kuthibitisha matumizi hayo ambapo alitolea mfano wa Sh milioni 196 hazina maelezo, Sh milioni 11 za vocha ambazo hazionekani pamoja na Sh milioni nane ambazo zinaonekana zimetumika lakini hakuna mrejesho wa matumizi yake.

  Cheyo amesema , kwa kuwa RAS wa sasa ni mgeni na hahusiki na mahesabu hayo hivyo anaupatia mkoa huo muda hadi Oktoba 31 wawe wameleta maelezo ya kutosha kuhusu matumizi ya fedha hizo ambapo pia kamati hiyo itaiandikia Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kuhakikisha kuwa mhasibu huyo anatafautwa na kuchukuliwa hatua.

  Awali Mwinyimvua alipotakiwa kutoa sababu za mkoa kupatiwa hati yenye mashaka alisema tatizo ni upungufu wa wahasibu katika ofisi yake ya RAS ambayo kwa kawaida ilitakiwa kuwa na wahasibu 12 lakini kwa sasa wapo nane.

  “Tatizo ni uhaba wa watumishi wa fani ya uhasibu katika ofisi ya RAS, lakini tumeshawasilisha taarifa kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Tamisemi.

  Hata hivyo utetezi wake haukukubaliwa na kamati hiyo, ilihoji taarifa za hesabu za miaka mingine katika mkoa huo ambazo zilitolewa na wahasibu hao nane inakuaje katika hesabu za mwaka jana ndiyo kuwe na hitilafu.

  “Ndiyo maana nasema pamoja na maagizo yangu mengine imarisheni kitengo cha ukaguzi wa ndani kwa kuwa kilichopo kimeonesha kuwa na udhaifu" amesema.
   
Loading...