Kwa hiyo CHADEMA haina wagombea mpaka wakaazime kwa majirani (CUF vs CCM)!Haina shida. Ililazimu kuhamia cdm kutimiza masharti ya sheria za uchaguzi. Haimaanishi alikuwa ameasi au kufukuzwa CUF. Sheria za tz ni tofauti na nchi zingine kama Kenya ambako mgombea urais na mgombea mwenza wanaweza toka vyama tofauti. Kwa tz mgombea na mgombea mwenza lazima watoke chama kimoja. Big Up Hon. Duni. Mapambano dhidi ya miccm lazima yaendelee. Wanaofikiri CUF itakufa kwa kukosa wawakilishi znz wasahau.
Hizo sheria zikikwepo tangu na tangu na vichama vyenu vikaingia kwenye uchaguzi kwa sheria hiyo hiyo. Ilikuwa ni busara kuzungusha akili sheria ifanyike marekebisho kuliko kuzungusha mikono.Kuna mi-CCM inabeza wakati haijui hata sheria mbovu ya uchaguzi ya nchi inasemaje.
Kwa hiyo wewe hushangai Chama kikongwe cha upinzani hakina wagombea urais?Nashindwa kujua watu wanashangaa nini!