Aliyekuwa meya wa Ilemela, Henry Matata afikishwa Mahakamani Kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mwanza, imemfikisha mahakamani aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata (63) na wenzake wawili wakikabiliwa na mashitaka ya kutumia vibaya madaraka.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo waliofikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Nyamagana ni aliyekuwa Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Justine Lukaza (42) na mfanyabiashara Hemedi Hamad (54).

Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Mwema Mella, alidai mbele ya hakimu Greyson Sumaye kwamba kati ya Juni mosi na Julai 31, mwaka 2014, washitakiwa hao walitumia vibaya madaraka kwa kutoa zabuni ya kutoza ushuru katika Kituo cha Mabasi cha Buzuruga kinyume cha utaratibu.

Alifafanua kuwa makosa waliofanya ni kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mamba 11/2007 na pia walikiuka sheria ya manunuzi ya umma namba 7/2011

Wakati kesi hiyo inafikishwa mahakamani jana, mshitakiwa Lukaza hakuwepo, hatua iliyomfanya Mwendesha Mashitaka kuomba mahakama hati ya kumkamata.

Hakimu aliridhia ombi hilo na kesi hiyo ilioahirishwa hadi Machi 29 mwaka huu. Washitakiwa wawili waliokuwepo mahakamani walikana mashitaka hayo na wako nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
 
Huyo meya ni jipu afadhali alipofikishwa kwa pilato na labda akili itamrudia na ndio ajue kuwa usaliti mwisho wake ni kusalitiwa
 
Hii ndio FAIDA ya kutumika kama DODOKI. Waliomkingia kifua na waje sasa wamteetee. Aibuuuuuuuuuuuuuuu! matata kweli kweli.
Matata ni kati ya wasaliti wakubwa wa siasa za upinzani jijini mwanza mwache aisome namba na hapo bado ile hotel yake siku ikipigwa chini ndio ataijua laana ya usaliti
 
Back
Top Bottom