Pamoja na kuwa na hoja na maono tofauti kuhusiana na "SAKATA LA RUSHWA YA WABUNGE WA ARUSHA", ukweli mmoja muhimu ni kwamba EL ANAHUSIKA lakini na hao waliokamatwa pamoja na kuwa mahakama itaamua, nao pia si WASAFI, suala la kama wametoa ama hawajatoa rushwa linaweza kuwa gumu kuthibitisha lakini haina shaka kabisa kwamba walitoa rushwa. LAKINI JE NI WAO PEKEE KATIKA CCM WALIOTOA RUSHWA? Jibu ni HAPANA KWANI HATA HAO WAKUBWA WANAENDELEA KUTOA RUSHWA AKIWAMO EL, ZIARA YAKE MWANZA ALIKUA AKIKUTANA USIKU NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU KUTOKA SHINYANGA, MWANZA, MARA NA KAGERA KUWASHIKISHA.
LAKINI KWANINI BASI WEMEKAMATWA HAO. KUNA THEORY NYINGI LAKINI NILIZOKUTANA NAZO NI KAMA IFUATAVYO:
1---Kwanza wanasema EL alikerwa na kauli kwamba yeye anatoka ukoo wa NDOSI, ni familia ya marehemu Meja Ndosi, kwa hiyo WAMASAI (MOLOIMET, LAIZER, POROKWA etc WAMEWEKA WAZI KWAMBA, EL ni MMERU na si MMASAI, jambo ambalo limemkera sana bwana mkubwa.
2---Pili mbali ya Moloimet, wanasema Mwenyekiti wa Vijana mkoa wa Arusha, Ole Porokwa ndiye kijana anayetajwa kuwa anatakiwa kugombea jimbo la Monduli na mwaka 2000 na 2005 alikataa kujitoa hadi alipotolewa kuwania jimbo hilo. Lakini pia Binafsi nina ushahidi wa POROKWA wa barua yake ya mwaka 2004 abayo alimuandikia Katibu Mkuu wa CCM wakati huo, Philip Mangula, na nakala kumpelekea Mwenyekiti Mkapa, akilalamikia kwamba aliitwa nyumbani kwa LOWASA kusutwa kwanini hamuungi mkono yeye na rafiki yake JK katika harakati zao za urais mwaka unaofuata (2005). Katika barua hiyo niliyoipata mwaka huo (2004) Porokwa alisema kwamba EL alimwambia, "UNAJUA KIJANA wewe na wenzako wa Mara na Dodoma muligharamia na kuchochea vijana pale Dodoma kutusaliti wakati wewe tunatoka kumoja...Mimi nasema Mkapa tumeshakubaliana naye kwamba JK atakua RAIS na mimi nitakua PM, kwa hiyo amua kutuunga mkono ama kuendelea, lakini ujue tutakushughulikia. Mwenzako MAra tumeshaanza kumshughulikia."