NALO LITAPITA
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 333
- 90
Wakuu,nimeamua kuja na jambo japo kuna watakaoniona tofauti. Nianze na ku declare intarest mi nimiongoni mwa waliohudhuria taifa pale na pia sikufanikiwa kuitwa katika orsl. Pia uchambuzi wangu hautaguza upendeleo ulioonyeshwa kwa watoto wa viongozi hili pia limenisikitisha.Nitajikita zaidi kwa ule usahili wa uwanjani. Wakuu uhamiaji wamerushiwa mawe mengi tukama wao ndo waliosababisha uhaba wa ajira hebu tutafakari yafuatayo. (1) Binadamu inawezekana in nature niselfish.Nafasi 70 zimetangazwa ni wazi tupo wengi wenyedegree, nani hakujua tutaomba wengi?.(2) ni wazi wenye vigezo tulikuwa wengi lakini tunasema wangeita wachache ni nani kati yetu angekuwa wa kwanza kukubali hasihudhurie kama ingesemwa wengi tumetimiza sifaila hapatikane wa kupungua?hapa napata wazo kuwa wengi wetu maombi yalikuwa hivi MUNGU NAOMBA NIITWE ILA TUITWE WACHACHE.(4) mfano ikatokea bunge letu wakaguswa na kilio juu ya uhamiaji wakatunga sheria kuwa kuanzia sasa usahili wowote ule uwe na ratio ys 1;3 nani wa kwanza kuikubali?Nina hakika sisi wenyewe tutaanza upya kuwa bora tuitwe tujaribu mbele kwa mbele. KUMBUKA NALO LITAPITA