Aliyekuwa dhaifu, mpole kwa kushamirisha ufisadi kila kona na huyu mbabe kwa lugha kali, tata na ngumu kwa kushamirisha hofu kila kopo yupi bora?

Jul 23, 2018
41
30
Namsikiliza mheshimiwa akiwa live huko Serengeti.

Dah lugha inayotumika kama hujamzoea unaweza sema basi leo viongozi wa mkoa huo hawana bahati. Lakini nashindwa kujua kama iko siku mambo yanaweza kubadilika kwa mheshimiwa kuja kuwa na lugha za staha kama ambavyo inategemewa kwa nafasi yake.

Lakini pia kama haya yote yana msaada ktk kudhibiti mambo mabaya kwa nchi yetu pengine si vibaya tukasema ukweli tunaumizwa na lugha tu si mbaya kama kuumizwa na ufisadi na ubabe wa matajiri kila kona ya inchi hii.

Bora kuwa na mbabe mmoja kuliko wengi waliopata mihela michafu kwa njia wanazojua wao waliokuwa hawagusiki asilani.
 
Aliye bora sio mkali wa mpole, aliye bora ni mimi na wewe kwani sisi ndio waajiri wa hao wawili.

Ni kupoteza muda kulinganisha hawa watu wawili ambao wanaishi kwa kodi zetu. Aliyebora ni mtu anayeweza kuiona fursa ya maendeleo mahali ambapo watu wanaliona jangwa lisilo na maji au uhai.

Aliyebora ni yule anayeweza kuona fursa ya maendeleo mahali ambapo kazungukwa na walevi na wavivu.

Aliyebora ni yule anayezitumia rasilimali tulizojaaliwa na Mungu kwa manufaa yake na wote wanaomzunguka.

Kuna mtaliano mmoja miaka kumi iliyopita kurudi nyuma kule bandarini, alikuwa na vespa tu, lakini ndani ya miaka mitano akawa tajiri mkubwa.

Aliona fursa ya usafirishaji wa makontena kupeleka bandarini, wakati wabongo wengi walikuwa hawaoni kitu. Aliyebora ni yule mbunifu na wala sio hawa wanasiasa wanaoishi kwa kodi zetu.
 
Unajua muda mwingine unaweza ukajifanya mkali lakini uka jeoperdize position ya dhamana uliyopewa na wale unaowaongoza na pia kulitia taifa hasara.

Upole na hivyo hivyo kama ukali. Unaweza kufanya maamuzi kwa kutokana na kujiona kwako mwamba au kujiona una huruma sana lakini mwisho wake ya backfire.

Mifano ipo mingi na itaendelea kutokea wala sihitaji kuieleza au kuitaja. Kama ni mfuatiliaji utaelewa na natumaini unaifahamu.

Cha msingi ni mtu kukubali ukweli mchungu kuwa hakuna binadamu aliekamilika hivyo kusikiliza ushauri ni jambo la busara. Kufanya maamuzi kuendana na hisia zako na matakwa yako kuna mipaka ya mahali na mahali. Kwa nafasi ya raisi ni nyeti sana na inabidi mtu uwe na busara sana. Ujue kuwa kuna kokosea, kukosolewa, kupendwa, kuchukiwa n.k.

Unatakiwa ujifunze tu namna ya kiungwana na ya kidemokrasia ya ku deal na hayo yote.

Unfortunately kwa sasa sioni hali hii ikiwepo.
 
Bora dhaifu. Kipindi chake tuliuza vijishamba /viwanja vyetu, na vibiashara vingine tukaweka mkono kinywani.

Awamu hii hakuna mnunuzi, hali ni tete.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom