Aliyekuwa Katibu Mtendaji wa TCU afunguka kuhusu kusimamishwa kwao kazi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,641
22,017
Aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

Mgaya ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo vya uhakika katika habari zao.

“Mimi nikiwa miongoni mwa watendaji waliopumzishwa kazi, napenda kueleza kuwa sihusiki na taarifa hizo, suala hili limeshapita na kutolewa uamuzi na serikali na tuiache Tume iendelee kufanya kazi,” alisema Profesa Mgaya alipozungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kukabidhi ofisi.

Aidha, Profesa Mgaya aliweka wazi kuwa, anaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata elimu ya msingi bure na kutolewa kwa elimu inayokidhi viwango stahiki kitaifa na kimataifa na kusema jambo hilo ni jema na linapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote.

Katika hatua nyingine, alimtaka Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi , Profesa Joyce Ndalichako kuendeleza jitihada za kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote ili kuwa na taifa lenye watu walioelimika vizuri na lenye mchango mkubwa katika kuendeleza taifa.
1.jpg
 
Ninachokiona Tz ya sasa ni kuwa waandishi wa habari au vyombo husika vya habari vimekuwa na uzembe kupindukia ktk kutafuta habari kutoka kwenye vyanzo. Vyombo vingi vimekuwa kama magazeti ya udaku, yaani yanaripoti tetesi na kuzifanya kuwa breaking news na wanaweka kwenye kurasa kabisa za mbele
 
Wasomi wa nchi hii shida sana!Yalioandikwa si ya siri bali yanajulikana kwani ni mambo yaliyopangwa na kufanywa na serikali iliyopita na waandishi wanayajua sasa kurudia kuyaandika leo hii ili kukumbusha umma ndio iwe kosa?
 
Ninachokiona Tz ya sasa ni kuwa waandishi wa habari au vyombo husika vya habari vimekuwa na uzembe kupindukia ktk kutafuta habari kutoka kwenye vyanzo. Vyombo vingi vimekuwa kama magazeti ya udaku, yaani yanaripoti tetesi na kuzifanya kuwa breaking news na wanaweka kwenye kurasa kabisa za mbele
Sio uzembe,
Ni elimu ndogo na ajira wanapeana mtoto wa mjomba kamaliza diploma mpeni kazi anapewa na matokeo yake ndio haya
 
Prof. Kawaumbua waandishi wa habari, na wale wote waliochangia kusupport yaliyoandikwa na magazeti

Kawaumbua waandishi kwa kusema kuwa hahusiki na taarifa zilizoandikwa magazetini kuhusu utaratibu wa kutumbuliwa kwao? Kwani ulitarajia aite waandishi wa habari na kusema yeye ndiye anahusika na taarifa hizo? Au unatarajia wenzake waje kusema wao ndio wanahusika? Kwa nini anajishtukia? Kama hahusiki na hizo taarifa akae kimya. Anatia mashaka. Na kimsingi anadhalilisha hadhi ya maprofesa. Kwa maoni yangu, huyu ndugu hana tofauti na yule Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyetumbuliwa na kuanza kulialia. Professor mzima unaacha kwenda kufundisha na kufanya tafiti unakuja kukanusha kitu ambacho hakina kichwa wala miguu. Hoja ni kwamba taratibu/sheria zimekiukwa. Kama taratibu/sheria zimekiukwa, itabaki kuwa hivyo bila kujali kwamba aliyetoa taarifa za kukiukwa kwa taratibu/sheria ni Prof. Mgaya au la. Kwa nini hasemi kuwa taratibu zote zilifuatwa? Kimsingi, anajipendekeza ili ateuliwe tena kwenye nafasi nyingine. Hovyo sana.
 
Hahahahaha! Neno KUFUNGUKA maana yake hapa Tanganyika ni tofauti na Kenya, au Uingereza.
 
Taratibu zipi (zitaje) ziluzokiukwa?
 
Aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

Mgaya ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo vya uhakika katika habari zao.

“Mimi nikiwa miongoni mwa watendaji waliopumzishwa kazi, napenda kueleza kuwa sihusiki na taarifa hizo, suala hili limeshapita na kutolewa uamuzi na serikali na tuiache Tume iendelee kufanya kazi,” alisema Profesa Mgaya alipozungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kukabidhi ofisi.

Aidha, Profesa Mgaya aliweka wazi kuwa, anaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata elimu ya msingi bure na kutolewa kwa elimu inayokidhi viwango stahiki kitaifa na kimataifa na kusema jambo hilo ni jema na linapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote.

Katika hatua nyingine, alimtaka Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi , Profesa Joyce Ndalichako kuendeleza jitihada za kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote ili kuwa na taifa lenye watu walioelimika vizuri na lenye mchango mkubwa katika kuendeleza taifa.View attachment 352347

Profs anaonekana njaa tuu inamsumbua
 
unategemea habari nzuri na za kiutafiti zitatoka wapi ikiwa waandishi wetu ni makanjanja na wenye elimu za hapa na pale akina kubenea type?
 
Ninachokiona Tz ya sasa ni kuwa waandishi wa habari au vyombo husika vya habari vimekuwa na uzembe kupindukia ktk kutafuta habari kutoka kwenye vyanzo. Vyombo vingi vimekuwa kama magazeti ya udaku, yaani yanaripoti tetesi na kuzifanya kuwa breaking news na wanaweka kwenye kurasa kabisa za mbele
mkuu tatizo waandishi wengi wa habari wamekuwa ni wanaitikadi na wafuasi wa kisiasa KUBENEA TYPE.wanaandika habari zinazopendwa na wafuasi wao tu tena habari hzo wanazichapisha bila hata utafiti wowote. hatar sana
 
Njaa hiyo daaah kama prof anahitaji huruma sijajua kwa undergraduates mm namsifu sana yule jamaa wanacte aliejitumbua mwenyewe
 
Back
Top Bottom