Aliyebambikiziwa kesi na polisi abainika kuwa mkora

Nafikiri hii inaonyesha kwa nini ni muhimu kuwa na kitengo maalumu kuchunguza matendo tata ya Polisi. Kuwaacha polisi kujichunguza hakutoi haki.
Mkuu upo sahihi.

Kwa statements kama hizo tena toka kwa msemaji wa polisi, tutegemee haki ingelitendeka kweli katika ufuatiliaji wao bila ya shinikizo toka Ikulu?

Ingekuwa busara na nidhamu kama wangelinyamaza kabisa kimya.

Hii inaonesha utovu wa nidhamu kiasi gani wanaufanya kwa commander in chief wao.

Yaani issue moja, mkuu anasema na wao wanasema!

Mada ni kubambikia mtu kesi, wamebambika hawajabambika?

Hayo mengine ni porojo tu, kama members wanavyosema ni 'kutaka kutakatisha kosa'.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JESHI la Polisi limesema linafanya uchunguzi dhidi ya mfanyabiashara Mussa Adam ambaye limebainika lilimbambika kesi ya mauaji.

Limedai kuwa wakati linawachukulia hatua baadhi ya askari wake walioshiriki kumbambika kesi, uchunguzi wa awali dhidi ya mfanyabiashara huyo umebaini ni mkora.

Wiki iliyopita, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ilieleza kuwa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi mkoani Tabora walimbambika kesi ya mauaji mfanyabiashara huyo.

Akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Ahmed Msangi, alidai mfanyabiashara huyo ni mkora.

Alidai alishafungwa miaka 20 jela kwa kosa la kubaka, alishaiba mahali na kukimbia na pingu na tukio la mwisho lililomfanya atiwe mbaroni na polisi na kubambikwa kesi ya mauaji, ni la wizi wa simu ya mwanamke kwenye kituo cha mabasi ambako alipigwa hadi kuvuliwa shati.

Msangi alidai mfanyabiashara huyo ni mtuhumiwa kama wengine, hivyo Jeshi la Polisi linamchunguza na akibainika kutenda kosa, atafikishwa mahakamani.

"Kilichoibuka hapa ni kitendo cha baadhi ya askari kumbambika kesi ambayo nayo tunachunguza ili nao wachukuliwe hatua," alisema.

Msangi aliongeza: "Lakini huyu mtuhumiwa naye ukweli ni kwamba siyo mtu safi, ni msumbufu kwenye jamii, ameshafanya matukio kadhaa.

"Pamoja na ukora wake, polisi hawakutakiwa wafanye walichokifanya (kumbambika kesi ya mauaji).

Walitaarifiwa kuwa kuna mtu amepigwa sana huko mtaani, walipofika walimkuta kweli akiwa katika hali mbaya, amepigwa hadi kavuliwa shati, kosa lilikuwa ni wizi wa simu ya mama mmoja, ambaye hata hivyo aliipata baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa.

"Bado ofisa wetu aliyetumwa kwenda Tabora kupeleleza tukio hili yuko huko anaendelea na kazi. Anapeleleza tukio la polisi waliodaiwa kumbambika kesi mtu huyu, lakini pia mtuhumiwa naye anachunguzwa kutokana na kosa au makosa yaliyomfikisha polisi, akibainika ameyatenda, atafikishwa mahakamani kama watu wengine."

Wiki iliyopita, Msangi akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa taarifa za awali zimeonyesha mfanyabiashara huyo alionewa kubambikwa kesi ya mauaji na baadhi ya askari polisi.

Msangi alisema jeshi hilo lilipokea barua ya malalamiko kutoka kwa mfanyabiashara huyo ndipo Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ilimtuma ofisa wake mwenye cheo cha juu kwenda Tabora kufanya uchunguzi.

Huu ni uongo. Sasa hiyo miaka 20 aliyofungwa aliimaliza lini? Kama alikamatwa kwa wizi wa simu kwa nini aliambiwa kavunja nyumba na kuiba halafu baadaye kesi ya mauaji???? Wanajichanganya tu hapa. Na vitu vyake anavyodai ilikuwaje? Au ndiyo mbinu ya kutompatia vitu vyake? Mtu kakamatwa kwa wizi wa simu, kapigwa sana hadi karibu ya kufa lakini anafika polisi na laki saba na vitu vyake vya biashara alivyonunua viko intact pamoja na yeye mwenyewe aliyepigwa sana.Haya ya ukweli??? Hela na vitu havikuibiwa wakati anapigwa!!! Alifikaje polisi akiwa msafi tu pamoja na vitu vyake na fedha wakati kapigwa sana na polisi ndiyo walienda kumuokoa? Kwanini hamkumfungulia kesi ya wizi wa simu? Kifungo cha miaka 20 kamaliza lini? Mnambambikia kesi nyingine tu hapa. Msangi acha kuongopa. Watanzania tuna akili ya kuhoji mambo.
 
[QUOTE="miss zomboko,

"Bado ofisa wetu aliyetumwa kwenda Tabora kupeleleza tukio hili yuko huko anaendelea na kazi. Anapeleleza tukio la polisi waliodaiwa kumbambika kesi mtu huyu, lakini pia mtuhumiwa naye anachunguzwa kutokana na kosa au makosa yaliyomfikisha polisi, akibainika ameyatenda, atafikishwa mahakamani kama watu wengine."

.[/QUOTE]
Huyu ofisa mliyemtuma alitokea wapi MAKAO MAKUU DAR/DOM?
Hivi huko tabora jeshi halina maofsa wa kushughulikia hili kosa mpaka ofisa atoke Dar/DOM?
 
Mkuu upo sahihi.

Kwa statements kama hizo tena toka kwa msemaji wa polisi, tutegemee haki ingelitendeka kweli katika ufuatiliaji wao bila ya shinikizo toka Ikulu?

Ingekuwa busara na nidhamu kama wangelinyamaza kabisa kimya.

Hii inaonesha utovu wa nidhamu kiasi gani wanaufanya kwa commander in chief wao.

Yaani issue moja, mkuu anasema na wao wanasema!

Mada ni kubambikia mtu kesi, wamebambika hawajabambika?

Hayo mengine ni porojo tu, kama members wanavyosema ni 'kutaka kutakatisha kosa'.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa Amiri Jeshi mkuu. Wangenyamaza to badala ya kutaka kuhalalisha uovu wao kwa kunyesha makosa aliywai tenda 'mtuumiwa'!
 
Back
Top Bottom