Aliyeitoa CHADEMA kwenye uanaharakati ni Dr. Slaa

Kidamva

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,578
1,984
Kumekwa na maneno mengi ya shutuma kwa aliyekuwa mgombea urais Wa Chadema, Edward Lowassa kutkana na ushairi wake Wa kuitaka Chadema iachane na uanaharakati.
Maneno haya inawezekana yanatolewa na wana CCM wasiotakia mema Chadema au wana Chadema wasioelewa au hata kuwa na kumbukumbu ya chama chao.
Mwanzilishi wa kuitoa Chadema kwenye uanaharakati alikuwa Dr. Wilbrod Slaa aliyekuwa Katibu Mkuu wakati huo.

Gazeti la Mwananchi la July 16, 2014, linaandika.

"Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kimeweka bayana
mkakati wake mpya wa kushika dola kwa
kukita mizizi yake tangu ngazi ya shina hadi ya Taifa.
Mkakati huo, ambao Chadema ilisema
unalenga kukiondoa chama hicho kutoka
kwenye uanaharakati na kukifanya kuwa
chama cha dola, umekuja wakati nchi
ikijiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari
makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema chama hicho tayari kimeunda matawi 196,000 kati
ya 250,000 yanayokusudiwa.
“Chadema imeshajiondoa kwenye harakati na kwenda kuwa chama dola. Tumefanya harakati kwa zaidi ya miaka 20 tukiwa na lengo la kukipeleka chama kwa wananchi, ili wakielewe na wakiheshimu, lakini sasa umefika wakati wa kujiandaa kushika dola,” alisema Dk Slaa.

Kwa hiyo Lowassa sio Wa kwanza kutoa ushauri huo. Cha ajabu wanaomshutumu Lowassa wanasema eti, afadhali alipokuwepo Dr. Slaa. Kweli watu ni wasahaulifu au wameamua kwa makusudi kuivuruga Chadema.
 
Back
Top Bottom