Ni miaka 2 sasa tangu nilipopigwa chini na mpenzi wangu niliyempenda sana, nilikuwa namtimizia mahitaji karibia Yote hata kwao nilikuwa najulikana kwa wazazi wake.
Ghafla akabadilika kama kinyonga akaniambia tuachane ameshapata jamaa mwingne bora zaidi yangu, kiukweli niliumia sana nilipojaribu kumbembeleza ndipo alipoanza kuniporomoshea matusi mazito na kejeli ikabidi kidume niwe mpole tu sikutaka kufanya lolote, nikapiga moyo konde maisha yakasonga.
Cha ajabu na kushangaza juzi alinipigia huku akilia ananiomba msamaha kwa yote aliyonifanyia anadai ulikuwa ni utoto na vishawishi kutoka kwa rafiki zake na dadake zake, mimi nikamwambia sirudii kula matapishi nikakata simu.
Jana amekuja home ameganda kwenye mlango huku analia tu nikijaribu kutoka nje anang'ang'ania mguu machozi kibeseni.
Msaada jamani nimfanye nini huyu msaliti? Sababu hata mama anasema nimsamehe nirudiane nae atakuwa amejifunza kutokana na makosa.
NB: Hivi wanawake ni nini haswa huwa mnahitaji? Maana hamueleweki kabisa.